Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Mara nyingine nikiwaza mambo yanavyofanyika hapa Tanzaniia, naona kama tumekuwa jumuiya fulani katika uwanja wa fujo. Tunaishi kwa matamko ya Raisi, mawaziri, wakuu wa Polisi, wakuu wa mikoa na mara nyingine katibu mwenezi wa CCM!
Hivi hakuna watu wenye akili nchini, na hasa viongozi, wakaona hilo ni jambo la ajabu sana halipaswi kabisa kuwa namna yetu ya kuendesha mambo yetu?
Angalia kwa mfano hili la maandamano ya Chadema. Siku zote nilifikiri Chadema wameruhusiwa kuandamana kwa sababu uongozi wa Tanzania, kutia ndani Raisi Samia na viongozi na Polisi nchini, walikuja kutambua kwamba maandamano ya vyama vya siasa ni haki yao ya kikatiba. Kumbe si hivyo. Kinachoonekana kapa ni kwamba Chadema wanaandamana kwa sababu ya mapenzi binafsi ya Raisi Samia!
Ina maana kwamba, bila agizo la Samia kusema acheni Chadema waandamane, IGP, wakuu wa wa mikoa wa Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, walikuwa wamejiandaa kutoyaruhusu na hata kuwapiga Chadema virungu kama wangeng'ang'ania kuandamana! Ndio maana Chalamila mwanzoni alitaka hata kutumia JWTZ kuzuia maandamano ya Chadema, na aliacha yaeendelee kwa sababu tu Raisi Samia kwa amri yake binafsi, aliruhusu labda kwa kumpigia simu Chalamila asiyazuie, sio kwa sababu ya kanuni za kikatiba!
Hivi ina maana Raisi Samia naye anaona hivi ndivyo anapaswa kuongoza Tanzania? Kwamba kwa kila jambo dogo na kubwa awe anapigiwa simu, mama eeeh, tuwaache waandamane au tuwapige? Mama eeh, tumkamate Tundu Lissu au tusimkamate? Mama eeh, tuendelee kumshikilia Mbowe au tumwachie, maaam eeh, tumfunge Mbowe au tumwachie huru? Really Samia, you enjoy that?
Angalia maneno kutoka kinywani mwa DC wa Mbeya juu ya maandamano ya Chadema huko Mbeya, pale alipokuwa akijibu tuhuma za Sugu kwamba alijaribu kuyahujumu maandamano ya Chadema
"...alipotafutwa kuzungumzia kauli hiyo alisema ameisikia na anasubiri taarifa rasmi, huku akifafanua kuwa maandamano hayo yaliruhusiwa na Raisi Samia Suluhu Hassan ndio maana hakuna aliyezuiwa kushiriki"
Hivi Watanzania wenzangu, mnaona ujinga huu wa kiuongozi unaoendelea nchini? Kwamba hawa watu, wakuu wa mikoa, polisi, mawaziri nk, wanataka nchi hii iendeshwe kwa matamko ya Samia kwa kila jambo moja moja?
Na kama huyu DC Mbeya angekuwa anaona mbali, angesema maandamano yanafanyika kwa sababu ni haki ya kikatiba ya Chadema, lakini the poor guy ameshakuwa totally mind controlled kusubiri maagizo!
Kusema kwamba maandamano yanafanyika "kwa sababu Raisi Samia ameruhusu" inapaswa kuwa jambo la aibu kuwekwa hadharani si tu kwa Raisi Samia mwenyewe, bali kwa Tanzania kwa ujumla. Kimsingi, hata Chadema hawapaswi kukubali hili, kwamba wanaandamana kwa sababu ya huruma binafsi ya Raisi Samia. Chadema mkikubali hili, kuna siku Samia akiamka vibaya atamwambia IGP usiruhusu Chadema waandamane!
Tanzania tunapaswa kufanya mambo yetu kwa taratibu za kikatiba, sio utashi wa mtu mmoja mmoja hata kama mtu huyo ndio Raisi wa nchi, au waziri,au IGP au Katibu mwenyezi wa CCM nk. Namna hiyo ya uongozi haitatufikisha popote.