Niko Sehem Nawasikia Vijana Wadogo Tu Wa Kisambaa Wakipiga Stori Zao Kwa Kisambaa Bila Tatizo, Huku Wakichombezea Na Kiswahili. Ni Hapa Dar. Hii Ni Tofauti Sana Kwa Wachaga Hasa Wamarangu. Watoto Tangu Wakiwa Vidudu Wanapigwa Mkwara Hakuna Kuongea Kichaga. Wanakua Na Dhana Hiyo Hadi Ukubwani Kisha Wanaona Soni Kuongea Kilugha. Napendekeza Pawe Na Siku Ya Kuongea Kilugha Ili Kutopoteza Hizi Lugha. Nawapa Big Up Wapare, Wamachame, Wakibosho, Wamasai, Wahaya Na Wengine Wanaodumisha Tamaduni