Kwa akili hizi za Watanzania, tunahitaji Rais mkali zaidi ya Magufuli

1. Bado nchi inawatu wazembe sana na walalamishi.
2. Maofisini bado watu utendaji wao upo chini sana...refer mradi wa maji Lindi.
3. Ndani ya CCM bado hawaamini kuwa mambo yamebadilika.
4. Upinzani ndiyo hovyo kabisa kazi yao kutetea bangi, madawa ya kulevya na watu wenye harufu ya ufisadi.
5. Wakuu wa mikoa na wilaya kila siku wanakurupuka kurupuka tu kwenye maamuzi yao.
Nafikiri tunahitaji Rais atakaye tawala kwa MKONO WA CHUMA
Unatumia hisia fanya tafiti utajua kuwa uongozi si ukali bali kufuata sheria pekee kwa kila mmoja.
 
Sasa ukali wa Raisi utarekebisha uchumi? au ukali. wa raisi una tija gani katika maendeleo? ni ujinga kuamini ukali unaweza leta maendeleo yoyote, kwanza watu wakali hua na uoga ndani yao...
 
UKIAPA KUILINDA KATIBA ALAFU UKAKENGEUKA HAKIKA UTAANGUKA TUU. TENA KIAPO CHA HADHARANI HUKU UMEBEBA KITABU KITAKATIFU!!.
KAULI MBAYA KABISA NI ILE YA KUSEMA KWENYESERIKALI YANGU HAKUNA MPINZANI (VYAMA MBADALA) ATATIA MGUU!! HUU NI UBAGUZI MBAYA SAAANA,MUNGU ATUSAIDIE.
 
Tuko ovyo kwakweli. Mauwizi kila kona. Halafu wanaoiba wanaona ni haki yao kuiba. Maadili yetu yako ovyo sana. Uvivu na vitu vinavyoonekana haviendi na taratibu, Sheria na kanuni zilizopo ndo vinaonekana vitu vya maana na hao wafanyao hao huonekana kama wajanja.

Hata uwizi unaitwa ujanja
Huyo mwenyekiti wako mbona hatuelezi ukweli kuhusu kile chombo alichowapiga changa la macho watanzania? Au unataka tuanze kulist ya kwake? Mtu kama huyo ana uwezo au dhamira ya kusafisha au ni kuendeleza chuki na visasi kwa kwa wanaompinga na maadui zake wa kisiasa?
 
Ina maana kwa uelewa wako ukali ndiyo unaotawala. Yaani ukitaka kutawala vema uwe mkali. Daah kweli tuna safari ndefu ya viwanda na mimi kabla sijaingia humu nilisikia kuwa huku ndo kuna magreat thinker kumbe ndiyo nyie ama na wewe mgeni kama mimi. Hata baba mkali watoto wake huishia kubebea mimba nyumbani. Kuna ethic zinazoambatana na ukali ili kuwa kiongozi bora ambazo yule jamaa hana.
 
Huo ukali utaleta unafuu wa maisha? Tunatakiwa tupate Rais anaejitambua na kutambua matatizo ya wananchi,sio mtu anakurupuka kuchukua form ya urais na kugombea kimasikhara.
Tunaitaji Rais mwenye maono ya maendeleo na uwezo wa kuongoza watu na sio kufoka na kuongea ovyo.
Sasa kama ninyi Ukawa mtu anatuhumiwa anatumia bangi ninyi ndio kwanza mnamkumbatia na kumpa ulinzi, kwa nini msifokewe?
 
Kama umewahi kusoma kitabu cha " mfalme juha" na hii ndio style yake ya uongozi
 
Machadema yameparaganyika kwa ukali huu w Magu haitaji watetezi wa wala bangi
 
Muhimu ni kujenga mfumo imara ya uendeshaji,na taaluma ziheshimike!
Fikiria kiongozi,adanganya anapewa kura.
Fikiria kiongozi,anaiba kura na ushindi.
Fikiria tatizo kubwa lipo kwenye elimu,Kiongozi anatafuta mambo ya kumpa umaarufu!
Fikiria taifa linazalisha ' division zero' kwa asilimia kubwa.
Fikiria asilimia kubwa ya wananchi nivijana,halafu hawana elimu,wala ubunifu.
Ukweli unapindishwa,siasa inafunika taaluma.
Viashiria vya ubora katika jamii vipo chini.
Hatakiwi mtu bali mfumo utakao dhibiti mapungufu.!
 
Nmependa hapo mwishoni mkono wa chuma,,safi kulala SAA kumi na mbili,,asie na kazi akafyeke mapori,Kuweka adhabu kunyongwa hadharani,Hapo sawa
 
1. Bado nchi inawatu wazembe sana na walalamishi.
2. Maofisini bado watu utendaji wao upo chini sana...refer mradi wa maji Lindi.
3. Ndani ya CCM bado hawaamini kuwa mambo yamebadilika.
4. Upinzani ndiyo hovyo kabisa kazi yao kutetea bangi, madawa ya kulevya na watu wenye harufu ya ufisadi.
5. Wakuu wa mikoa na wilaya kila siku wanakurupuka kurupuka tu kwenye maamuzi yao.
Nafikiri tunahitaji Rais atakaye tawala kwa MKONO WA CHUMA
Mimi nasema tunahitaji Katiba mpya yote hayo yatamalizwa na Katiba mpya hata katiba mpya haitoshi pia bila utawala wa Sheria
 
Huo ukali utaleta unafuu wa maisha? Tunatakiwa tupate Rais anaejitambua na kutambua matatizo ya wananchi,sio mtu anakurupuka kuchukua form ya urais na kugombea kimasikhara.
Tunaitaji Rais mwenye maono ya maendeleo na uwezo wa kuongoza watu na sio kufoka na kuongea ovyo.
Unamaanisha kuwa yule fisadi Mkuu ambaye hata mia tank ikipita mbele yake basi Luna percent yake ndo angepaswa kuwa rais? Yaani nywele nyeupe
 
Unamaanisha kuwa yule fisadi Mkuu ambaye hata mia tank ikipita mbele yake basi Luna percent yake ndo angepaswa kuwa rais? Yaani nywele nyeupe
Jamaa kaongea point ila wewe unaanza kuvuruga kabisa, sidhani kama kafikiria hivyo aisee
 
Back
Top Bottom