Kutoka January hadi Machi watu 30,000 waachishwa kazi sekta binafsi

Mh Lowassa ndio maana analalamika

Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA na Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa amekosoa utendaji kazi wa Rais wa sasa, Dk. John Magufuli na kusema kwamba unamtia shaka kutokana na utaratibu wa uongozi wake.

“Hali ya siasa nchini hivi sasa ni ya hamasa, lakini isiyo na misingi endelevu kutokana na jinsi Serikali mpya inavyofanya kazi kwa ‘style’ mpya.

“Kwa kipindi kifupi, atakuwa maarufu, lakini hakuna mafanikio ya kiuchumi mbele ya safari. Kwa mfano, rais amekuwa akichukua maamuzi ya kugawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni Bunge.

“Kugawa pesa si kazi ya rais, hiyo ni kazi ya taasisi kama Bunge ambalo lina mamlaka ya kuidhinisha bajeti,” alikosoa Lowassa.

Katika maelezo yake, Lowassa alisema anasikitishwa na hali ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania na pia haridhishwi na idadi kubwa ya watu kuachishwa kazi.

“Ninasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi katika mashirika mbalimbali kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.

“Bandarini sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50 baada ya kampuni nyingi za mizigo kufunga shughuli zake wakati pale kulikuwa na vijana wetu wengi waliokuwa wameajiriwa.

“Hao walioachishwa kazi, hivi sasa wako mitaani, kwa ujumla hali inatisha, maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu,” alisema Lowassa ambaye wakati wa Uchaguzi Mkuu alikuwa akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumzia nchi wahisani, Lowassa alisema kitendo cha nchi hizo wakiongozwa na Marekani kusitisha baadhi ya misaada zikiwamo fedha za Changamoto ya Milenia (MCC), ni pigo kwa uchumi wa Taifa.

“‘Donors’ wamesitisha misaada, lakini sisi tunasema tunataka nchi ya viwanda, hivi fedha tutazitoa wapi kama si kuwategemea hao ‘donors’ wa ndani na nje kutusaidia katika hilo?

“Hawa ‘donors’ si watu wa kuwabeza, ‘they will pull us back’ (wataturudisha nyuma)… Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo ili mfumo huo uwe endelevu,” alisema.
 
Yani kama hapo bandari ukute hizo container za magumashi ndio zilikuwa treated kama fast track...
Waliokuwa wanalipa kodi kwa kuwa hawamjui mtu ndio makontena yao yanachukua miezi...
Sasa si bora waende ili hawa customers wa ukweli wanufaike na upungufu wa foleni za kutoa makontena...na biashra zao zistawi waendelee kulipa kodi zaidi
 
kuna demu alikuwa anafanya kazi kampuni fulani ya clearing and forwading aliniringia sana juzi kanipigia simu kaniomba elfu kumi kwa unyenyekevu wakati alikuwa hapokei simu zangu
Hahahaha viva Magufuli
Heshima yako imerudi :D
 
Hii inawezekana ni kweli, japo inawezekana pia imetiwa chumvi kwa sababu za kisiasa, lakini kutokana na utumbuaji wa majipu na kubana matumizi, biashara nyingi sana zimedorora...kuna watu wanasema hali itaboreka huko mbeleni,ila sijui itachukua muda gani.....
Mpaka tutakapo mpata JK Mwingine
 
Bora kuwa na makampuni machache yanayolipa kodi kuliko mengi lakini kodi hewa...
Ni mpito tu mambo yataeleweka siku za usoni...
Hakuna namna

Mfano kusema makontena yamepungua bandari...wakati mapato ya serikali yanaongezeka ni obvious kuwa wale waliojipunguza ni wakwepa kodi...waende kwa usalama...kama vipi wakajipange upya waje kimtazamo wa kulipa kodi
Nafikiri yatakuwa yameongezeka kutokana na ukusanyaji wa madeni, na sio kutokana na uingizwaji wa bidhaa na uboreshwaji wa biashara.
 
Bora kuwa na makampuni machache yanayolipa kodi kuliko mengi lakini kodi hewa...
Ni mpito tu mambo yataeleweka siku za usoni...
Hakuna namna

Mfano kusema makontena yamepungua bandari...wakati mapato ya serikali yanaongezeka ni obvious kuwa wale waliojipunguza ni wakwepa kodi...waende kwa usalama...kama vipi wakajipange upya waje kimtazamo wa kulipa kodi

Umewahi kujiuliza why almost kila mfanyabiashara anakwepa kodi?
labda kodi ni kubwa kupita kiasi?
umewahi fikiria hili?
je solution ni kuwalazimisha wote walipe kodi au kupunguza kodi?
 
kuna demu alikuwa anafanya kazi kampuni fulani ya clearing and forwading aliniringia sana juzi kanipigia simu kaniomba elfu kumi kwa unyenyekevu wakati alikuwa hapokei simu zangu
da sasa ikawaje ulimpa au..maana huo ndo muda wa kupiga ..mzigo man
 
Amisikia tu hajawa na uhakika ahakikishe kwanza ndo atuletee tena
 
Kama kilimo ni ajira why usiwapeleke hao wanao mpaka usubiri watu wafukuzwe?
Nimekupa Like ya nguvu hahahh. Tuendelee kuwa na wezi wazembe tangu miaka YA 60 tuache vijana kama sio watoto wetu wafanye kilimo na shule wamesoma come on now!
 
Back
Top Bottom