Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,140
- 26,092
Sasa hivi kuungua masoko huria si kitu cha ajabu.
Masoko yanaungua kila leo.
Soko Kuu Kariakoo
Soko la Karume
Soko la Mbagala
Soko la Moshi
Soko la Geita
Soko/Mall ya Mwanza
Haya ni ndani ya hiki kipindi kifupi tu.
Nenda Masoko mengine hapa Dar, hali ni ile ile.
Uchafu wa wiki iliyopita bado upo.
Wafanyabiashara wamejazana hadi watu kupishana kwa kukwepesha mabega.
Mahali pa watu 10 wapo watu 30.
Hapa mtu anauza ndizi, mwingine anauza mawese kwa madebe, na mbele mafuta ya nazi.
Hakuna usimamizi wa aina yoyote.
Halmashauri la kwao ni kukusanya ushuru wa siku tu!
Hamna cha afya wala usafi!
Na anayevuta sigara hana pa kuitupa.
Kwa nini soko lisiungue?
Cha ajabu wanasiasa wanaliona hilo, Mkuu wa Mkoa analiona hilo, Halmashauri wanaliona hilo.
Soko likiungua wanakuwa wa kwanza kutoa pole na kuunda "
kamati za kuchunguza moto".
Hili litaendelea mpaka lini?