Uvamizi kwenye misitu ya serikali iliyohifadhiwa kwa ajili ya kilimo nafikiri ni kosa kwa mujibu wa sheria zetu tulizojitungia wenyewe Bungeni. Ukimpa nafasi mvamizi ya kuvuna mazao yake, msimu mwingine atalima na kusubiri huruma ya kuambiwa avune na huo utakuwa ni mchezo wake kila msimu! Dawa ni hiyo ya kufyeka ili asirudie tena kulima kwenye hifadhi.