Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,984
- 32,128
KUTOKA MAZIKONI: CHIRAU ALI MWAKWERE, JUMA MWAPACHU NA ALLY SYKES
Ally Sykes hakupata kunieleza kama alipata kukutana na Chirau Ally Mwakwere.
Ali Mwakwere ndiyo kanifahamisha jana tukiwa Pande kumzika Juma Mwapachu.
Pande iko kilomita kiasi cha 10 kutokea Tanga mjini na ndiyo kijiji alichozaliwa Hamza Kibwana Bakari Mwapachu mwaka wa 1913.
Tuko Tanga Chumbageni nyumbani kwa kina Mwapachu msibani ni asubuhi kiasi cha saa nne visomo vimeanza.
Nimekaa na Salim Aziz tunajuana miaka mingi nilipokuwa Tanga.
Ali ananiambia Chirau Ali Mwakwere anakuja kutoka Nairobi kuhudhuria maziko.
Salim anaendelea kunieleza kuwa yeye na Ali Mwakwere wamesoma shule moja Shimo la Tewa, Mombasa na ni mtu wake wa karibu sana.
Tukiwa pale mazikoni akawa anawasiliana na Ali Mwakwere akamfahamisha Jumbe Menye aliyekuwa MC ajitayarishe kumpokea Muheshimiwa Chirau Ali Mwakwere muda mfupi ujao.
Salim Aziz akanifahamisha usuhuba uliokuwapo baina ya Juma Mwapachu na Ali Mwakwere.
Alipomaliza mimi nikamwambia Salim Aziz kuwa mimi kisa cha Wadigo hawa wawili wasomi wa haja kukutana nimekipata kwa mwenyewe Juma Mwapachu.
Kisa hiki Ali Mwakwere kakieleza msibani aliposimama kutoa rambirambi na In Shaa Allah nitaiweka video yake hapa mumsikie mwenyewe akizungumza.
Mimi ninachotaka kukisema hapa ni kuwa Juma Mwapachu aliniambia kuwa Chirau Ali Mwakwere alishangaa na pia kushtuka kumkuta Mdigo mwezake Balozi Ufaransa.
Katika mazungumzo sasa ndiyo Juma Mwapachu akamweleza Mwakwere historia ya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu kuwa alisoma Makerere.
Juma Mwapachu akamweleza Ali Mwakwere historia nzima ya baba yake na harakati zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na mchango wa baba yake kumpa Julius Nyerere uongozi wa Tanganyika.
Ali Mwakwere akamuahidi Juma kuwa yeye anakwenda kwao Kwale ambako ni mbunge na ataitisha kikao maalum agenda ikiwa Hamza Kibwana Bakari Mwapachu apewe mtaa Kwale kama Mdigo wa kwanza kusoma Makerere.
Hili lilifanyika.
Kwale kuna Mtaa wa Hamza Mwapachu.
Tuko Pande.
Salim Aziz ananiambia, "Mohamed Ali Mwakwere kaniuliza kama umekuja mazikoni, nikamwambia mbona tulikuwa na wewe pale tumekaa pamoja?"
Kiasi cha watu wawili wakaniambia kuwa Ali Mwakwere ananitafuta.
Hapa tuko nje ya msikiti wa Pande tushasalia jeneza tunaelekea makaburini.
Hivi ndivyo nilivyokutana na Chirau Ali Mwakwere.
Mimi nikamfahamisha kuwa tulikaa jirani ndani Masjid Riadha, Lamu Maulidini mwaka wa 2009.
Ali Chirau Mwakwere akanifahamisha kuwa amesoma kitabu cha Abdul Sykes na chanzo chake ni Ally Sykes.
Ali Chirau anasema alikuwa Muthaiga Country Club akamuona mzee mmoja kakaa kwenye meza na mkewe.
(Hapa napenda kutahadharisha kuwa kumuona Mwafrika Muthaiga si kitu cha kawaida kwani hiyo ni "Exclusive Club" ya mamilionea).
Ali Mwakwere akanyanyuka alipokaa akaenda kumsalimia yule mzee.
Yule mzee akajitambulisha kuwa jina lake ni Ally Sykes.
Chirau anAli Mwakwere anasema Ally Sykes alimletea kitabu cha Abdul Sykes na ile bahasha ameihifadhi hadi leo.
Kitabu hiki kilimuathiri sana Chirau Ali Mwakwere.
Anasikitika kuwa alipokuja kuwa Balozi wa Kenya Tanzania Ally Sykes alikuwa keshafariki.
Msikilize Chirau Ali Mwakwere hapo chini:
View: https://youtube.com/shorts/y4fn_l2IQo4?si=Il2k_3yxbxUZKeOb