Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,373
- 13,134
Ukitazama madogo asubuhi na mapema wanabeba mabegi mazito migongoni kuisaka elimu siku nzima wanakesha mashuleni kurudi mpaka jioni.
Wengine wanasomeshwa kwa lazima mpaka siku za weekend lengo ni kupata matokeo mazuri ya mitihani yao.
Wana sura zilizo na matumaini lakini moyoni mwangu kumejaa huzuni sana nikiwatazama kaka na dada zao mitaani kuna muda unatamani kuwaambia madogo kuwa wanapoteza muda na wanapotezewa muda wao huko wanakoenda asubuhi na mapema na kurejea majumbani kwao kiza kizito.
Ila unamua tu kukaa kimya na kuendelea na maisha yako lakini madogo hawana future yoyote kabisa wanajiendea tu sawa na kuku aliyekatwa kichwa.
Safari ya madogo na watoto wetu kwenye elimu ni sawa na safari ya kichaa ataenda umbali mrefu mwisho anarejea na takataka.
Kama familia haijiwezi ni vyema ndugu zangu hata kasi ya kuzaa tupunguze serikali zetu hizi hazijali lolote kuhusu umasikini wetu.
Kuzaa zaa hovyo tuachane na aina hii aina ya maisha.
Kwa ufupi taifa linazalisha rundo la masikini kwa kasi sana ndio maana kusifia viongozi na watu wenye pesa inaonekana ni kazi ya kujipatia pesa.
Hakuna future hapa taifani, hakikisha unazaa utakao weza walea na kuwatengenezea njia, viongozi wetu hawaishi kama tunavyoishi sisi wananchi wa kawaida wao wanawaandalia kesho yao bora watoto wao kielimu na kifedha.
Sisi wananchi wa kawaida tuna jiendea tu kama vichaa, tuna zaa masikini na tunaongeza rundo la masikini maana hata mifumo ya elimu yetu hai support kutukomboa na huu umasikini wetu.