Kwa kumuacha huku Onana hapa sasa tumeenda sawa na Kunifurahisha, ila naomba Kibu Denis apewe Adhabu Kali au aombe Radhi leo kwa Mkapa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,818
118,608
Ujio wa kipa mpya kutoka Guinea, Moussa Camara 'Spider' umemfanya winga wa Simba, Willy Onana kung'oka Msimbazi baada ya taarifa kuvuja kuwa yeye ndiye anayempisha kipa huyo aliyetua kuziba nafasi ya Ayoub Lakred aliyeumia kambini Misri.

Taarifa ambazo Mwananchi tangu awali ilishazidokeza katika matoleo ya nyuma kwamba, kipa huyo aliyepewa mkataba wa miaka miwili akitua tu Msimbazi, basi Mcameroon huyo atachomolewa kikosini zimedhihirika.

Usajili wa Camara ni wa dharura kutokana na kuumia kwa Ayoub Lekred, ambaye alionekana tegemeo ndani ya kikosi hicho, hivyo ujio wake ataongeza nguvu dhidi ya makipa wenzake Hussein Abel na Ally Salim.

Katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo, yaliyofanyika leo Ijumaa Agosti 2, 2024, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Onana hakuwa sehemu ya kikosi na taarifa za ndani zinaeleza keshapata timu huko Qatar anayoweza kujiunga nayo wakati wowote.

Chanzo: mwananchi_official

Yaani kabisa GENTAMYCINE nikukatae / nikuchukie halafu UTOBOE? Haya mliompenda Onana mfuateni aendako Oky?

Imeisha hiyo........!!
 
Kama fredi bado yupo basi hakuna chamaana
Bora hata Fred kidogo Mkuu ila kwa Onana alikuwa anatuchelewesha tu. Kwenye 5 Fed anaweza Kufunga 1 ila Onana kwenye 15 si tu hawezi Kufunga 1 bali hata tu Kugongesha Besela pia hawezi. Na huu Umri wangu wa sasa Nikijifua vilivyo na nikapagwa namba 9 au 10 Timu nyingine na Yeye nyingine bado nina uhakika Nitafunga na Yeye hatofunga. Acheni aende na Nimefurahi ile mbaya Kuachwa.
 
Yaani kabisa GENTAMYCINE nikukatae / nikuchukie halafu UTOBOE? Haya mliompenda Onana mfuateni aendako Oky?

Imeisha hiyo........!!

Asa mpaka kapata timu ambayo inampa mshahara mnono zaidi ya anaolipwa Simba si maanake katoboa? Wewe unamchukia mwenzio kapata ofa zaidi sasa nani mshindi?
 
Mshindi ni Mimi niliyemchukia kwani Kaondoka katika Timu yangu pendwa ya Simba SC. Kama umenuna mfuate huko.
 
Kwa sababu ya uwendawazimu wa kumuabudia KIBU, tiketi yangu nahesabia nimekula hasara, ni kama nimetembea kariakoo tu nikaangusha elfu 15, na sio gemu hii tu(ambayo nishalipia tiketi), sintoenda na gemu nyingine aidha kibu atoke aombe radhi, na kama tungekuwa tuna UMOJA mashabiki wa simba tungesusia kwenda viwanjani..

Ishu ya kibu ni upuuzi usiovumilika, hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu, aabudiwe ye nani, kawa pele au messi, kama ferguson alikorofishana na beckham, arterta alimuuza aubameyang ambae alikuwa mfungaji bora wa timu, kibu ye nani, akivungiwa na hili basi mjiandae kisaikolojia lwa kubwa kuliko hili.
 
Hatuna mbadala wa kibu Acha tukubali kumuabudu ili tufaidike kwa kuifunga yanga
 
Kwa sababu ya uwendawazimu wa kumuabudia KIBU, tiketi yangu nahesabia nimekula hasara, ni kama nimetembea kariakoo tu nikaangusha elfu 15, na sio gemu hii tu(ambayo nishalipia tiketi), sintoenda na gemu nyingine aidha kibu atoke aombe radhi, na kama tungekuwa tuna UMOJA mashabiki wa simba tungesusia kwenda viwanjani..

Ishu ya kibu ni upuuzi usiovumilika, hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu, aabudiwe ye nani, kawa pele au messi, kama ferguson alikorofishana na beckham, arterta alimuuza aubameyang ambae alikuwa mfungaji bora wa timu, kibu ye nani, akivungiwa na hili basi mjiandae kisaikolojia lwa kubwa kuliko hili.
Kampeni ZOMEA KIBU inaendelea kwenye magrupu ya WhatsApp.
Hatumtaki huyo Mkimbizi ***** zake
 
Kwa sababu ya uwendawazimu wa kumuabudia KIBU, tiketi yangu nahesabia nimekula hasara, ni kama nimetembea kariakoo tu nikaangusha elfu 15, na sio gemu hii tu(ambayo nishalipia tiketi), sintoenda na gemu nyingine aidha kibu atoke aombe radhi, na kama tungekuwa tuna UMOJA mashabiki wa simba tungesusia kwenda viwanjani..

Ishu ya kibu ni upuuzi usiovumilika, hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu, aabudiwe ye nani, kawa pele au messi, kama ferguson alikorofishana na beckham, arterta alimuuza aubameyang ambae alikuwa mfungaji bora wa timu, kibu ye nani, akivungiwa na hili basi mjiandae kisaikolojia lwa kubwa kuliko hili.
Mkuu nakuomba leo nenda SIMBA DAY kwani nasikia Kibu Denis atatuomba RADHI wana Simba SC wote pale Uwanjani.
 
Nashukuru mkuu,nilipumzika ndio nmeamka, saa 10 hii siwezi kwenda tena, nasubiri kwa hamu aombe huo msamaha, nitatengua maamuzi yangu na kwenda kutizama game za simba, kama akiomba msamaha basi nitasamehe, na game zijazo nitakuwa naenda kama kawaida.
 
Back
Top Bottom