Kwa mliosoma mkitumia majina mawili na mkaongeza la tatu,nisaidieni hapa!!!

Njia rahisi ni kuliongeza hilo jina la tatu lakini liwe katikati. Ukiliweka mwanzo au mwisho ndio itabidi ukaape mahakani.
 
Mimi nimesoma hadi chuo nikitumia majina mawili ninataka kuongeza la tatu msaada please (tafadhali) kwa hatua za kuchukua.
Nisaidieni wana jf
Vyeti vyako haviwezi kubadilishwa, vitabaki na majina hayo tu hata ukiapa kuongeza la tatu
 
Kwa sasa sijui mambo yako vipi lakini mwaka 2012 mimi niliongeza jina la tatu baada ya kuambiwa kwenye mkataba lazima utumie majina matatu!
1. Nilimwona karani wa mahakama ya mwanzo, akachukuwa fomu na kuijaza kadri nilivyomwelekeza kisha akanirudishia kwa ajili ya kuweka sahihi
2. Nilichukuwa ile fomu na kuipeleka mamlaka ya mapato Tanzania na kuweka " stamp duty" ya sh 500
3. Nilirudisha fomu kwa karani na kuipeleka kwa hakimu kwa ajili ya kuweka sahihi na muhuri.
Jumla ya gharama zote ilikuwa ni sh 5500/=
 
Majina huongezwa, kupunguzwa, hubadilishwa au kurekebishwa kwa nyaraka maalum ya kisheria inayoitwa Deed Poll. Hii huandaliwa, kusajiliwa na kuchapishwa. Baada ya hapo, mbadili jina huanza kulitumia jina jipya. Kiapo/Affidavit hakitumiki kubadili jina. Kiapo hutumika kupambanua tu majina yaliyopo kwenye nyaraka tofauti kwa muda ule tu.

Uko sawa "councel" Petro E. Mselewa kwa nilivyomuelewa shida yake ni kupambanua na si kubadilisha majina ndi maana ushauri wangu ni kuwa atumie kiapo kupambanua (verify) hayo majina.

Kaka ...
 
Nashukuru sana.Sasa ni mahakama gani,ya mwanzo au hata ya wilaya au mkoa kote wanafanya hivyo?Pia baada ya kiapo sasa jina wataongeza kwenye vyeti au watanipa tu barua ya utambulisho?
Sio lazi Mahakamani....unaweza kupata huduma hii pia ofisi za Wanasheria..
 
nafikiri nenda kwa mwanasheria au mahakamani utajaza kitu inaitwa deed poll then utaenda kuisajili wizara ya ardhi kama sijakosea baada ya muda kisheria (nafikir itangazwe kwenye govt gazzete)utakua umebadili jina
3a4aa1db57696ea45551ad0bfa2ef91f.jpg
 
Cheti cha kuzaliwa vip? Kina majina mawili? Na km huna chuo walikupokea vip?
 
Tatizo liko wap? Mbona mimi natumia hayo mawili? Hilo la tatu ni la kazi gani? Tumia majina yaliyoko kwenye vyeti vyako na vitambulisho.

Kuna wanawake wana tabia ya ujinga wakiolewa wanajifanya waume zao wanawapenda basi wanaongeza jina la mme ahaaaaa yalimkuta mwl mmoja yupo vyeti feki kisa hicho kijina cha tatu. Sory kama wewe si mwanamke.

Jina la tatu litakusumbua umesema lipo cheti cha kuzaliwa basi inatosha.

Mambo ya kubadilisha majina yana matatizo eg bashite.

Binafisi jina langu inabidi liandikwe kwa herufi R lakini cheti cha darasa la 7 kilikuja na L basi ilinilazimu kutumia L Hili kutoa usumbufu wa kwenda kubadilisha.
 
Back
Top Bottom