Kwa kianzio cha bajeti ya 25M, naweza kufikia hatua gani ujenzi wa nyumba ya vyumba 4.

Acha uoga kopa japo kidogo angalau 20m, kwa sababu inaonekana kipato chako ni kikubwa
Bado sijaona ulazima wa kukopa kwa sasa, labda siku za usoni na siombei hilo litokee sababu mikopo inaumiza kwa muda mwingine kwa mtu ambaye hajainuka kiuchumi.
 
Heri za Sikukuu wana jamvi.

Mwaka ndio huo umekatika, presha imeanza kupanda na kushuka kwa kuukabili mwaka ujao.

Kwa upande wangu ninapla kuukabili mwaka ujao mapema iwezekavyo kwa kazi ya kuushtua ujenzi wa nyumba ya kuishi.

Nyumba itakayokuwa na vyumba 4:

Chumba cha kwanza Master, hiki naplan kiwe na ukubwa wa kutosha maana ndio kitakuwa cha Baba/Mama mwenye nyumba. Humo angalau pawe na nafasi ya kuweka kabati la nguo, meza kwa ajili ya mambo ya kawaida kama kujisomea, dressing table n.k

Chumba cha Pili, kitakuwa cha wageni wa jinsia kike, hiki hakuna haja ya kuwa master. Watatumia public toilet/washaroom

Chumba cha tatu, kinaweza kuwa master/ sio master, kitatumiwa na watoto pamoja na msaidizi wa kazi(Dada). Hiki mnaweza kunishauri zaidi namna kiwe na sifa zipi.

Chumba cha nne, kitakuwa sio master, kwa ajili ya watoto wa kiume na wageni wa kiume.

Sifa zingine za nyumba:

-Sitting room yenye ukubwa wa kutosha

-Dinning, yenye ukubwa wa kawaida tu maana sio ya kukaa sana, watu watakaa Sitting room.

-Jiko, chenye nafasi cha kuweza kuweka vitu muhimu vya humo jikoni au niseme vitu vya kisasa.

- Store

-Public toilet/washroom.

Location ni Dodoma.

Karibuni kwa mawazo na ushauri!
Mkuu...kweli Duniani wawili wawili...

Nilitaka kuanzisha uzi wa namna hii tofauti ni eneo tu....mimi eneo ni Dar huku...kiwanja ni Flat labda wataalam waje watoe makadirio kuna mmoja kasema hapo naishia kwenye msingi ramani hii hapa.
 
Attachments

  • LASTANZA (7).jpg
    LASTANZA (7).jpg
    2.5 MB · Views: 7
  • LASTANZA (8).jpg
    LASTANZA (8).jpg
    2.4 MB · Views: 5
Karibuni Nile house 🏠 🏠 designs!!

kwa sasa tumeboresha huduma zetu Ili kukufikia mteja zaidi, tunatengeneza michoro na muonekano (3d) wa nyumba, majiko, sebule, bars, mandhari( landscape ) na huduma yoyote unayotaka kuanzisha,
Wasiliana nasi Leo tukupe huduma unayohitaji,

Call/Whatsapp 0715477041
 
Nakubaliana na wazo lako la kutoa kuwa muumini wa nyumba kubwa, ila hili wazo lako naona linawafaa zaidi watu ambao tayari wana familia zilizosimama na wala si yule anayeanza au yuko mwanzo wa kujenga Familia.

Kuanzia sasa hadi mtoto wa kwanza aje aanze kujitegemea itapita miaka 25, sasa wakati akiwa nyumbani unataka tubanane kwenye nyumba ndogo maana atakuwa na wenzio pia(watoto wenzake), hili suala la kubaba ndio silitaki.

Nimeplan kujenga nyumba ya kueleweka then ishu ya kujenga iishe na zifuate issue zingine za maendeleo.
Kila mtu ana plan zake, hivyo hizi ndio plan zangu
Bro usiogope mim nimejenga vyumba 3 ila nyumba kubwa san, saiv najipana na usaf
 
Vyumba vinne hapo boma tu litakula;
20M (For best quality housing)
15M (for standard quality)
10M (for poor quality)

Ila kwa maelezo yako nazan unataka kitu quality so ni wewe uamue unajenga vipi

I'm talking from experience
Mkuu, boma bila hata kupaua ndio likale milioni 25 😳😳
 
Heri za Sikukuu wana jamvi.

Mwaka ndio huo umekatika, presha imeanza kupanda na kushuka kwa kuukabili mwaka ujao.

Kwa upande wangu ninapla kuukabili mwaka ujao mapema iwezekavyo kwa kazi ya kuushtua ujenzi wa nyumba ya kuishi.

Nyumba itakayokuwa na vyumba 4:

Chumba cha kwanza Master, hiki naplan kiwe na ukubwa wa kutosha maana ndio kitakuwa cha Baba/Mama mwenye nyumba. Humo angalau pawe na nafasi ya kuweka kabati la nguo, meza kwa ajili ya mambo ya kawaida kama kujisomea, dressing table n.k

Chumba cha Pili, kitakuwa cha wageni wa jinsia kike, hiki hakuna haja ya kuwa master. Watatumia public toilet/washaroom

Chumba cha tatu, kinaweza kuwa master/ sio master, kitatumiwa na watoto pamoja na msaidizi wa kazi(Dada). Hiki mnaweza kunishauri zaidi namna kiwe na sifa zipi.

Chumba cha nne, kitakuwa sio master, kwa ajili ya watoto wa kiume na wageni wa kiume.

Sifa zingine za nyumba:

-Sitting room yenye ukubwa wa kutosha

-Dinning, yenye ukubwa wa kawaida tu maana sio ya kukaa sana, watu watakaa Sitting room.

-Jiko, chenye nafasi cha kuweza kuweka vitu muhimu vya humo jikoni au niseme vitu vya kisasa.

- Store

-Public toilet/washroom.

Location ni Dodoma.

Karibuni kwa mawazo na ushauri!
Inategemea na ukubwa wa nyumba na ujenzi huo unafanyika mkoa gani
 
mkuu room 4 ujengee tofar 3500? sirias
utumie cement 100 sirias, unajenga ama unapaka paka cement.

kwa maelezo ya mtoa mada nyumba yake inataka SPACE yaan room kubwaa, siting ilioshiba
Hata mm nimepata shock humu kama hujui nyamazq ujifunze hyo ni tofali 5500 mpk 6000 kwengine sitaki kuingia
 
JF tunazidiana uwezo. Kuna mtu million 25M ni hela ya msingi mpaka finishing. Mwingine in pesa ya boma na kupaua. Mwingine ni pesa ya boma. Mwingine 25m, hata msingi haitoshi. Ndo maana kila mtu ana Ushauri wake.

Ukichangia nyuzi za ujenzi na magari humu JF, siku zote weka angalizo kwamba unachangia kulingana na kipato chako. Kuna watu mpaka adundulize aipate hiyo 25m ni shughuli pevu sana. Unadunduliza kununua gari ya 25m, wakati kwa wengine hiyo hata ushuru haitoshi. Ndo uhalisia wa maisha.

Ukichangia nyuzi za ujenzi na magari humu JF epuka hizi kauli, “mtanzania wa kawaida”, “mtanzania halisi”, vipato vya walio wengi” nk. Wewe pambana na Hali yako. Mtanzania wa kawaida hajulikani.

Siku zote; maisha yako ni ndoto ya wengi.
 
Kwenye mazingira kama ya Chanika,Mlandizi au Bagamoyo kwenye aridhi ya kichanga isiyozalisha nyufa Mil 25 Iinatosha kujenga na kupaua.. maana hauhitaji nondo nyingi km unajenga kwenye maeneo yenye udongo wa kinongo.
 
Back
Top Bottom