abulaaliyah77
JF-Expert Member
- Oct 13, 2021
- 1,750
- 1,156
AiseeeMama anakosea sana kuachana na kundi la wanyonge ambao ndiyo wengi na kuanza kukumbatia kundi la walichonacho ambao hawazidi hata millioni 3 nchi nzima
Wametangaza bei ya kuunganishiwa umeme ibadilishwe kutoka elfu 27 lakini ukumbuke umeme siyo anasa ni hitaji la msingi kwa wananchi wote bila kujali vipato vyao pia kila tukinunua LUKU tunakatwa hela ya kusambaza umeme.
Hiyo hela inaenda wapi?
Unajua ni kwa nini awamu ya tano mliweza kuunganisha umeme kwenye zaidi ya vijiji elfu 8? Kwa hali hii mtaweza kumaliza vijiji elfu 2 vilivyobaki? Unajua kuwa vijijini miundombinu ni mbovu kabisa na nguzo za umeme hakuna ,kwa hiyo hao ndiyo wapandishiwe bei ya kuunganisha?
Alianza waziri wa nishati January Makamba kuwadanganya watanzania kuwa mgao wa umeme unaotikisa nchi kwa sasa unatokana na awamu ya tano kuzuia maintanance baada ya hayati Magufuli kusema hataki kusikia mgao wa umeme na hivyo vifaa kupata uchakavu uliosababishwa na kuwaka mfululizo kwa miaka 5!.
Kabla ya uongo wake haujakauka Tanesco wamesema mgao wa umeme unasababishwa na kupungua kwa maji kwenye mabwawa na siyo regular maintanance iliyosemwa na Makamba.
Kwenye mkumbo wa kusema uongo hadharani aliingia pia waziri wa uwekezaji Godfrey Mwambe baada ya kuwadanganya watanzania kuwa hakuna mkataba wowote uliowahi kusainiwa kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo!
Mwambe bila kujali onyo la wahenga linalotaka kuogopa Mungu na technologia akasahau kuwa kuna video ikionyesha rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi ujenzi wa bandari ya Bagamoyo!
Je jiwe la msingi huwa linawekwa bila mkataba wowote? Swali hilo atajibu Mwambe.
Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.
Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.
Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.
Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?
Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege
Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?
Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?
Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?
Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa??
*Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.
Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
*
Muda utaongea .