Kwa Hili la Salum Mwalimu, CUF Inastahili Pongezi ni Mwanzo Mzuri wa Reality ya UKAWA!.

Pasco u are always fair in your analysis, only that certain people have their interest of which if in your post you happen to provoke, they will call you "buku saba"! I hate such people but I cant change them!All in all its a good move that Chadema has at least one strong supported candidate in Zanzibar and CUF are in favour of him.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania hatujasahau chadema ni chama cha kikristo nakumbuka yule mpuuzi mmoja toka chadema alisamama bungeni na kuhoji kwanini migahawa ifungwe mwezi wa ramadhan zanzibar .. Wazanzibar wanaakili sana ardhi yao haitaingia najis kutawaliwa na CDM ...
Mkuu njiwa.

Hawa jamaa wanadhani watanzania wamesahu udini wa Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwa akili tako kina Tundu Lissu na wafuasi wa Chadema wanavyowatukana Wazanzibar halafu wawape kura.

Akili tako mwenyewe...
Aliewatukana Wazanzibar ni nani kati ya Pinda wa CCM aliesema Zanzibar ni mkoa wakati ile ni nchi huru, Lissu ni lini amewatukana wazanzibar???
 
Akili tako mwenyewe...
Aliewatukana Wazanzibar ni nani kati ya Pinda wa CCM aliesema Zanzibar ni mkoa wakati ile ni nchi huru, Lissu ni lini amewatukana wazanzibar???
Soma hii kiduchu.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman (Pichani) ameshangazwa na mwanasheria mwenzake Tundu Lisu kwa kutofahamu madhumuni na malengo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliozaa serikali ya umoja wa kitaifa.--Kauli ya Mwanasheria huyo aliitoa katika baraza la wawakilishi wakati akifafanua baadhi ya mambo ya kisheria baada ya wajumbe wa baraza hilo kumtaka afanye hivyo kufuatia kauli ya ya Tundu Lisu aliyoitoa bungeni wiki hii.-“Sasa kuja kwa haya yametuonesha kwamba kuna wenzetu kumbe wana fikra kwamba Zanzibar iliwahi kutawaliwa.--Maana mtu anaposema marekebisho ya 10 ya Zanzibar yamjitangazia uhuru maana yake ana fikra na huyu ni mwanasheria mtu kafika mpaka kuwa mbunge anayeaminika na chama chake lakini anasema kwa kufanya hivyo Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa?,” alihoji Othman.-Akijadili bajeti ya wizara ya makamu wa rais wa jamhuri ya muungano, huko Dodoma Mbunge wa Singida Mashariki wa Chama Cha (CHADEMA) Tundu Lisu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Zanzibar imefanya katiba kwa kujitangazia kuwa ni nchi.-Othman alisema marekebisho ya katika ya Zanzibar yalikuja baada ya hoja nyingi ambazo hazikuwa na majibu katika muungano ambayo ilikuwa ikisema ni Zanzibar ni sehemu ya muungano, lakini kama nini mkoa? Shehia? Kata? au kijiji?, haya hayakuwa na jibu katika katiba ya muungano.-Kufuatia maridhiano Zanzibar ndipo wazanzibari wakamaua kufanya kukufikia marekebisho ya 10 ya katiba yao ambayo ilifafanua kuwa zanzibar ni nchi na ndivyo ilivyo kwa sababu haikuwahi kutawaliwa kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanavyofikiria.-“Marekebisho ya 10 ilichofanya ni kusema kwamba ikiwa mtu hatambui, maana ilikuwa imeshaonesha dalili kwamba kuna wengine hawatambui hilo tena wakubwa. Sasa marekebisho ya 10 yalipokuja ni kufafanua tu, kama kuna mtu hatambui sisi wenyewe tunajitambua” alisema mwanasheria huyo huku akiungwa mkono na wajumbe kwa kupigiwa makofi.-Huku akishangiriwa na wajumbe wa baraza hilo mwanasheria mkuu alisema hakuna mtu ambaye atawazuwia kusema “Aaah katiba yenu isiwe namna gani au isiwe hivi na ndio maana unakuta katiba za muungano zipo nyingi lakini kila mmoja ina muundo wake kwa mujibu mlivyokubaliana nyinyi wenyewe.”-Mwanasheria mkuu alisifu muungano wa miaka mingi wa Uswizi ambao unatambulika na kuigwa duniani kutokana na kufuata misingi imara iliyowekwa na wananchi wenyewe.-Alisema muungano ambao umedumu na unasifiwa ni Swiss Federation kwa sababu umeanza tokea mwaka 1292 na umekwenda kwa mafahamiano hadi mwaka 1874 wakatunga katiba ambayo wameifanyia mapitio upya mwaka 1999 na nchi hiyo ina serikali 26, lugha nne rasmi na ndio muungano amabo umedumu na nchi ambayo ni imetulia duniani.-Mwanasheria huyo alisema mashirika yoye ya kimataifa yapo Uswizi kwa sababu ya muungano huo uliotumilia na kwa sababu umekuwa na misingi imara ya kuhakikisha muungano ule unaweza kuhimili mabadiliko yoyote yatakayokuja ya kisiasa.-“Mheshimiwa Naibu Spika nitumie fursa hii hapa hapa niseme wakati tupo katika mchakato wa maoni ya katiba nadhani ni wakati mzuri kuiweka sawa ile misingi ya muugano kama Uswizi,”na kuongeza: “Wakati mwengine napata wasiwasi nasema hii khofu yangu niiseme hapa kwamba tunaanza kubishana kuhusiana na watunza nyumba wawe wangapi, waendeshaji nyumba wawe wangapi, wawili, watatu, wanane au watano? Lakini tatizo letu la msingi mimi nadhani ni nyumba yenyewe iweje. Kama tunaamua kuishi, maana mfumo wa sasa hivi mmoja anaishi nyumba kubwa na mwengine mabandani huko uwani huo sio utaratibu tunao.”-Aidha aliwaambia wajumbe hao kwamba wanzanzibari wana mambo ya msingi ya kujadili kuliko kuzungumzia idadi ya watunza nyumba akimaanisha kero za muungano zilizopo na kushindwa kuafikiwa.-“Kwa hivyo mimi niwaombe sana waheshimiwa wajumbe, niwaombe na wazanzibari wenzangu na wananchi wote, kwamba huko mbele tusije tukalaumiana kwamba tumefanya marekebisho ya 10 kimakosa na tumejitangazia uhuru. Sasa hivi tuondoe fikra hizo lakini tunaweza kujieleza kwa hoja za msingi na mambo ya msingi katika hoja hii hapo ndipo tutakapojenga utawala bora ndani ya muungano,” aliongeza Mwanasheria huyo.-Akitoa ufafanuzi zaidi kwa wajumbe hao kuhusu muungano Othman alisema hata suala la uraia limepewa kipaumbele katika katiba ya Uswizi ambapo mtu anapozaliwa ndipo anapopewa uraia wake.-“Pale unapozaliwa ndio panapokupa uraia, na kuna mengi ambayo nadhani tatizo liliopo kwa wenzetu ni kwamba hawajifunzi kwamba muungano ni kitu gani. Muungano ni suala ambalo nchi mbili mnapoungana, nchi zilizokuwa huru ni suala la makubaliano na mtakachokubaliana ndicho ambachi kitakuja katika katiba yenu,” alisema Othman.-Othman ambaye ni mwanasheria aliyewahi kuandika waraka (paper) aliyoipa jina ‘masuala ya yasiokuwa na majibu ndani ya muungano’ aliwaambia wawakilishi hao kwamba maelezo ya Tundu Lisu yamejaa hadaa na yamejaa upotoshaji tena upotoshaji ambao umepindukia mipaka ya kweli.-“Mimi nimepata kusoma na kuangalia hiyo hutuba ya Mhe Tundu Lisu… lakini pia nimeona majibu ambayo yalitolewa na mhehsimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyesema kuwa maeelzo ya Mbunge Lisu yamejaa hadaa na upotoshaji naungana naye,” alisisitiza huku makofi ya wajumbe yakitawala ndani ya baraza hilo.-Tokea kuanza kwa kikao cha baraza la wawakilishi kwa kiasi kikubwa mijadala wa bajeti umetawaliwa na suala la muungano ambapo wajumbe wengi wamekuwa wakiungana na wananchi kudai maslahi zaidi kwa zanzibar ikiwemo kurejesha kwa hadhi ya rais wa zanzibar na mamlaka kamili ndani na nje ya nchi.
 
haa haa kwani wapiga kura lazima wawe wanachama wa chama hicho? mkuu leo umeamka vibaya ama..kwani wana cuf hawawezi mpa kura?

ebwana labda huyo hajajua maana ya ukawa, na nadhan hafuatilii siasa kwa ukaribu, sio lazima chadema iwe na wanachama wa kutosha kule Zanzibar, bali ile hali ya kuungana tu inawatia nguvu wanachama wa CUF kumpa kura salumu mwalimu kwan ni vyama tofauti lakini vyenye dhumuni moja.
 
Mnawafanya cuf hawana akili nyinyi jimbo la kikwajuni gumu ndo wamewachia chagadema mbona mji mkongwe hawatlitoi
 
Hawa ndio tunaowaita Masheikh Ubwabwa
Usiwe punguani wewe msome Tundu Lissu.

Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu amesema Muungano wa Tanzania umekufa kikatiba. Lissu aliyasema hayo wakati alipoulizwa msimamo wake juu ya rasimu ya katiba na muundo wa serikali katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango, Magic FM.-Akijibu swali hilo alitolea mfano wa wakati wa maadhimisho ya siku ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo alisema anaekagua gwaride na kupigiwa mizinga 21 anatakiwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye amiri jeshi mkuu lakini kwa sasa katika maadhimisho hayo rais wa Zanzibar ndiye anayefanyiwa yote hayo kutokana na katiba ya sasa ya Zanzibar kuitambua Zanzibar kama nchi.-Alisema "Katiba ya sasa ya Zanzibar inasema rais wa Zanzibar ni mkuu wa nchi ya Zanzibar, ni kiongozi wa serikali, ni Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Idara Maalum. Kimsingi sababu kubwa ya Muungano ilikuwa ni masuala ya ulinzi na usalama na Zanzibar imeyaondoa kwenye Muungano" na kumalizia kusema kuwa katiba ya sasa ya Zanzibar ya leo ni waraka wa Uhuru.Lissu alimalizia kwa kusema namna pekee ya kubaki na Muungano ni kuwa na serikali tatu huku akiwakosoa wanaosema mapendekezo ya tume ya katiba kuwa serikali tatu ni gharama wanakosea kwani hakutakuwa na gharama kubwa kwa kusema kutakuwa na jumla ya wabunge 314 tu tofauti na sasa ambapo kuna jumla ya wabunge 438 tu.-Hata hivyo alipoulizwa kama CHADEMA inaona kuna haja kuwepo Muungano alisema ipo na kuongezea "Ndoa ya kulazimishana hapana, kama upande mmoja unataka out is out". Lissu alimalizia kwa kusema wananchi wa kawaida wa Zanzibar hawautaki Muungano kwani hawaoni faida yoyote.-Katika Mahojiano hayo ya muda wa saa zima, Tundu Lissu aliongelea mambo mbalimbali ikiwemo suala la kodi ya kadi simu.-
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye green nyongeza yake hii hapa...
"Wakati uandikishaji ukitakiwa kuendelea huko mwanza, taarifa zinasema uandikishwaji unaonekana kushindikana", maana hata wale waliokuwa watoe semina ya matumizi ya hizo BVR hawakuwepo
Mleta mada hilo ni sawa, ila hii hofu inayoendelea ya kuhusu kutokuwepo uchaguzi mkuu mwaka huu umeiona? Ww kwa kuwa uko karibu na jikoni una maoni gani? Dalili za dhahiri kwangu ni hilo zoezi la BVR linavyofanyika kwa hila na mwendo wa konokono wakati muda si rafiki.
 
sheikh ubwabwa umechanganyikiwa
Msome Padre Slaa hapa chini.

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuhujumiwa na Chama chaDemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana 'kauli za kichochezi' zinazotolewa dhidi yake kuhusu sababu za kukataa kushirikiana nao bungeni.-Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema kuwa licha ya kuhujumiwa na CHADEMA lakini pia wanasikitishwa na kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa kwa kudai kuwa CUF sio chama cha upinzani nchini."Tunasikitishwa na kauli hiyo ya Dkt. Slaa na nikimnukuu anasema kuwa 'CUF siyo chama cha upinzani Tanzania tena, eti kwa sababu kiko serikalini Zanzibar' na kwa hiyo CHADEMA hawawezi kushirikiana na CUF katika kuunda kambi ya pamoja bungeni.-"CHADEMA wanaishambulia sana CUF hivi sasa, wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kitendo cha CUF kuwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni dhambi kubwa mno na kuwa Watanzania wasiiunge mkono CUF Tanzania bara, jambo ambalo ni ndoto za alinacha na kamwe halitatokea kwani Watanzania wa sasa hawadanganywi kwa propaganda zisizo na maana,"aliongeza.Kauli ya Bw. Mtatiro inatokana na Tamko la Kamati kuu ya CHADEMA lililotolewa na Dkt. Slaa, kuwa CC ya chama hicho imemuagiza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli kwa kuhusisha wabunge wa CHADEMA pekee.Akitoa tamko hilo, Dkt. Slaa alisema: "Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, kamati kuu imezingatia kuwa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na CCM kuunda Serikali ya Umoja Wa kitaifa."Na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za muungano na kwa kuwa vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge vimo katika ushirikiano na CUF, Kamati Kuu imeona kuwa CHADEMA haiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo."Sasa kwa mfano tukiazimia kitu kinachopingana na serikali, Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye Makamu wa kwanza wa Rais huko Zanzibar unategemea atakubaliana nacho ili apingane na serikali, hivi vyama vingine navyo tayari vimeshakuwa sehemu ya watawala maana wameamua kushirikiana na CUF katika kamati yao," alisema Dkt. Slaa.Akizungumzia maazimio hayo, Bw. Mtatiro alisema kuwa CUF haiwezi kuwalamba miguu viongozi wa CHADEMA kwani hakuna faida yoyote wala umuhimu ambao wao wameonesha tangu walipojaribu kila namna kuwafanya wafanye kazi kwa umoja na vyama vingine na kugonga ukuta."Mara zote CHADEMA wamekuwa na historia ya kuvisaliti vyama vingine vya upinzani huku wakikimbilia kwa umma kuomba waungwe mkono wao peke yao," alidai.Aliongeza kuwa CHADEMA kina matatizo mengi sana tangu mwaka 2007, na waliwavumilia kwa kiasi kikubwa na hata baada ya uchaguzi mkuu kuisha mwaka jana, CUF iliiomba CHADEMA iweze kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuwa na kambi ya upinzani imara zaidi na yenye nguvu."CHADEMA walikataa kabisa suala hili kwa maelezo kuwa “wao wako tayari kuungana na CUF tu katika kambi ya upinzani na kuwa hawaviamini vyama vya NCCR, TLP na UDP, na tulijaribu kuwasihi lakini hawakutaka kubadili msimamo huo.-"Lakini baada ya yote hayo, jana (juzi) CHADEMA wametoa kauli ya kinafiki,- eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza dola, yaani CUF na kuwa wao CHADEMA wako tayari kushirikiana na NCCR-Mageuzi," aliongeza.Bw. Mtatiro alisema kuwa hivi karibuni NCCR ndio walikuwa kikwazo kwa CHADEMA kushirikiana na vyama vingine, hata mwezi haujapita wamegeuka na kudai CUF ndiyo adui."CHADEMA ni chama popo sana, hawajui wanachofanya, wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20 Tanganyika, sasa hawana haja na CUF na vyama vingine, wanadhani majimbo 20 ndio Ukombozi wa Tanzania umemalizika.-“Ni sawasawa na maskini sana anayeamka ghafla anajikuta tajiri, hajui namna gani atatumia utajiri wake, anaanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umaskini wao, anawatukana majirani huku anaendelea kuponda mali na wasichana warembo katika kijiji hichohicho, siku moja mali zinaisha……hadithi ya tajiri mjinga inaishia hapo," aliongeza Bw. Mtatiro kwa jazba.Aliendelea kukishutumu chama hicho kuwa kinafanya kusudi kutoa kauli za kichochezi, wakiamini kuwa CUF ikifa bara wao watapumua mno.Alisema ni wazi CHADEMA wanaiogopa CUF, huku wakifahamu fika kuwa chama hicho kina mtandao mkubwa na kina mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi.Bw. Mtatiro alidai kuwa kitendo cha CHADEMA kuwadharau Wazanzibari, kudharau maamuzi ya wananchi wa Zanzibar katika nchi yao, kudharau katiba ya Zanzibar ni kitendo cha kijinga mno.-"Wazanzibar ndio walioamua kwa kupiga kura kuwa wanahitaji serikali yao, ya umoja wa kitaifa kwa maslahi ya nchi yao ya Zanzibar kwa kujali amani maendeleo na ustawi wa taifa lao."Wazanzibari ndio walioamua kuwa chama kitakachoongoza katika uchaguzi kitatoa rais na mawaziri na cha pili kitatoa pia makamu wa kwanza wa rais na mawaziri. Wakapiga kura, wakatoa maamuzi haya, wakayaingiza katika katiba yao ya Zanzibar katika mabadiliko ya 10 ya katiba," aliongeza.Alisema ni ujinga kudai CUF kuwa katika mfumo wa serikali iliyoamuliwa na wananchi katika upande mmoja wa nchi ni dhambi.---Alihoji kuwa, CUF ilipopata nafasi ya pili Zanzibar CHADEMA walitaka ikiuke matakwa ya wananchi na kukataa kuingia serikalini ili iwafurahishe CHADEMA ambao Zanzibar hawana hata mjumbe wa mtaa wala tawi?"Nani asiyejua kuwa CUF ni chama chenye nguvu na mtandao Zanzibar na Tanganyika na ni chama cha pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande zote za muungano? Nani asiyejua kuwa CHADEMA ni chama kilichoko Tanganyika peke yake?"Nani asiyejua kuwa CHADEMA kinaumizwa sana na mafanikio na utulivu wa kisiasa Zanzibar yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na busara na viongozi wa CUF ambao hawakuweka maslahi ya chama mbele katika kulinda uhai na maisha ya Wazanzibar?" alihoji.Bw. Mtatiro aliyewania ubunge katika Jimbo la Ubungo na kushindwa na Bw. John Mnyika wa CHADEMA, alidai kuwa CUF kama chama chenye nguvu kubwa Zanzibar watazidi kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi kila mara bila kujali kama CHADEMA watakasirika au la.Aliongeza kuwa chama kipi ili kuwatumikia Watanzania, kuwatetea katika madhila yote na manyanyaso wanayofanyiwa."Tutaendelea kuwa katika SUK na kulinda maamuzi na matakwa ya wananchi wa Zanzibar lakini kwa upande wa Tanzania bara ambako katiba iko wazi, kuna chama kimoja kinachoongoza dola na vingine vyote vikiwa vyama vya upinzani, tutaendelea kuheshimu matakwa ya kikatiba yaliyopo Tanzania bara," alisema.Aliwataka CHADEMA wafahamu kuwa CUF kitazidi kuwa chama cha kitaifa kwa kuzidi kupata wabunge wengi kutoka Bara na Zanzibar, kujiimarisha pande zote za nchi hadi waione njema inayosubiriwa na Watanzania wote.Bw. Mtatiro aliongeza: "CHADEMA na watu wote wanaoitakia mabaya CUF watakufa na kukiacha chama hiki kikishamiri kama tegemeo la pekee la Watanzania," alisema.
 
Back
Top Bottom