Kutesa Kwa Zamu- Ikulu

siku hizi hao vihiyo wanavuta pesa za RESEARCH wanakula alafu wanakuja jambo forums wanapata taarifa kikulainiiiiiii amabazo zamani walikuwa wanahaha kuzipata ..hapa watu ni vichwa bwana ..alaa..
 
Jamaa amenitumia PM anasema kesho asubuhi sana ataweka vitu vya ajabu hapa, ila ana wasiwasi kama JF haitafungwa; nami nimemhakikishia kuwa JF ni immortal kama alivyokuwa Mzee Punch!

Kitila,

Usije ukaanza zile PM za Mwanakijiji Na mwafrika wa Kike kule kwenye picha za ....

Kweli umetumiwa PM?
 
FD,

Maneno yako ni mazito na machungu lakini ni ya ukweli.

Kitu kimoja natahadharisha though wale wanaofurahia umaarufu wa ccm vijijini ni hili. Hali za maisha ya watu vijijini zinadumaa na hiyo si sign nzuri. Watu wa vijijini wakiendelea kuwa nyuma hivi na kuwa marginalized like this matokeo yake ni mabaya.

Angalia vita vya ndani vilivyotokea kwa majirani zetu Rwanda, Congo, Burundi, Uganda, nk kisha ujibu maswali haya. Hivi hao rebels walianzia mijini au vijijini? Ilikuwaje rahisi kwa rebel leaders kupata wafuasi?

Jibu rahisi ni kuwa, makundi yote hayo yalijengeka vijijini ambapo watu wengi wamekwisha kata tamaa. Kama ccm itaendelea kushinda kwa kutumia nguvu ya watu walioko vijijini at the same time ikitumia mabilioni kujenga majengo ya BoT huku hao wapiga kura wake wakifa kwa njaa na magonjwa yanayotibiwa, basi ccm itabidi ijilaumu yenyewe siku hao wajinga wa vijijini wakichoka na maisha.

hili pia litauma masikioni mwa wengi ila ni ukweli.

Mwafrika wa kike,

Umegusia pazuri. Tanzania yetu watu ni masikini sana na HAWANA SHULE, yaani hawajaenda shule, nchi yetu ni kubwa magazeti hayafiki hata kwenye baadhi ya wilaya!.

Uelewa wa hao wananchi ni MDOGO mno ndugu yangu yaaani ni tofauti kabisa na unavyofikiri.

Kuweka issue vizuri naomba ukibahatika kuja bongo, nitafute tufanye sampling twende kwenye kama wilaya tatu vijijini kabisa ujionee why CCM is there to stay FOREVER!.

Vyama vya upinzani vingeshinda/kuweka kambi vijijini! mjini siku hizi uelewa wetu ni mkubwa saaaana.

Lakini Tatizo ndugu yangu kubali ukatae, VYAMA VYA UPINZANI WANA VIONGOZI WENGI WABABAISHAJI!, natamani niwaweke pamoja niwape shule ya nguvu!
 
Jamaa amenitumia PM anasema kesho asubuhi sana ataweka vitu vya ajabu hapa, ila ana wasiwasi kama JF haitafungwa; nami nimemhakikishia kuwa JF ni immortal kama alivyokuwa Mzee Punch!

huyu jamaa bila kupata tabu huyu ni Hasara alienzisha ile ya picha yeye ni mtu wa kubeep tu kisha anatokomea....angalia sana kuongea kwake nina uhakika ni Hasara huyu
 
JF bwana..kesho asubuhi.... watu mimacho imetutoka....asubhi kwa
saa za wapi GMT? GMT +3, BMT....au za USA??
Haya tunasubiri..
 
Duh, kumbe nami mlikuwa mnanisubiri, haya endeleeni kusubiri! Acheni hizo jamaa, mnapenda umbeya tu kama wazee wacheze bao au wanawake wa saloon!
 
mie nadhani kuan haja ya kuweka term of reference katika kutoka breaking NEWS,mtu hauwezi kuteka akili za watu wa kukata nondo kama Mkapa wakisubiri udaku..
mie nataka Picha zile na hii habari ziwekwe hapa ili mjadala ufungwe
 
Mwafrika wa kike,

Umegusia pazuri. Tanzania yetu watu ni masikini sana na HAWANA SHULE, yaani hawajaenda shule, nchi yetu ni kubwa magazeti hayafiki hata kwenye baadhi ya wilaya!.

Uelewa wa hao wananchi ni MDOGO mno ndugu yangu yaaani ni tofauti kabisa na unavyofikiri.

Kuweka issue vizuri naomba ukibahatika kuja bongo, nitafute tufanye sampling twende kwenye kama wilaya tatu vijijini kabisa ujionee why CCM is there to stay FOREVER!.

Vyama vya upinzani vingeshinda/kuweka kambi vijijini! mjini siku hizi uelewa wetu ni mkubwa saaaana.

Lakini Tatizo ndugu yangu kubali ukatae, VYAMA VYA UPINZANI WANA VIONGOZI WENGI WABABAISHAJI!, natamani niwaweke pamoja niwape shule ya nguvu!

Hapa ndio unakosea kabisaa,

Kati ya wilaya ambazo zilikuwa nyuma kielimu kwa muda mrefu ni wilaya ya watani zangu wakurya na wajaluo - wilaya ya Tarime.

Mpaka kufikia mwaka 1989. Tarime ilikuwa na shule ya sekondari moja tu ( Tarime Sekondari). Passing rate ya wanafunzi ilikuwa chini ya asilimia 5%.

Pamoja na hayo yote, Tarime ilikuwa miongoni mwa wilaya za kwanza Tanzania kuchagua mbunge wa upinzani mwaka 1995 - Mabere Marando.

Katika uchaguzi wa mwaka 2005 - Tarime ilichukuliwa na CHADEMA na sasa hivi halmashauri ya wilaya inaongozwa na CHADEMA.

Na ninakukumbusha wana-ccm kuwa muwe makini sana na Tarime kwa sababu ni wilaya ya mpakani na kuna wakurya na wajaluo wengi sana upande wa Kenya. Kama serikali itaendelea kuuza machimbo ya wakurya kwa wazungu kama ambavyo imefanya sasa hivi huko Tarime,
jiandae kuona the next civil war ikianzia Tarime!

I said it, it is very sad but true.

Haya mambo ya kujifariji kuwa vijijini watu hawajasoma kwa hiyo watachagua ccm forever ni ndoto na kama kweli unaipenda nchi yako inabidi uanze kutekeleza misingi ya maendeleo kabla mambo hayajaharibika
 
hivi hamkuona huruma kuna wakati aliingia na maneno machache "naona nyoka wawili wananusa"
 
bungeni kumewaka moto,suala RICHMOND,
nilishawahi kusema kuna viongozi wengi ni member humu..lowassa kanyanyuka
 
mwenzenu kibarua kimeungua...kahamishwa ofisi... wakati compyuta yake imepelekwa kwa fundi... msiniulize nimejuaje...
 
mwenzenu kibarua kimeungua...kahamishwa ofisi... wakati compyuta yake imepelekwa kwa fundi... msiniulize nimejuaje...

Nimeongea naye kwa simu nami pia sasa hivi, kaniambia hivyohivyo, analia ile mbaya. Labda mtu aanzishe michango hapa ya kuokoa familia yake!
 
Unajua hawa wazee inabidi tuwasaidie kidogo kwenye mambo ya kompyuta haya. Mzee alitapika mengi kwenye posti ya kwanza na ikawa kama mtu anajicha uso sokoni!!
 
Back
Top Bottom