Kwa hili, Kigwangalla ujizulu

hivi upo aware kuwa hakuna sheria inayowaruhusu watu wa afya formal au informal asector kutangaza biashara au huduma zao kwenye vyombo vya habari? zaidi ya mabango kwenye sehemu husika? do research.
Hii issue nilikua sijui... ila mitishamba ndo wanaongoza kutangaza.... na sheria inasemaje kuhusu adhabu kwa kufanya hilo
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoDk. Hamis Kigwangalla alipotembelea Kituo ya Tiba Asilia ya Fore Plan Clinic kilichopo Ilala -Bungoni, Dar wiki chache zilizopita.

Na Waandishi Wetu

WAKATI idadi ya watu wanaoamini katika tiba ya mitishamba badala ya hospitali ‘Tiba Mbadala’ inayotolewa na kliniki mbalimbali nchini ikizidi kuongezeka, Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ imebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya matabibu katika tiba hizo, Risasi Jumamosi linakumegea.



Baadhi ya madawa

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa mhudumu wa kliniki maarufu jijini Dar (jina lipo), madawa mengi yanayotolewa kwa wagonjwa si ya asili kama yanavyotangazwa, ni mchanganyiko wa vumbi la miti pori isiyo na sumu na dawa za kisasa zinazopatikana hospitalini ambazo husagwa.



Majani ya Mlonge

“Sikia, tunafahamu kinachoendelea tunakaa kimya kwa sababu tunapata riziki. Katika dawa mia moja utakazoambiwa ni za asili, mbili au tatu ndiyo kweli zimetokana na mitishamba moja kwa moja, nyingine siyo,” alisema mhudumu huyo.

KWANI INAKUWAJE?
“Kwa mfano kuna watu wanakuja kwa maumivu ya miaka mingi ya mgongo au mwili, kinachofanyika ni kuchukua vidonge vya kisasa vinavyotibu au kupunguza maumivu na kuvichanganya na vumbi la miti hiyo halafu mgonjwa anapewa. Sasa kama mtu atapata nafuu kidogo, anaona ni kweli jamaa ni wataalam.

WATU WAMIMINIKA
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, watu wengi, hususan wanawake, wamekuwa wakimiminika kwenye kliniki mbalimbali zinazotoa tiba mbadala wakiamini watapata nafuu, hasa kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakiteseka kwa miaka mingi bila kupata nafuu mahospitalini.



Quatam Magnetic Analyzer

KIFAA CHALALAMIKIWA
Uchunguzi wa OFM umebaini kuwa kuna kifaa kinaitwa Quatam Magnetic Analyzer, matabibu wengi hawana ujuzi wa kukitumia lakini wanakitumia kuwarubuni watu kuwa kinatoa majibu ya magonjwa ya mwili mzima.



NINI MADHARA YAKE

Gazeti hili liliwasiliana na daktari bingwa mmoja wa (jina kapuni) na kumsimulia kinachotokea kwa tiba mbadala ambapo alisema kama ni kweli, wanaokwenda kutibiwa katika baadhi ya kliniki hizo, wana hatari ya kuyafanya magonjwa yao kuwa sugu au kuambukizwa mengine.
“Dawa za hospitalini zina vipimo vilivyowekwa kwa matumizi ya binadamu na kila dawa ina ujazo wake kulingana na matumizi. Mfano dawa ya kuponya uvimbe, haitakiwi kuwa katika mchanganyiko ambao haujaandikiwa na daktari.
“Unapochanganya na unga wa miti, unaweza kuua nguvu ya dawa na kumfanya mgonjwa kutopata nafuu au kuzua kingine, maana hujui nini kinazaliwa pale ambacho kinaweza kusababisha ugonjwa mpya au hata saratani.”

HUYU HAPA MTOA TIBA
Mtoa tiba mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mloe, akiwa hajui yupo na OFM, alikiri kuwa baadhi ya watoa tiba ni waongo katika kutoa huduma hiyo kwa lengo la kujiingizia mamilioni ya shilingi.
“Haya mambo yapo hapa Bongo. Tunawapa madawa yaleyale ya hospitalini, lakini sisi tukiwa tumeyachakachua na kuyaweka kwenye makopo kisha kuyapachika majina. Tunafanya mchanganyiko huo ili ulete maana halisi ya tiba mbadala.

“Kwa mfano anayeugua kisukari, unampa mchanganyiko utakaompa nafuu, akija mara ya pili unamuonesha dawa nyingine ambayo unamhakikishia itamaliza tatizo lake na unamtajia bei kubwa, anatoa akiamini atapona na sisi tunapata pesa,” alisema tabibu huyo.



TABIBU JJ MWAKA

Hivi karibuni, tabibu wa tiba mbadala, Juma Mwaka Juma ‘JJ Mwaka’ aliingia katika figisufigusi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto baada ya naibu waziri wa wizara hiyo, Dk. Hamis Kigwangalla kuibuka kwenye kliniki yake, Ilala jijini Dar kwa kufanya ukaguzi.

Katika ziara hiyo ya ghafla, inadaiwa, Mwaka aliingia mitini hivyo kutakiwa kuwasilisha wizarani vibali vinavyomruhusu kutoa huduma agizo ambalo alilifanya na kubainika ana sifa. Kuna taarifa yeye na Tabibu Simon Rusigwa wamebainika kuwa na vyeti halali baada ya kuchunguzwa tiba zao.



TABIBU FADHILI

Huyu naye juzikati aliingia kwenye songombingo la kudaiwa kuchunguzwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba, ana harufu ya kukwepa kodi. Lakini mwenyewe alisema yuko sawa, hadaiwi na TRA wala hana magumashi kwenye huduma yake.

Juzi, saa 8: 14 mchana, Risasi Jumamosi lilimtafuta Dk. Kigwangalla ili kumsikia anasemaje juu ya kuwepo kwa madai hayo. Hata hivyo, simu yake iliita bila kupokelewa. Chanzo.GBP
 
Sheria ya madaktari kujitangaza iko wazi, hata professional doctors n the same! Wanajulikana kwa tafiti zao, kwa hiyo hao madaktari wanachotakiwa n kutangaza dawa zao sio uganga wao! Waende muhimbili kitengo cha tiba asili na TFDA wakaverify dawa zao, then waanze kuzitangaza dawa zao sio kupiga hadithi zisizo na kichwa wala miguu
 
Kufuatia kigwangala kuwapiga stop waganga wa tiba asilia kujitangaza kwenye vyombo vya habari na kuwawekea mikiriti kibao,leo waziri wake ametoa kauri ya kuwakaribisha wataalam hao wa tiba mbadala kufanya mashauriano bila kutumia utemi,kigwangala umechemka wajibika
huyu achana nae wala hafiki kokote atakuwa wa kwanza kufukuzwa
 
no need. matapeli wamezidi sana mjini na vijijini. siku hizi utansikia mganga anakwambia mizimu inataka kitimoto rost, bia creti, raba mpya andy1, jeans mpya na t-shirts pamoja na iPhone 6.
ukimpelekea vyote hivyo anakwambia mizimu imeona tatizo lako na itakuponyesha ukienda hospitali.
Rudisha Picha ya bujibuni bana au hata weka nyingine inayoweza kumuwakilisha bujibuji vizuri.
 
Naibu yupo sahihi, hawa jamaa wanapiga pesa kwa njia haramu, wawajibishwe.
 
Mkuu kigwangala ajiuzuru tu
Wamwone nani?kiranja wake kesha sema atakutana nao sijui aibu hiyo ataificha wapi huyo kigwa
Umeonaeeee?
Nani anakulazimisha kwenda?
Hiyo avatar yako tuinakuhukumu pamoja na id yako
Kweli kabisa kigwa kakrupuka ili kutafuta kiki
Kigwa ameingia kwa kulipiza visasi tu
Ebu jiangalie kmono wako wa kulia kuna kitu kama nyoka
inaonekana ni mwathirika wa hili katazo...pole mkuu ndio mambo ya sheria
 
Kufuatia kigwangala kuwapiga stop waganga wa tiba asilia kujitangaza kwenye vyombo vya habari na kuwawekea mikiriti kibao,leo waziri wake ametoa kauri ya kuwakaribisha wataalam hao wa tiba mbadala kufanya mashauriano bila kutumia utemi,kigwangala umechemka wajibika
kigwangala sio smart sana kwenye maamuzi yake mengine ili kwa hili alikua sahihi, huwezi ukafanya issue ya afya za watu ikawa soko huria mkuu, hata huyo waziri sidhani kama ataawaachia freely kama zamani, sekta ya afya ilikua pango la walanguzi
 
kigwangala sio smart sana kwenye maamuzi yake mengine ili kwa hili alikua sahihi, huwezi ukafanya issue ya afya za watu ikawa soko huria mkuu, hata huyo waziri sidhani kama ataawaachia freely kama zamani, sekta ya afya ilikua pango la walanguzi
Kwa mnavyowashambulia viongozi wa serikali ya kikwete naamini hata serikali hii ikimaliza muda wake mtaishambulia hivyo hivyo wakati nyinyi wenyewe ndio mlio wachagua
 
inaonekana ni mwathirika wa hili katazo...pole mkuu ndio mambo ya sheria
Kigwangala hana ubavu wa kushindana na kumshinda waziri wake na kama alikuwa anatafuta kick sasa ndio kagonga mwamba
 
Kwa mnavyowashambulia viongozi wa serikali ya kikwete naamini hata serikali hii ikimaliza muda wake mtaishambulia hivyo hivyo wakati nyinyi wenyewe ndio mlio wachagua
oya mimi mbona sijamshambulia mkuu? na kwa taarifa yako sikumchagua pia
 
Sheria ya madaktari kujitangaza iko wazi, hata professional doctors n the same! Wanajulikana kwa tafiti zao, kwa hiyo hao madaktari wanachotakiwa n kutangaza dawa zao sio uganga wao! Waende muhimbili kitengo cha tiba asili na TFDA wakaverify dawa zao, then waanze kuzitangaza dawa zao sio kupiga hadithi zisizo na kichwa wala miguu
Miaka yote walivyokuwa wanafanya hivyo serikali ilikuwa wapi?
 
Mbona na yeye ni Dr.wa tiba asili yeye alivyopata ulaji anataka kuwageuka wenzie,amshukulu WAMA.
 
Back
Top Bottom