Wanabodi Hili wazo langu tu.
Matukio yanayoendelea kwa sasa juu ya polisi na usalama wa watu tunahitaji kuunganisha nguvu na kuangalia watu wenye uwezo wa kutatua changamoto zetu.
Nilikuwa naangalia uwezo wa Mhe. Mwigulu juu ya yanayoendelea nikaona, yamemshinda kwa sana. Anahitaji msaada na kupumzishwa. Amefikia ukomo wa kupambana na changamoto za Idara yake anayoongoza.
Anahitaji kupumzika. Nimeangalia nje ya uzio wa CCM nikaona Mhe. Lema anaweza pambana na changamoto hizo na pengine kuzimaliza.
Mimi ni mtu ninayeamini katika umoja na utaifa zaidi ya uchama.
Naomba tuwe na wazo chanya katika hili.