Kwa mara nyingine tena, hapa ndipo anapokosea Rais Magufuli

CCM ndio tatizo,ilikuwa na nafasi ya kumwonyesha anapokosea na kumkanya lakini yenyewe imesimamia kumuunga mkono hata akiendesha kupeleka Lori korongoni

Usijali, wakinyamaza sisi tutasema, wakisifu ujinga, sisi tutakosoa na kuwalazimisha kugeuza njia, wakiwa tayari kukosoa sisi tutaungana nao ili ilani yao ya CCM itekelezeke kwa maslahi ya watanzania wote.

Hatununi kwa udhaifu wao lakini wasijaribu kutunyamazisha.
 
hoja yako inakila vigezo lkn waliopga kelele za ndiooo hawata kuelewa zaid ya kukubeza kuwa we2 n mpinzan il hal ukwel unajionesha! kwan mikataba mibov ilisainiwa na wapinzan? wafanyakaz hewa waliajiriwa na upinzan? mikataba ya hati ya dharura ililetwa na upinzan? na kadha wa kadha hvyo wanao mkebeh mtoa post,mkijhb hayo maswal hapo juu hakika hamtampika na kumkebeh mtoa post!

Hawataweza hawa. Wamefundishwa hivyo, zamani walikuwa wakienzi fikira za mwenyekiti, leo wanaenzi fikira za mazimwi waliolelewa na kutunzwa kwa kodi za watanzania. (mnisamehe)
 
Pata tort ya hennessy, v.s.o.p nitalipa. Wazalendo tupo wengi tu huku mitaani, pamoja na machungu yote wanayotupatia, tupo tunahangaika kujipatia riziki kihalali na tukiwa tayari kuipigania nchi yetu.

Endeleza hayo hayo. mungu atakuongezea kipato na maarifa zaidi.

Tuungane kuwaumbuwa hawa wababaishaji wetu.
 
CCM ndio tatizo,ilikuwa na nafasi ya kumwonyesha anapokosea na kumkanya lakini yenyewe imesimamia kumuunga mkono hata akiendesha kupeleka Lori korongoni

Wataweza wapi ? Tazama namna wanavyohangaika kutetea uovu na wanavyohangaika na hii post. Lakini tushukuru. Kuna siku wataamka na kukumbatia huu ukweli. CCM msaidieni Rais wetu JPM kwa kumwambia ukweli sio kusifia hata kama anakosea.
 
Mwanzoni tulifikiri labda anaweza kujirekebisha baadae lakini hadi sasa anazidi kuharibu. Tanzania tokea kuingia madarakani kwa rais Magufuli kumeibuka maamuzi mengi yanayotikisa na mara zote tunaaminishwa kuwa hufanywa maamuzi hayo kwa uzalendo mkubwa wa Rais wetu.

Alianza na kutumbuwa bandarini, na kuna wafanyakazi walisimamishwa wengine kwa maamuzi ya hadharani na kunasibishwa na upigaji dili kabla ya uchunguzi kufanyika. Kuna makosa yalifanywa watu waliharibiwa wasifu wao na kuchonganishwa na jamii kwa kauli tu zisizostahi utaratibu wa kiutumishi. Hili pia liliwagusa watendaji wengine kadhaa ama kwa kutenguliwa na wengine kuahidiwa kupangiwa kazi nyengine.

Lengine ni sakata la ufisadi na kuundwa kwa mahakama hiyo. Rais alituaminisha kuwa kuna ufisadi wa kutisha na kuunda mahakama kwa gharama na kwa haraka lakini baadae wenye dhamana wakaja hadharani kutwambia hakuna kesi za mafisadi. Rais JPM anafanya kosa la kukurupuka kila wakati ambapo kwa maoni yangu anaanzisha jambo kwa nguvu zote na kuaminisha jamii kwamba yuko vizuri na hatimae anapoteza credibility kila uchao.

Huu ufisadi umemshinda na kinachoonekana ni visasi tu. Mifano iko mingi ya waliohusika na ufisadi na wizi na hata kusemwa katika vyombo vya dola kama bunge na kutolewa maazimio. Mimi nilifikiri haya ndiyo ilikuwa aanze nayo mfano kuna ESCROW. Liko wazi kabisa lakini kalikwepa.

Kuna kishindo cha vyeti feki ambapo watu kadhaa walichukuliwa hatua na Rais aliahidi kuwashughulikia wote. Lakini kwanza kazi hii nayo imeguswa na kuachwa na tayari imeharibika kama ilivyoharibika ajenda ya ufisadi. Kuna kupendeleana na ubaguzi. Baadhi ya kada haziguswi na taasisi nyeti zimeachwa. Hakuna usawa na uzalendo kuna majungu na visasi kwa baadhi ya makundi. Katika hili tunaambiwa leo eti wanasiasa hawamo, baadhi ya vikosi vya ulinzi havimo na kuna undumi lakuwili. Polisi wanachunguzwa na taarifa zinatolewa lakini jeshi la Ulinzi wao haliwahusu. Huo uzalendo wa kuwagawa watu unatoka wapi ?

Kuna suala la madawa ya kulevya nalo limeharibiwa tayari, ilitumika nguvu kubwa kuliibua na limeishia isivyotarajiwa, Bado tatizo lipo na ile misingi haijaguswa. Rais JPM kalirukia hili suala nyeti na kuliharibu na sasa linaelea.

ANAPOKESEA RAIS JPM

Mara zote anakosea kujua pa kuanzia. Inawezekana hana nia ya dhati au hashauriki na hivyo huamua kujitosa yeye mwenyewe kwa kuliibua jambo ambalo halina mikakati. Mara ngapi Rais anaibua issue lakini hafiki hatua hata mbili kunaonekana mapunguifu ama ya kisheria au ya kiutumishi na suala hilo hupoteza haiba kwa haraka ?

Hapo ndipo anapokosea Rais wetu. Hatimae mambo makubwa yanapotea bure kwa kukosa mikakati na kujuwa pa kuanzia.

Hajui pa kuanzia na hatimae hajuwi pa kumalizia. Kwa ufupi Rais wetu amekosa mwelekeo yote aliyoanzisha hayana misingi na kitu kikikosa misingi hakidumu kitapotea na kuanguka tu.

FAIDA.

Rais anaibuwa hoja na hatatuwi tatizo huu ndio ukweli. Na kwa kuibuwa hoja hizi bado hajaonesha mpya, akumbuke wapinzani walishaibua zamani na walipuuzwa na akiwemo yeye Magufuli wakati alipokuwa anatetea chama (CCM) kuliko nchi. Wakati ule alikuwa kimya leo anatuaminisha kuwa ni mambo mapya. Rais hapa anafanya siasa za kizamani. Rejea hoja za mikataba ya madini, Ufisadi n.k.

UZALENDO.
Kwani nani mzalendo ? jee mzalendo ni Rais tu kwa kuwa ndio kawa Rais ? hii dhana inavurugwa ili kujinufaisha kisiasa. Uzalendo ni pamoja na kusimamia sheria, kuziandaa sheria kulinda rasilimali za nchi na kutenda haki. Uzalendo si kupitisha sheria fyongo halafu ukaja kulia baadae eti nchi inapigwa. Kwani ulikuwa wapi ? Uzalendo ni asili ya mtu si maigizo kwa kuwa umekuwa Rais, mbunge au jaji. Uzalendo unaishi na haupotei kwa matukio.

WAPI PA KUANZIA NA NINI KIFANYIKE.
Pa kuanzia panaeleweka na naamini hata Rais JPM anapaelewa. Kuna pahala kama nchi tumejikwaa tukiri CCM ilituingiza Chaka huo ndio ukweli. Tatizo ni CCm na vyombo vyake kuanzia kwenye chama, bunge na wasomi wake. Chama kilishindwa kuiongoza serikali kuweka misingi ya kulinda nchi na rasilimali zake. Bunge lilishindwa kudhibiti ukada na likapitisha miswaada ovyo na kukomoa wapinzani hatimae nchi leo imeliwa. Wasomi wa CCM walishindwa kukosoa.

Tufanye na tutunge katiba mpya yenye mwelekeo mpya wa kuijenga Tanzania. Kupitia hili viwanda vitapatikana na rasilimali zitalindwa. Rasimu ya warioba irejeshwe na iboreshwe ikionekana kuna haja. Nje ya hapa Kingozi yoyote anaetokana na CCM amepoteza uhalali wa kuhoji ufisadi, kuporwa, mikataba na rasilimali zetu. CCM kaeni kimya na rais JPM anyamaze.

Tunahitaji jambo jipya kama taifa walau CCM na JPM zungumzeni Katiba mpya watanzania watawaelewa. Ufisadi, mikataba mibovu, rushwa, madawa ya kulevya na vyeti feki hayo ni matunda ya CCM kwa kuongoza nchi hadi sasa.

Rais Magufuli anapajuwa anapokesea. Akipatia wote tutamsifu lakini si kwa haya ya machozi ya mamba.

Kishada.

cc Lizaboni and Co.
Chadema kilichobaki ni kumkosoa Rais Tu kila kukicha, wenyewe hamna dira wala muelekeo, chama kinawaozea mkononi .
 
Kwani hujasikia mwana mkuu wa sheri-hiya pale mjengoni kakwambia kama wakitakiwa kulipa hilo ni deni la wabongo wote,,!! Ina maana hawajali ili mradi sifa za kinanihii za majitaka wao hawajali hata wakishindwa mahakamani,,ina maana aliyeongea vile yule mwana mkuu wa mzee sheri-hiya anajua suala kama la kuzuia kifusi cha watu ni kosa na wao watashindwa tu,ila hawajali kwani wao ubao wa namba si upo mgongini mwao hawaisomi namba,,sasa hilo ni moja ya dubwasha la kuitwa kurupakalism
 
Chadema inahusika nini hapa? Acha hizo sisi wengine tunavyama vyetu sio chadema. Nakushauri jibu hoja kama huna cha kujibu nyamaza.
 
Kwani hujasikia mwana mkuu wa sheri-hiya pale mjengoni kakwambia kama wakitakiwa kulipa hilo ni deni la wabongo wote,,!! Ina maana hawajali ili mradi sifa za kinanihii za majitaka wao hawajali hata wakishindwa mahakamani,,ina maana aliyeongea vile yule mwana mkuu wa mzee sheri-hiya anajua suala kama la kuzuia kifusi cha watu ni kosa na wao watashindwa tu,ila hawajali kwani wao ubao wa namba si upo mgongini mwao hawaisomi namba,,sasa hilo ni moja ya dubwasha la kuitwa kurupakalism

Kama wamerogwa vile au wametamukiwa ubwabwa. Yaani wanazidi kumpoteza rais wetu. Hawamsaidii wanazidi kumzamisha.

Binafsi nina wasi wasi na wasaidizi wake isije ikawa wana mkakati wa kummaliza kwa njia ya MISIFA. Hawa wanamchochea wakijuwa huwa anapenda hivyo ili aharibikiwe.

Nina wasi wasi kuwa hii ni mbinu ya kisomi kumaanisha mtoto akilia mpe wembe achezee.
 
Mwanzoni tulifikiri labda anaweza kujirekebisha baadae lakini hadi sasa anazidi kuharibu. Tanzania tokea kuingia madarakani kwa rais Magufuli kumeibuka maamuzi mengi yanayotikisa na mara zote tunaaminishwa kuwa hufanywa maamuzi hayo kwa uzalendo mkubwa wa Rais wetu.

Alianza na kutumbuwa bandarini, na kuna wafanyakazi walisimamishwa wengine kwa maamuzi ya hadharani na kunasibishwa na upigaji dili kabla ya uchunguzi kufanyika. Kuna makosa yalifanywa watu waliharibiwa wasifu wao na kuchonganishwa na jamii kwa kauli tu zisizostahi utaratibu wa kiutumishi. Hili pia liliwagusa watendaji wengine kadhaa ama kwa kutenguliwa na wengine kuahidiwa kupangiwa kazi nyengine.

Lengine ni sakata la ufisadi na kuundwa kwa mahakama hiyo. Rais alituaminisha kuwa kuna ufisadi wa kutisha na kuunda mahakama kwa gharama na kwa haraka lakini baadae wenye dhamana wakaja hadharani kutwambia hakuna kesi za mafisadi. Rais JPM anafanya kosa la kukurupuka kila wakati ambapo kwa maoni yangu anaanzisha jambo kwa nguvu zote na kuaminisha jamii kwamba yuko vizuri na hatimae anapoteza credibility kila uchao.

Huu ufisadi umemshinda na kinachoonekana ni visasi tu. Mifano iko mingi ya waliohusika na ufisadi na wizi na hata kusemwa katika vyombo vya dola kama bunge na kutolewa maazimio. Mimi nilifikiri haya ndiyo ilikuwa aanze nayo mfano kuna ESCROW. Liko wazi kabisa lakini kalikwepa.

Kuna kishindo cha vyeti feki ambapo watu kadhaa walichukuliwa hatua na Rais aliahidi kuwashughulikia wote. Lakini kwanza kazi hii nayo imeguswa na kuachwa na tayari imeharibika kama ilivyoharibika ajenda ya ufisadi. Kuna kupendeleana na ubaguzi. Baadhi ya kada haziguswi na taasisi nyeti zimeachwa. Hakuna usawa na uzalendo kuna majungu na visasi kwa baadhi ya makundi. Katika hili tunaambiwa leo eti wanasiasa hawamo, baadhi ya vikosi vya ulinzi havimo na kuna undumi lakuwili. Polisi wanachunguzwa na taarifa zinatolewa lakini jeshi la Ulinzi wao haliwahusu. Huo uzalendo wa kuwagawa watu unatoka wapi ?

Kuna suala la madawa ya kulevya nalo limeharibiwa tayari, ilitumika nguvu kubwa kuliibua na limeishia isivyotarajiwa, Bado tatizo lipo na ile misingi haijaguswa. Rais JPM kalirukia hili suala nyeti na kuliharibu na sasa linaelea.

ANAPOKESEA RAIS JPM

Mara zote anakosea kujua pa kuanzia. Inawezekana hana nia ya dhati au hashauriki na hivyo huamua kujitosa yeye mwenyewe kwa kuliibua jambo ambalo halina mikakati. Mara ngapi Rais anaibua issue lakini hafiki hatua hata mbili kunaonekana mapunguifu ama ya kisheria au ya kiutumishi na suala hilo hupoteza haiba kwa haraka ?

Hapo ndipo anapokosea Rais wetu. Hatimae mambo makubwa yanapotea bure kwa kukosa mikakati na kujuwa pa kuanzia.

Hajui pa kuanzia na hatimae hajuwi pa kumalizia. Kwa ufupi Rais wetu amekosa mwelekeo yote aliyoanzisha hayana misingi na kitu kikikosa misingi hakidumu kitapotea na kuanguka tu.

FAIDA.

Rais anaibuwa hoja na hatatuwi tatizo huu ndio ukweli. Na kwa kuibuwa hoja hizi bado hajaonesha mpya, akumbuke wapinzani walishaibua zamani na walipuuzwa na akiwemo yeye Magufuli wakati alipokuwa anatetea chama (CCM) kuliko nchi. Wakati ule alikuwa kimya leo anatuaminisha kuwa ni mambo mapya. Rais hapa anafanya siasa za kizamani. Rejea hoja za mikataba ya madini, Ufisadi n.k.

UZALENDO.
Kwani nani mzalendo ? jee mzalendo ni Rais tu kwa kuwa ndio kawa Rais ? hii dhana inavurugwa ili kujinufaisha kisiasa. Uzalendo ni pamoja na kusimamia sheria, kuziandaa sheria kulinda rasilimali za nchi na kutenda haki. Uzalendo si kupitisha sheria fyongo halafu ukaja kulia baadae eti nchi inapigwa. Kwani ulikuwa wapi ? Uzalendo ni asili ya mtu si maigizo kwa kuwa umekuwa Rais, mbunge au jaji. Uzalendo unaishi na haupotei kwa matukio.

WAPI PA KUANZIA NA NINI KIFANYIKE.
Pa kuanzia panaeleweka na naamini hata Rais JPM anapaelewa. Kuna pahala kama nchi tumejikwaa tukiri CCM ilituingiza Chaka huo ndio ukweli. Tatizo ni CCm na vyombo vyake kuanzia kwenye chama, bunge na wasomi wake. Chama kilishindwa kuiongoza serikali kuweka misingi ya kulinda nchi na rasilimali zake. Bunge lilishindwa kudhibiti ukada na likapitisha miswaada ovyo na kukomoa wapinzani hatimae nchi leo imeliwa. Wasomi wa CCM walishindwa kukosoa.

Tufanye na tutunge katiba mpya yenye mwelekeo mpya wa kuijenga Tanzania. Kupitia hili viwanda vitapatikana na rasilimali zitalindwa. Rasimu ya warioba irejeshwe na iboreshwe ikionekana kuna haja. Nje ya hapa Kingozi yoyote anaetokana na CCM amepoteza uhalali wa kuhoji ufisadi, kuporwa, mikataba na rasilimali zetu. CCM kaeni kimya na rais JPM anyamaze.

Tunahitaji jambo jipya kama taifa walau CCM na JPM zungumzeni Katiba mpya watanzania watawaelewa. Ufisadi, mikataba mibovu, rushwa, madawa ya kulevya na vyeti feki hayo ni matunda ya CCM kwa kuongoza nchi hadi sasa.

Rais Magufuli anapajuwa anapokesea. Akipatia wote tutamsifu lakini si kwa haya ya machozi ya mamba.

Kishada.

cc Lizaboni and Co.
Ndg kwa kifupi hueleweki! Maana wewe umejikita kwenye lawama kwa Rais, kama wanavyotoa lawama wengine. Kwanini huwa tunayaona mabaya pekee.... Ina maana rais huyu ana mabaya tuu? Hana mazuri?
Unapo post habari kama unania ya kuelimisha, basi balance story, weka mazuri na mabaya yake! Nahisi ulikuwa na lengo jema ila lengo umelipoteza na kulipotosha kwa ajili ya ushabiki fulani. Aidha ni wa kiitikadai ya chama fulani au ya kikanda fulani.
Mimi nilieko mtaani naamini kuna baadhi ya mambo ameyamudu kabisa! Kama la uzalendo! Hilo halina ubishi kabisa. Labda uwe na sababu zako binafsi ndiyo utazidi kupinga.
Ukweli usiopingika kuwa Tanzania siku hizi hakuna yale madaraja ambayo walikuwa ndiyo hasa chanzo cha manung'uniko na ndiyo yalisababisha watu tukaanza kuichukia serikali.
Hivyo basi pamoja na hayo mabaya mnayoyasema kwa Rais pia kuna mengi mazuri kayafanya tena kwa muda mchache, ila hamtaki kuyaona wala kuyathamini.
 
Mtoa mada unaweza ukwa na point, ila unapotupa lawama zote kwa CCM nadhani unakosea, na nadhani hata wewe mwenyewe unajiponga kwamba si CCM wote wenye nia mbaya na nchi yetu unaposema RASUMU ya Warioba iendelezwe kua katiba ya nchi, wakati Warioba ni CCM kufa. Hapa lamsingi, ni kubadili katiba ya nchi, kuweka malengo "vission" ya nchi kikatiba, tujue kama nchi tunataka kufika wapi, na tu aendaje hapo tunapotaka kwenda.
Wapinzani walianza viziri sana walipoona CCM wanatoka kwenye reli baada ya kupindisha mapendekezo ya rasimu ya Warioba pale walipokuja na "project UKAWA", chakushangaza nao wamepata cold feets, wakanza kubadili gear angani mara UKUTA mara hili. Hapa kama tungestick na UKAWA, ninauhakika tungekua mbali sana sasahivi.
Nashauri UKAWA ipewe nguvu tupiganie katiba mpya kama taifa, katiba iliyopita imefanya sehemuyake, tunataka katiba mpya yakutupeleka miaka 50 mingine.
Kwa kuangalia anachokifanya JPM ni wazi kwamba anapingana na wasioitakia TZ mema, na kwabahati mbaya katinga ngazi za juu ndio wengi, hivyo hata yeye kwa lolote atakalojaribu kufanya lazima limtese na limchukulie nguvu zaidi, muda na rasilali zingine. Lamsingi ni kufumua mfumo mzima ambao msingi wake mkubwa ni katiba ya nchi. Vinginevyo atafanya anayofanya ila keshokutwa akiondoka tunarudi nyuma hata kuliko ambapo tungekua.
 
Huyu bwana hii nchi keshahiaribu kbsa. Ajira kafuta, uhakiki ulifanyika kwa ubaguzi (hapa keshagawa taifa), fao la kujitoa halipo, rambi rambi zina.liwa hadharani bila aibu, increment nayo ilipigwa panga mchana kweupeeeeeeee ni shida. Huyu bwana keshahiaribu hii nchi, tunaishi basi tu
Lkn wana "ccm B" huwa mna matatizo gan? Kila siku nchi kaiharibu ndio nn sasa. Je, nyie mnaweza kutengeneza nchi wakati mngali mnatumia wanachama wanaotemwa na ccm A" vp hapo kweli kutakuwa na mabadiliko?
 
Tatizo kubwa mi ccm yote wanamwogopa mno Magu
Kwa kuwa hasikizi wapinzani basi huko fisiemu hakuna wa kumwambia chochote zaidi ya kumsifia na kumuacha apuyange na kututokomeza kusiko julikana
Vp kuhusu nyie kwa dj mboe mna jeuri
 
Back
Top Bottom