Kutajwa kwa Mbowe: Kisa ni Billicanas inayomilikiwa na Mbowe Hotels

S

Sasa kama mmiliki hujuim kinachoendelea ndani ya kitu chako then Sijui tukuiteje! Yaani unaown kitu halafu uhalifu unafanyika kwenye Kitu chako then wewe huhusiki kabisa. So hakuna siasa hapo na kama alivyosema Maknda wengine wanakamatwa kuisaidia polisi kama huhusiki povu la nini?!?!?!?
Ukipangisha nyumba siyo lazima ujue mpangaji ana vitanda vingapi na nani analala chumba gani. Hivi ukiwa na guest house lazima ujue nani kalala nani?
 
fe687bd2e091811772a5a9d429230680.jpg


MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Viongozi wa Dini, Askofu Wiliam Mwamalanga, amesema amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja Freeman Mbowe kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Askofu Mwamalanga alisema kamati yao ilitilia shaka Bilicanas iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya Mbowe Hotels, kwamba ni moja ya maeneo yanayotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kufanya biashara zao, lakini si mwanasiasa huyo.

Alisema ukumbi huo wa starehe kuhusishwa na biashara hiyo, haikumaanisha kwamba mmiliki wake ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anahusika.

“Sisi tulisema klabu ya Bilinacas inajihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya kwa sababu walikuwa wanaingia watu mbalimbali ambao walikuwa wakiendesha shughuli hizo, lakini hatukumtaja mmiliki wake Mbowe ndiye anayejihusisha na dawa hizo,” alisema Askofu Mwamalanga.

Alisema kamati hiyo itashirikiana na Serikali ili kuhakikisha biashara ya dawa za kulevya inatokomezwa na wahusika wote wanafikishwa kwenye mikono ya sheria.

Kamati hiyo pia imempongeza Rais Dk. John Magufuli kumteua Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya mwenye taaluma ya kusimamia suala hilo, jambo ambalo limesaidia kutotajwa watuhumiwa hadharani badala yake wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

Chanzo: Mtanzania
 
Ukipangisha nyumba siyo lazima ujue mpangaji ana vitanda vingapi na nani analala chumba gani. Hivi ukiwa na guest house lazima ujue nani kalala nani?
Of course if your irresponsible hutajua!
 
Kama serikali inatambua kuwa Bilicanas iligeuzwa kitovu cha wauza unga ilishindwaje kuwakamata hhao wauza unga halafu leo ilete majungu?

Mkuu jitahidi basi kuuliza maswali kwa kutumia akili zako,Muda wa Unanjua mm nani ushaisha hiki ni kipindi cha hapa kazi tu......na bila nguvu kazi ya Taifa hakuna kutimiza hii kauli.
 
Kitu cha pekee cha kumsafisha, awe serious na hiyo kesi....ajisafishe

asipokuwa serious....analo
Hawezi kuanza kujisafisha mpaka ahojiwe,ameshatumiwa barua rasmi ya wito na huyo nayo aikatae.Kiongozi gani muoga wa polisi huyo bure kabisa
 
waliitwa wamiliki wa casino nyingi tu

mbowe angeenda na kusafisha hali ya hewa

kujifanya kugoma, kuna watu wanazua maswali mtaani...

Nyie si mna serikali mkamateni basi hata kwa nguvu au bado mnamuogopa? Huyo ndio Freeman Aikaeli Mbowe
 
Mkuu jitahidi basi kuuliza maswali kwa kutumia akili zako,Muda wa Unanjua mm nani ushaisha hiki ni kipindi cha hapa kazi tu......na bila nguvu kazi ya Taifa hakuna kutimiza hii kauli.
Hivi hata darasa la saba umefika kweli?
 
Imefahamika kuwa Mbowe alitajwa kuhusika na madawa ya kulevya kwa vile ni mmiliki wa Mbowe Hotels inayoendesha ukumbi maarufu wa Billicanas.

Inasemekana ukumbi wa Billicanas ambao huwa unatumiwa na wanamziki wengi mastar na wafanyabiashara wakubwa kilikuwa kama kituo kinachotumiwa na wauza unga kukutana.

Wadadisi wa mambo wanasema Mbowe amehusishwa kwa sababu za kisiasa tu, mhusika ambaye angetakiwa kuitwa ni meneja wa hotel au meneja wa ukumbi na siyo Mbowe binafsi ambaye hata baadhi ya watumishi wa hotel hiyo waliochini ya mameneja hawajui na wageni wanaoingia pale hawajui.

Nawasilisha.
Sasa rafiki Meneja kazi yake ni kuhakikisha wanapata faida sasa kama walijua hilo ilikuwa kazi ya Tiss kwenda na kufanya kazi yao.Na kama walikuwa ndiyo station yao basi ilikuwa rahisi kuwapata
 
Acha maneno leta.....no fact. Cha msingi aende akapimwe damu hizo longo longo nyingine mtatujazia tuu kurasa bure , nasikia ile kitu ukitumia hata uki flash na dawa gani kipimo lazima kionyeshe. Ifike wakati sasa tuheshimiane sio kujificha kwenye vivuli vya taasisi mbalimbali halafu unapoitwa kwenye sheria unakwepa kwepa.
 
Kuitwa kupitia chombo cha habari si utaratibu unaokubalika kisheria.

Hata Makonda alisema hatahudhuria mwito wa kamati ya bunge kwa kuwa alikuwa hajaalikwa kwa maandishi.
uko sahihi..ishakuwa
 
Na hao wengine waliotajwa wanamiliki nini? Hivi kwanini watu wanamtetea Mbowe kabla hata hajatoa maelezo polisi?
 
Hawezi kuanza kujisafisha mpaka ahojiwe,ameshatumiwa barua rasmi ya wito na huyo nayo aikatae.Kiongozi gani muoga wa polisi huyo bure kabisa
Kuna kesi iko mahakamani ikihoji uhalali wa RC kuita mtu aende polisi badala ya ofisi ya mkuu wa mkoa.

Kazi ya kuita mtu polisi ni ya polisi wenyewe tena kwa RB, Makonda alikuwa na RB ya polisi?
 
Back
Top Bottom