Kuyeyuka na kupotea kwa Mimba

OCC Doctors

Senior Member
Jul 20, 2018
111
169
Kifuko cha ujauzito baada ya mimba kutunga (gestational sac) ni muundo uliojaa maji unaozunguka kiinitete (embryo) wakati wa wiki chache za ukuaji wa kiinitete.

Tatizo la Kuyeyuka kwa mimba 'Blighted ovum' hutokea pale ambapo kifuko cha ujauzito (gestational sac) kinakua bila kiinitete (embryo), hutokea ikiwa kiinitete hakikui. Kawaida hugunduliwa katika wiki za kwanza za ujauzito kupitia ultrasound. Dalili ni maumivu ya tumbo na kutokwa damu kidogo.

Sababu kubwa ya mimba kuyeyuka huwa ni shida ya vinasaba (chromosomal abnormality) ambapo kunakua na hitilafu za kimaumbile wakati wa mgawanyiko wa seli za uzazi.

Wakati wa kurutubishwa kwa yai, kikawaida yai huanza kujigawa muda mfupi baada ya kurutubishwa na mbegu ya kiume. Baaada ya siku 10, seli zinazojigawa ndio huunda kiinitete.

Mimba kuyeyuka inamaanisha kiinitete hakiundwi. Shida hizo za vinasaba huweza kupelekea mwanamke kubeba mimba ambazo hazifiki hitimisho.

Status-Post.jpg
 
Samahani kwa kuingia deep mtaalamu, unnecessary but I have to ask maana nina interest kubwa na uwanja wa embryology..

Stage ya kuunda kiinitete (embryo) sio siku ya 12?
Maana day 0-3, cleavage inakua katika morula stage, day 4-8 ni blastocyst stage na day 9-12 ndio embryonal stage.

Naomba unieleweshe kwenye mapungufu.
 
Back
Top Bottom