Obugwa Izoba
JF-Expert Member
- Nov 16, 2013
- 9,961
- 10,427
Kila mtu anajua mwenyewe na ndoa yake
🤣🤣🤣kazi yangu ni moyaaa akili tunatumia zakeSio kweli bwana...
Kila mtu ana sababu ya kumpenda mtu aliyenae...jamaa anafaidi utundu wa kihaya🤣🤣
Mkuu shkamooSwali zuri sana..... nami naomba kujibu kama ifuatavyo, ndoa sio tendo la ndoa tu, sasa ukiacha tendo la ndoa yapo yafuatayo:
1. Ulinzi wa mali zako, mwanamke aliye mke wako atajitahidi kulinda mali zako huku akifikiria kuna kesho maana yake anawaza future ya maisha yenu, wengi wakiambiwa kuna kesho huwa wanawaza labda kufa, hata usipokuwa kesho inakuja.
2. Anakupatia watoto, hii unaweza sema aah! nitazaa huko nje, mke akizaa anakuwa na kiu ya kuongeza uzao wako na anawatunza watoto kwa mapenzi yote kwa sababu anajua mume wake uko pembeni, kumbuka kuzaa sio kazi, kazi kulea mwana.
3. Mwanamke ataunganisha familia, kiuhalisia kuna familia ndugu hawaelewani, uwepo wa mke anakuwa mtu kati(mediator) na hapa upate mke sahihi wengine wanakuja kugombanisha.
4. Mke ni msaidizi wa mwanaume, na hapa sio usaidizi wa kazi za ndani noo, ni kumsaidia mwanaume kutimiza malengo yake, kumbuka malengo ya mwanaume ndo huwa malengo na msimamo wa familia, mwanamke hawezi kuja na ya kwake lazima atasimama na kumsupport mume, kumbuka hakuna mwanamke atapenda kusemwa kwamba hapo shost ulikosea kuchagua, kwahiyo hata kama mwanaume hayuko njema kiuchumi, atasaidiwa, tuna mifano kuna wanaume hata mahari walisaidiwa na wake zao.
5. Mke anakuletea Heshima katika jamii, sio heshima tu na kuaminika, kuna nyumba ukienda kupanga hujaoa au kuolewa huruhusiwi kwanini unaonekana huna heshima, huwezi kuwa Raisi wa nchi hii hujaoa, ukiachana Katoliki mengine huwezi kuwa Askofu hujaoa: Kiufupi kama haujaoa au kuolewa unawekwa kundi la wahuni, kama ndugu zangu kataa ndoa
Marhaba mkuuMkuu shkamoo
Umesema sahihi MkuuHaya maneno ya hekima kabisa Toka Kwa wazee.
Vijana wanaoa Kwa msukumo wa kupata tendo la ndoa, kosa kubwa sana hilo, hautaweza kuona thamani ya mke kama tendo la ndoa ndio kipaumbele chako.
Mke asipokua Rafiki Yako na msaidizi wako hata hayo mambo ya utelezi hayatakaa sawa.
Hatupishani sana Mzee mwenzangu, swala la malezi ya watoto, uangalizi na usimamizi wa baadhi ya mambo.
Kingine ananipa changamoto za kuendelea kupambana zaidi.
Kadri muda tunavyozidi kusogea, tendo la ndoa linakua sio kipaumbele sana.
Mzee wa kazi mbona kama unataka kuunda bomu ili limlipukie jamaa🤣🤣Hata wewe ujapata mtu sahihi, unajidanganya tu, Kama unabisha nunua simu ya Huawei P9 niletee nii set and mpe mkeo kwenye birthday yake!
Hapana atatangulia yeye,Binafsi Mke wangu ni Msaidizi wangu kwenye mambo mengi, mathalani;
Ananisaidia kusimamia baadhi ya miradi tuliyoanzisha pamoja (Nafanya hivi Kwa kujua kwamba nitawahi kufa kabla yake, hivyo Jukumu la kulea watoto litabaki kwake).
Anasaidia malezi ya watoto wetu
Anasaidia kunipa Utulivu wa mwili na akili
Boss jifunze kuandika basi unaandika kama mtoto wa darasa la kwanza aah, haipendezi namna hii.mm mke wang nje ya tendo la ndoa ni mtumish wangu mwaminifu,,ananitumikia kwenye ajira niliyomwajiri pia ni shushushu wangu mzuri sana kuniletea taarifa za waajiriwa wengine..
Kiufupi kazi ya ushushushu anaimudu vizur sana na ananisaidia sana ktk hii biashara!!
Mungu ampe maisha marefu uyu mwanamke💯💯
Kwa hiyo,hawapo waliokosa vyote? Asiejielewa kwenye 30, ukifika 45 ndo atajielewa?Umesema sahihi Mkuu
Unapofika kuanzia miaka 45 ndiyo utajua kwamba Utulivu wa familia ni muhimu zaidi ya kuzagamuana...
Mke wangu ananisaidia kulea watotoWengi tulikuwa tunatamani kuoa, tukiamini baada ya kuoa maisha yatakuwa full starehe na hakutakuwa na migogoro.
Wapo waliofanikiwa kwa kupata watu sahihi, mpaka wakikaribia kuzeeka sura zao zinakuwa zinafanana.
Pia wapo waliokosa watu sahihi, na kujikuta wameingia kwenye ndoa yenye changamoto; ambao ukikutana nao njiani, sura zao zimekuwa nzito na zimejaa majukumu mazito na ghadhabu za kuingia kwenye ndoa.
Na wengi tunaoteseka kwenye hizi ndoa ni wanaume, sema huwa tunavumilia ndio maana ata takwimu zinaonyesha wanaume wanakufa haraka kuliko wanawake.
Sasa tujiulize swali; Kwa sisi wanaume tulio oa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?
R.I.P MkuuBinafsi Mke wangu ni Msaidizi wangu kwenye mambo mengi, mathalani;
Ananisaidia kusimamia baadhi ya miradi tuliyoanzisha pamoja (Nafanya hivi Kwa kujua kwamba nitawahi kufa kabla yake, hivyo Jukumu la kulea watoto litabaki kwake).
Anasaidia malezi ya watoto wetu
Anasaidia kunipa Utulivu wa mwili na akili
Mzee wa nongwa
Mzee wa kazi mbona kama unataka kuunda bomu ili limlipukie jamaa🤣🤣
Mwamba akiiona hii ata-rap sana. Kwenye ku-rap hata 2 Pac akasome.