Kutoka Mahakamani: Mbunge wa Arusha Godbless Lema apata dhamana

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Ni asubuhi tena kwa mbali jua limeanza kuchomoka huku Arusha ikiwa ni siku ya kupatiwa haki kwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema baada ya kuwekwa kizuizini kwa takribani miezi ninachoamini ni kwamba Mahakama kuu leo itatenda haki kwa Lema.
================
Ulinzi nje eneo la mahakamani umeimarishwa sana
Ulinzi wa nini? Wanadhani kuna mtu atafanya fujo kumnyakua kwa nguvu. Wanashadadia upuuzi wakati wezi mitaani wanatesa!
 
leo hakimu atasikiliza upande wa Lema halafu siku ingine ataita aje asikilize upande wa serikali akimaliza ndio siku ingine aite pande zote asome uamuzi.tulia kama unanyolewa kisongo leo atarudi tena

Akisha rudi Kisonge unakuwa umejenga viwanda vingapi??Toka awamu imeanza mnadeal na wapinzani tu hakuna cha maana zaidi ya chuki visasi na ubaguzi hakuna hata mlichoachieve.

Upumbavu mtupu
 
usishangilie mapema. ujue lema anapigania mdhamana tu ila lema ana kesi kama tatu au zaidi hatimae ataishia lupango. tatizo anapewa mdhamana juu ya mdhamana halafu hana adabu anatukana anadakwa tena.

Amemtukana nani wewe
 
Leo tarehe 03/03/2017 ndio rufaa ya mbunge Lema kusikilizwa kama ana haki ya kupata dhamana na Mahakama Kuu.
Sasa wewe unawahi kuanzisha thread ya mstari mmoja kwa jambo nyeti kama hili na unajua hutaweza kutoa updates unamaanisha nini? Hebu waachie akina Francis12 wanaoweza kutoa live updates Yanayojiri kutoka mahakamani kwenye kusikilizwa rufaa ya dhamana ya Mbunge Godbless Lema. Mods (Mod 1 Mod 2 Mod 3 Mod 4 Mhariri Active Rider Bridger Paw ), mnapounganisha threads kigezo kisiwe nani kawahi ku-post but kuzingatia details na clarity ya thread na kama ni issue inayoendelea uwezo wa mhusika kutoa live updates.
 
Waandishi wa habari wawili tukiwa nje ya eneo la mahakamani tumekamatwa na Jeshi la Polisi .tumeshikiliwa kwa muda lisaa baada ya majadiliano na wahusika tumeachiwa tumezuia kuingia mahakamani.
 
Lowassa ambaye aliitwa Fisadi na Godbless Lema Leo amewasili mahakamani kusikiliza kesi ya Lema. 'Usilipize Ubaya kwa Ubaya''

akiwa katika mavazi yake ambayo Mara nyingi huvaa shati jeupe na Suruali nyeusi Lowassa alionekana Mchangamfu kuliko Baadhi ya Vijana waliomtupa Lema na Kupambanana Jamii Forums bila kumpa sapoti yeyote mahakani.
 
Waandishi wa habari wawili tukiwa nje ya eneo la mahakamani tumekamatwa na Jeshi la Polisi .tumeshikiliwa kwa muda lisaa baada ya majadiliano na RC wa Mkoa wa Arusha tumeachiwa tumezuia kuingia mahakamani.
Daaaahh mmekamatwa kwa sababu gani?
 
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Ni asubuhi tena kwa mbali jua limeanza kuchomoka huku Arusha ikiwa ni siku ya kupatiwa haki kwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema baada ya kuwekwa kizuizini kwa takribani miezi ninachoamini ni kwamba Mahakama kuu leo itatenda haki kwa Lema.
================
Ulinzi nje eneo la mahakamani umeimarishwa sana.
Wananchi wamezuia kuingia mahakama kwenda kusilikiza kesi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema.
Waandishi wa habari wawili tukiwa nje ya eneo la mahakamani tumekamatwa na Jeshi la Polisi .tumeshikiliwa kwa muda lisaa baada ya majadiliano na RC wa Mkoa wa Arusha tumeachiwa tumezuia kuingia mahakamani.
Tupe update kila kinaendelea mkuu
 
Back
Top Bottom