Kura za maoni CCM Arumeru kurudiwa

Kaka si ulisema huyu jamaa alikuwa anajiandaa kuingia Chadema na ukatuwekea na picha juzi kati akiwa na kamanda Lema?? sasa itakuwaje hapa na anatakiwa apigiwe kura tena na chama chake??

Mkuu Mwana Mpotevu.
Huyu jamaa kweli ni muongo sana anatakiwa kutuomba radhi members wote wa JF.

Lakini kwa tabia za waongo navyozijua hawezi kukosa sababu anaweza kukwambia Lema, alimkataza.
 
Mtanzania, ni kweli kutokana na Katiba ya CCM hiyo kanuni ya asilimia 50 ipo.

Ambacho unakosea na hukisemi kwa wazi ni kuwa hiyo kanuni iliwekwa kando kabla ya 2010. Hiyo kanuni iliwekwa kando na Mkapa akiwa Mwenyekiti kabla ya Uchaguzi Mkuu wa CCM wa 2005 uliompitisha Kikwete kuwa mgombea. Kikwete alipowashinda akina Mwandosya na Salim hakupata zaidi ya asilimia 50, na sikumbuki kama uchaguzi ulirudiwa.

Hiyo kanuni haijawahi kutumika tena toka 1995 wakati Mwalimu alipoitumia kama njia ya kumuengua Msuya, ili Kikwete apambane na Mkapa. Si kweli kuwa ilibadilishwa kwa ajili ya 2010 tu.

Kanuni za Chaguzi za CCM zinakinzana na Katiba ya CCM kuhusu ugombeaji, na hii ni mojawapo tu.

Hiyo kanuni haikutumika Igunga wala Uzini.

Msimamizi haundi kanuni wala haamui kanuni ipi atumie na ipi aiteme. Kama ilivyo sawa, msimamizi husimamia kanuni zote zinazoongoza uchaguzi kwa wagombea wote waliopitishwa na chama, kutokana na kanuni zilizopitishwa na Kamati Kuu, KABLA ya Uchaguzi.

Haiwezekani wagombea wote wasiwe sahihi (hakuna mgombea aliyepinga kuhusu Sioi kupitishwa kwa chini ya asilimia 50), msimamizi Arumeru asiwe sahihi, halafu Kamati Ya Siasa ya Wilaya pia isiwe sahihi, halafu Kamati Ya Siasa ya Mkoa isiwe sahihi, na kama muujiza Kamati Kuu pekee ndiyo ione kosa hilo katika kanuni.

Talk about shifting the goalposts AFTER taking the penaly kick.

Ushauri wangu kwa Sioi Sumari ........ ikifika hiyo March 1 JIENGUE na uepukane na karaha na mizengwe ya akina Wassira na Chitanda. (Katika hili JK hana bifu ila anapelekwa tu kama bodaboda.....what's new!!! Kwake nadhani yoyote ni sawa).

Kiungani,
Kikwete alishinda round ya kwanza yaani alipata zaidi ya asilimia 50 round ya kwanza ndio maana hakukuwa na haja ya uchaguzi kwenda round ya pili. JK alipata kura 1,072 kati ya kura 1800. Salim 476 na Mwandosya 122.

Igunga hivyo hivyo Dr. Kafumu alipata kura zaidi ya asilimia 50 kwenye round ya kwanza. Hata Uzini, Raza alishinda mara ya kwanza. Dk Peter Kafumu alishinda kwa 588 kati ya wajumbe 950 waliopiga kura kwa Igunga.

Hizo chaguzi zote tatu nina uhakika kwa asilimia 100. Fuatilia matokeo yake hata hapa JF.

Huu utaratibu ulibadilishwa kwa waraka wa uchaguzi mwaka 2010 ili kuondoa gharama za kurudia uchaguzi kwa wanachama wote.

Hilo la kwamba hakuna aliyelalamika inawezekana sio sahihi. Ukiona CC ya NEC wameingilia kati most likely Sarakikya alilamika. Baada ya uchaguzi malalamiko yanapelekwa kwenye vikao vya chama na kujadiliwa na kamati zote ila maamuzi hayatolewi mpaka NEC. Kikawaida huwezi kujua malalamiko ya wagombea unless wewe ni mjumbe pia.
 
Siku chache baada ya Wiliam Sarakikya kutaka kuhamia Chadema huku aliekuwa mshindi wa tano (Msani) akihamia chadema chama cha Mapinduzi wamekubaliana na matakwa ya Wiliam Sarakikya kuwa uchauguzi huo urudiwe, kamati kuu ya ccm (CC) kupitia msemaji wake Nape Nauye amesema uchaguzi huo utarudiwa tarehe 1-3-2012, huku akiwataja watakao chuana kuwa ni Wiliam Sarakikya na Sioi Sumari alie tumia zaidi ya mil 100 kwenye uchaguzi uliopita.

milioni mia kwa kazi gani ukizingatia ni kura za maoni
 
CCM wakitaka kukumwaga, wanazusha sababu zisizo na kichwa, kiwiliwili wala miguu. Kwamba Sioi ana utata na uraia wake - hawakuliona hilo kabla hajachukua form? Mwaka 2010 kuna watu walizidiwa kwa kura tatu tu na wala uteuzi haukurudiwa!
 
Hapana......Hapa tunazungumzia utaratibu......Kila chama si kina taratibu mkuu?,achana na suala la past ama present issues...Swala ni je,utaratibu uliotumika kuwapata wagombea Urais na wale wa viti maalum ulikuwa ni sahii?,upo kwenye katiba ya CHADEMA?......

Halafu......Achana na suala Rushwa ndani ya CCM....Nilichotaka mimi unieleze ni kwa nini Nassari anaendesha harambee ya kuchangisa fedha za kumsaidia katika uchaguzi ilhali bado hajapitishwa na chama kama mgombea Ubunge wa CHADEMA?.......Isije suala hili likaja kuleta matatizo mbeleni(endapo Nassari atachaguliwa) na kuleta mgogoro miongoni mwa walioomba kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA....Hili ni angalizo tu
Siwezi kuongelea uteuzi wa viti maalumu 2010 sasa jambo ambalo tumelijadili sana humu zaidi nitakachofanya ni kukuunganisha na thread yenyewe.

Kuhusu issue ya Nassari kuchangiwa pesa sidhani kama kuna tatizo kwa taratibu za Chadema hata katibu CDM wa wilaya Arumeru amesema hakuna tatizo kama mtu anachangiwa na rafiki zake, kama kungekuwa na vitendo vya rushwa vingeripotiwa lakini hadi sasa hakuna aliyeripori zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.
 
Kwa ufafanuzi sahihi ni kwamba kilichofanyika leo na CC ya NEC ya CCM ni kupanua demokrasia ya maamuzi kwa kurejesha majina mawili ya mshindi wa kwanza katika kura za maoni na mshindi wa pili ili sasa Mkutano Mkuu wa jimbo upigie kura majina hayo mawili na baadae kutoa fursa kwa vikao vya juu yaani Kamati za siasa za wilaya na mkoa na baadae CC kujadili na kumpitisha mmoja wapo. Sioni mkanganyiko tena. kwani katika hesabu za kawaida kati ya hao wawili, lazima mmoja apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote au wagongane au wafungane kwa kupata asilimia hamsini kila mmoja. huo ndiyo uzuri wa demokrasia. lazima ifuate ili kumpata mtu anayekubalika zaidi kuwakilisha chama chetu.
Wale ambao hawana hoja, na badala yake wanataka kupinga kila kitu, sasa niwakati wa kuaibika.
 
Wakuu,

Hapa huyu mheshimiwa Mwigulu amechemsha sana. Ni aibu kwa chama kikongwe kama CCM wanashindwa kuielewa na kuifuata katiba yao.

Kama ni kweli kwamba Nape alitetea kwenye TV kwamba sio lazima kufikisha asilimia hamsini, naye hapo anachemsha. Imekuwaje chama kikongwe hivyo kikafika mahali ambapo viongozi wake wakuu wanashindwa hata kuielewa katiba yao?

Najua ile kura ya maoni ya mwaka 2010 imewachanganya lakini ni kosa kubwa watu wote hao kuchanganyikiwa na kushindwa kuuona ukweli mpaka CC ndio inakuja kuwaambia kwamba mmekosea?

Sasa kama secretariat ya CCM hawaijui katiba yao, vipi wale wenzetu kule wilayani? Vyama vimeingiza Wababaishaji ambao wanafikiri wanaweza kufanya mambo bila kusoma na matokeo yake ndio hayo.

Mambo mengine yanasikitisha sana!

Usisahau kuwa huu ndiyo uchaguzi pekee mdogo au kura za maoni za jimbo ambao utasimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM - Taifa. Ni historia katika utendaji kazi wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya CCM tangu kuanzishwa kwa TANU/CCM. Akishindwa Msekwa anaenda JK mwenyewe kusimamia kura za maoni ya CCM ya jimbo moja la uchaguzi.

Kazi ipo.
 
Kwa ufafanuzi sahihi ni kwamba kilichofanyika leo na CC ya NEC ya CCM ni kupanua demokrasia ya maamuzi kwa kurejesha majina mawili ya mshindi wa kwanza katika kura za maoni na mshindi wa pili ili sasa Mkutano Mkuu wa jimbo upigie kura majina hayo mawili na baadae kutoa fursa kwa vikao vya juu yaani Kamati za siasa za wilaya na mkoa na baadae CC kujadili na kumpitisha mmoja wapo. Sioni mkanganyiko tena. kwani katika hesabu za kawaida kati ya hao wawili, lazima mmoja apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote au wagongane au wafungane kwa kupata asilimia hamsini kila mmoja. huo ndiyo uzuri wa demokrasia. lazima ifuate ili kumpata mtu anayekubalika zaidi kuwakilisha chama chetu.
Wale ambao hawana hoja, na badala yake wanataka kupinga kila kitu, sasa niwakati wa kuaibika.

Huyu ndiye anaewasumbuwa hakuna kingine wanafki wakubwa nyinyi CCM!!

1.JPG
 
Siwezi kuongelea uteuzi wa viti maalumu 2010 sasa jambo ambalo tumelijadili sana humu zaidi nitakachofanya ni kukuunganisha na thread yenyewe.

Kuhusu issue ya Nassari kuchangiwa pesa sidhani kama kuna tatizo kwa taratibu za Chadema hata katibu CDM wa wilaya Arumeru amesema hakuna tatizo kama mtu anachangiwa na rafiki zake, kama kungekuwa na vitendo vya rushwa vingeripotiwa lakini hadi sasa hakuna aliyeripori zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.
Na mgombea Urais je?.....

Haya bana......Najua umefunika kombe ili Mwanaharamu apite...

Btw.....Mshaurini Nassari awe makini.....
 
Na mgombea Urais je?.....

Haya bana......Najua umefunika kombe ili Mwanaharamu apite...

Btw.....Mshaurini Nassari awe makini.....
Bala hapa wa kumshauri ni JK na CCM yake, kimvuli cha Lowasa kitamuandama kila aendapo, hakuna utaratibu wa asilimia kwenye kura za maoni za CCM, Utaratibu ni kwamba alieshinda kashinda, kama wameamuwa kumchinjia dogo baharini wangekata tu jina lake na kusema haya ndio maamuzi ya kamati kuu full stop. Mbona Nape tuliambiwa amefungiwa duniani mpaka mbinguni!!
 
Na mgombea Urais je?.....

Haya bana......Najua umefunika kombe ili Mwanaharamu apite...

Btw.....Mshaurini Nassari awe makini.....
Katiba inasema hivi:-
7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika mkutano mkuu kwa uamuzi.
 
Kaka si ulisema huyu jamaa alikuwa anajiandaa kuingia Chadema na ukatuwekea na picha juzi kati akiwa na kamanda Lema?? sasa itakuwaje hapa na anatakiwa apigiwe kura tena na chama chake??
Cant you see the impact of the message (picture) nani alitegemea uchaguzi kurudiwa.
 
Kwa ufafanuzi sahihi ni kwamba kilichofanyika leo na CC ya NEC ya CCM ni kupanua demokrasia ya maamuzi kwa kurejesha majina mawili ya mshindi wa kwanza katika kura za maoni na mshindi wa pili ili sasa Mkutano Mkuu wa jimbo upigie kura majina hayo mawili na baadae kutoa fursa kwa vikao vya juu yaani Kamati za siasa za wilaya na mkoa na baadae CC kujadili na kumpitisha mmoja wapo. Sioni mkanganyiko tena. kwani katika hesabu za kawaida kati ya hao wawili, lazima mmoja apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote au wagongane au wafungane kwa kupata asilimia hamsini kila mmoja. huo ndiyo uzuri wa demokrasia. lazima ifuate ili kumpata mtu anayekubalika zaidi kuwakilisha chama chetu.
Wale ambao hawana hoja, na badala yake wanataka kupinga kila kitu, sasa niwakati wa kuaibika.
Nchemba...

Suala hapa si kutokuwa na hoja......Suala hapa ni kwa nini utaratibu huu hamkuutangaza toka awali kiasi cha kutangaza kwamba Sioi Sumari ndio mshindi na kinachosubiriwa ni kupitishwa kwa jina la nani atagombea kwa tiketi ya CCM na ngazi za juu za CCM(vikao)...

Mlipaswa kueleza mapema ni utaratibu gani ungetumika(kama ni ule wa kwa mujibu wa katiba ya CCM-wa 50% ama ni ule uliotumika mwaka 2010)...Hali hii inaweza kupelekea mkanganyiko/migongano miongoni mwa wanachama na hivyo kusababisha chama kushindwa katika uchaguzi......
 
Siwezi kuongelea uteuzi wa viti maalumu 2010 sasa jambo ambalo tumelijadili sana humu zaidi nitakachofanya ni kukuunganisha na thread yenyewe.

Kuhusu issue ya Nassari kuchangiwa pesa sidhani kama kuna tatizo kwa taratibu za Chadema hata katibu CDM wa wilaya Arumeru amesema hakuna tatizo kama mtu anachangiwa na rafiki zake, kama kungekuwa na vitendo vya rushwa vingeripotiwa lakini hadi sasa hakuna aliyeripori zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.

Kuchangiwa Sh10 milioni na magari manane kwa ajili ya kura za maoni? Hahaahaaa!haaaa! Chadema bana..

Halafu unajifanya kuwashikia akili watu wa Arumeru na wagombea wengine eti hakuna aliyeripoti, ebu nenda kawahoji wagombea wa Chadema waliochukuwa fomu Arumeru wanasema sio kuwasemea.
 
Katiba inasema hivi:-
7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika mkutano mkuu kwa uamuzi.
Ina maana hakuna fursa kwa wanachama wenye sifa kujitokeza kugombea na majina yao kujdailiwa na vikao vya juu vya chama?.....

Naomba(kama hutojali) kunielewesha hapa mkuu.....
 
Kwa ufafanuzi sahihi ni kwamba kilichofanyika leo na CC ya NEC ya CCM ni kupanua demokrasia ya maamuzi kwa kurejesha majina mawili ya mshindi wa kwanza katika kura za maoni na mshindi wa pili ili sasa Mkutano Mkuu wa jimbo upigie kura majina hayo mawili na baadae kutoa fursa kwa vikao vya juu yaani Kamati za siasa za wilaya na mkoa na baadae CC kujadili na kumpitisha mmoja wapo. Sioni mkanganyiko tena. kwani katika hesabu za kawaida kati ya hao wawili, lazima mmoja apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote au wagongane au wafungane kwa kupata asilimia hamsini kila mmoja. huo ndiyo uzuri wa demokrasia. lazima ifuate ili kumpata mtu anayekubalika zaidi kuwakilisha chama chetu.
Wale ambao hawana hoja, na badala yake wanataka kupinga kila kitu, sasa niwakati wa kuaibika.
Mkuu Mwigulu,

Asante kwa kuja hapa na kutoa ufafanuzi. Lakini wewe kama msimamizi wa uchaguzi ilitakiwa hili kulijua toka mapema na kuliweka wazi. kwamba uchaguzi haukuisha kwani hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50 kama katiba inavyosema.

Hapa ungelikuwa muungwana tu na kusema ulifanya makosa na bahati nzuri kamati kuu imegundua na kuyarekebisha makosa hayo. Kuanza kutumia njia nyingine yoyote kuelezea hili kosa binafsi nitasema ni ubabaishaji. Kila mtu anakosea, lakini ni vizuri kukiri kosa na kusonga mbele.

Hayo makosa madogo madogo inatakiwa vijana tena na elimu zenu nzuri tu msiyafanye. CCM imakuwa ikidhalilishwa sana kwa watendaji kutokufuata taratibu. Ifike mahali mjirekebishe na nyie kama vijana muwe wa kwanza kujifunza na kufanya mabadiliko.

Unajua ningelikuwa mimi ningesema tu, "Sorry guys, I screwed up!" lakini bahati wazee kule CC wamerekebisha.
 
Back
Top Bottom