Kwa matukio haya, hivi bado kuna watu wanatoka na wasichana wa chuo?

bobby dolat

Senior Member
May 18, 2015
167
263
Wadau nawasalimu,

Nimeshawishika kuuliza hili swali baada ya mfululizo wa matukio mfano wa lile la SAUT ambalo si la kwanza kutokea katika vyuo vyetu lingine lilitokea chuo fulani hapa dar kati ya 2011-2012 ambapo binti alimwitia mwizi mpenzi wake wa siku nyingi ambapo alipigwa vibaya hadi marafiki wa binti walipoanza kupaza sauti kwa uchungu wakiiiambia ile mob iliyokua ikimpiga yule jamaa kuwa jamani huyo sio mwizi bali ni mpenzi wake

Wakaacha kumpiga akakimbizwa hospital na akafa upon arrival
Mob ile ilishikwa na hasira sana baada ya kuelezwa ukweli hasa zilipokuja taarifa jamaa kafa.Binti alishauriwa ahame chuo kwa usalama wake

Lakini cha kushtua zaidi huyu jamaa alikua ndio mfadhili mkuu wa huyu binti chumbani kwa binti kulichafuka kwa thamani na appliances mbali mbali kwa hisani ya huyu jamaa, hata hivyo msaada wa hali na mali aliokua akiutoa kwa binti huyo ndio uliotumika kumuhonga kijana mwingine wa chuo na siku ya tukio marehemu alikua amewafuma hotelini wakifundishana hesabu na ndipo akaamua kuwahi chuoni chumbani kwa binti kwenda kusomba mali zake alizomnunulia binti ikiwemo laptop, printer ndogo, music system tv set na vingine vingi, wakati akiendelea na zoezi la kuingiza vitu hivyo kwenye gari binti akafika na kumuitia mwizi.

Milolongo ya visa vya mabinti wa chuo kuwatendea unyama wafadhili wao ni vingi mno Ingawa sio vyote vinaishia kwenye kifo.Duce pia kati ya 2009-2010 kulitokea kisa cha namna hii ambapo kijana alifariki kwa kujichoma/kuchomwa kisu kwa utapeli wa mapenzi uliofanywa na binti wa chuo hicho hasa baada ya jamaa kupiga gharama za mnara wa matumizi aliokwisha kuujenga tangu binti akiwa first year.

2006 nikiwa bado sijaoa nilikwenda kumtembelea msichana wangu hostel kwake alipanga nje ya chuo hostel zilizotambuliwa rasmi na chuo, alipanga vyumba viwili self contained na ndani palijaa kila kitu friji ndogo chumbani kubwa sebuleni, dining table, sofa set ya nguvu kitanda cha kifahari na vingine vingi.Nilikua nakosa nguvu ya kumuuliza hivyo vitu alivitoa wapi wakati ni mwanafunzi na hana kazi hadi siku moja nilipopata majibu ya swali Hilo
Nilikua ndio nimemaliza chuo hivyo Sina kazi Nilikua naenda kushinda hapo nakula hapo na hata kulala hapo

Usiku wa manane tukiwa tumelala na binti baada ya kutoka kuangalia dunia kigeu geu live makumbusho, mfadhili mkuu wa huyu binti akafika na gari nje na kuja kugonga dirishani akimwasha binti amfungulie mlango nikamuuliza binti ni nani akajibu hata yeye hujui.Hakufungua mlango na jamaa nje akaanza kufoka kwamba nilijua tu una bwana mwingine na maneno mengi

Watu wakatoka na landlord akamuomba binti afungue mlango binti akafungua
Bila watu kuwepo tungeweza kuuana na yule jamaa.Jamaa alilia kwa uchungu akisema anasubiri pakuche alete canter abebe vitu vyake binti hakua remorseful at all na ikawa ndio mwisho wao kwa tabia ile nami nikabaki nae kama pambo tu mwisho nikaoa msichana mwingine na yeye pia ameolewa na jamaa mmoja Tegeta Nyuki na ametulia kabisa.


Sasa ni nini hasa kinawafanya mabinti wanapokua chuo wawe na mawenge kiasi cha kukosa utu?
Je sio wao labda ni umri?

Na kwa hali hii Je tunawashauri vipi wanaume wenzetu wanaowekeza kimapenzi kwa wasichana wa vyuo? Maana tumeona wazi kundi Hilo halina utulivu kwenye mapenzi, Ingawa sio wote lakini iwapo tukisema tuweke katika % inaweza kuvuka 50%

Kwa muktadha wa matatizo yaliyojitokeza kwa ujumla wake Je ipo haja ya kuwashauri wanaume wenzetu ambao bado hawajaoa na wanatafuta kuaandaa wenza wa maisha kuachana kabisa na kundi hilo la mabinti wa vyuo na badala yake waweke nguvu zao kutafuta mabinti waliokwisha kufika kazini? Ambao wameshafanya fujo zote na sasa wametulia na wanahitaji familia?

Karibuni kwa mjadala
 
Nadhani dawa sio kuacha kudate wasichana wa chuo dawa ni kudeal na hawa watu wanaokurupuka na kuanza kumtoa mtu roho kisa kaitwa mwizi pasipo kumchunguza kwanza kama tuhuma huzo zina ukweli
 
Mleta mada una point nzito. Hawa mabinti wa siku hizi asilimia kubwa hawana UTU. Hayo matukio ya kupanga wanaume yapo sana tu. Unaweza kukuta binti mmoja ana midume mpaka mitano. Na kila mtu anapangwa kwa nafasi yake akijua yuko peke yake. Kuna Mzee mmoja ni Bosi mkubwa wa Benki moja hapa mjini alikuja kugundua anatafuna msichana mmoja na kijana wake wa kumzaa. Na dogo alimzimikia Demu kiasi cha kwenda kumtambulisha home ndio issue ikapasuka. Hawa mabinti wa Chuo hawana UTU...afadhali upate mwanamke anayejitambua wa Makamo.
 
My heart goes to the victims. But I do believe some brothas were simply born to be played, it's their fate. Whether College girls, high school girls, social media girls, club girls, groupie kinda girls, church girls, you name 'em.

Some brothas even get played by the type that ain't no playing type, while other brothas roll comfortably with the type that play, and never get played.
 
Yeah man i also feel sorry for the victims it's quite painful
 
Yaani kwa kweli mabinti wa chuo ni kichefu chefu sana sishauri mtu aende huko kabisa labda kama ni kujipumzisha tu
 
Nadhani dawa sio kuacha kudate wasichana wa chuo dawa ni kudeal na hawa watu wanaokurupuka na kuanza kumtoa mtu roho kisa kaitwa mwizi pasipo kumchunguza kwanza kama tuhuma huzo zina ukweli
Ni kweli kabisa lakini mkuu mtu unaanzaje kumuitia mtu mwizi huku ukijua implication yake kwamba atauawa
Ina maana maksudi ya mwenye kutamka neno mwizi lengo Lake ni uuawe

Hao wanaoanza kupiga mtu hadi kumuua wana makosa makubwa sana lakini Bahati mbaya hiyo ni mada nyingine, mada ni hawa wanaotamka hilo neno huku ukijua mwenzie atauawa
Hivi unaweza kumuitia mwizi mtu unaempenda? Kwa sababu yeyote ile?
 
Wenyewe wanaona sifa kuwa na msululu wa wanaume. Madhara yake ndo haya MTU kutolewa uhai.
 
Nadhani dawa sio kuacha kudate wasichana wa chuo dawa ni kudeal na hawa watu wanaokurupuka na kuanza kumtoa mtu roho kisa kaitwa mwizi pasipo kumchunguza kwanza kama tuhuma huzo zina ukweli

we hujawahi kuibiwa ndio mana unasema hivyo!, mi mwenyewe wezi nawachukia sanaa, utachunguza nini wakati ukiangalia unaona kabisa kuna vitu alishabeba, huyo dada ndio kavu" mana alijua kabisa kumwita mwizi atamhatarishia maisha yake, nimeona video yake akipgwa aisee huwezi kuiangalia mara mbili.
 
Siku zote nasema

Age 18-24 usiguse, na zaidi awe chuo. Lasivyo jiandae kwa lolote. Nakaa chuo ni staff na nyumba yangu iko barabarani kuelekea hostel. Ninayoyaona ni makubwa na mazito hayasimuliki kias kwamba ukiambiwa huwezi amini.

Rai kwa wanaume wenzangu, acha kuwekeza kwa watoto wa chuo, subiri wamalize watakukuta huko. Akisharudi mtaani akili huwa zinawarejea utafikiri shadidu za rejea.

Dont touch, watoto wadogo lakini range zinazowabeba ni za wazee na waheshimiwa ambaxo ukiambiwa lazima uzimie siku tatu.
 
Ni kweli kabisa
 
Mtoa mada umeongelea hili swala vzr sana, pongezi.

Nakubaliana na wewe kua hao mabinti wa vyuo kinachowasumbua ni utoto wa kutokujitambua baadae watakua wapi, makundi yenye vishawishi vya ajabu (coz mnakutana na tabia mbali mbali, sasa binti akiwa kichwa panzi, ndio anaendeshwa)
Wkt wakiwa pale wanachojua wao wanasoma wakimaliza watapata kazi maisha yatazidi kua mazuri,
Lkn kwa kua bado ni binti kila mwanaume anamtolea macho hvy hujiona hakuna kama yeye duniani na kuamua kuwapanga.

Matukio ni mengi sana kiukweli ila yote hua sababu ni hizo hapo juu,

So mnaweza kuwavumilia au mnaweza kuwaacha wamalize ujana mje muwaoe wakiwa makazini au wakiwa wanasota maisha nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…