Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
my self cna chuki na zitto bt kuwa rais hapana coz hana mshikamano na wenzake nasikiri endapo ataingia madarakani itakuwa na serikali isiyokuwa na cooparation na pili anaamini mawazo yake always ni sahihi bt kuwa waziri mkuu anafaa
 
Hata Slaa ana uchu wa madaraka, Una ushahidi kuwa Zito anatumiwa na CCM?

Ujana wake nayo ni sifa? kwani ukiwa mzee huwezi kuwa rais?
sababu za kuto mchagua Zitto Kabwe
1. hana sifa ya kugombea urais coz hajatimiza umri unaotakiwa na sheria
2. hana sifa ya kugombea coz ana uchu wa madaraka
3. hana sifa ya kugombea urais coz hana Busara na hekima
4. hana sifa ya kugombea coz anatumiwa na ccm
 
Pengine watamchague Zitto eti kwa sababu ni Muislamu. Lakini kwa nchi inayotaka mabadiliko ya dhati huwezi mpatia Zitto Urais akamkataa Dr Slaa. Urais wa nchi unaangaliwa vigezo vingi sana. Mtu aliyekuwa Mwanajeshi, au Polisi ukimpa Urais bila kumpatia mafunzo ya utawala mnajua athari zake na mumeziona. Mtu aliyekuwa Shehe wa Msikiti au Mchungaji mnajua majukumu yake awapo Msikitini au Kanisani. Mtu aliyekuwa Mwalimu ukimpa majukumu ya Taifa mnajua faida zake. Mtu kama Zitto Kabwe nitampa nafasi ya mtu kama Mnauye lakini madaraka ya Urais atalewa madaraka. Dr Slaa sio wa kumjaribu kila mtu anajua. Hapo ni sawa na yule Bwana aliyemfananisha na Lion Messi. Tukubali tukatae Watanzania hata JK alimkimbia kwenye mdahalo. Tukiachilia mbali mambo ya udini watu wawili tu sasa hivi wanatufaa nchi hii kuwa Marais na ni Lipumba na Dr Slaa. Sasa kwa vile swali lilimuelekea Dr Slaa basi amepewe kura za "NDIO"
 
Dr. Slaa anastahili kupewa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu zifuatazo:

1. Si mtu wa kuzusha maneno na ni mtu makini sana kwa kauli zake. Mfano mwaka 2010 aliweza kubaini kontena lililokuwa likiingizwa nchini likiwa na kura zilizochakachuliwa. Kura hizo zilikamatwa na zimehifadhiwa chadema makao makuu!

2. Juzi juzi Dr. Slaa alitoa taarifa kuwa mtoto wa rais Kikwete, Ridhiwan amekamatwa Uchina akiwa na dawa za kulevya na kwamba Kikwete alikwenda kumwokoa. Ratiba ya rais siku hizo ilionesha rais alikuwa ziara nchi kadhaa za africa including rwanda. Pamoja na hayo inawezekana J.K alipaa usiku kwa ungo akafika uchina kumwokoa r1. Dr. Slaa ni makini na hawezi danganya!.

3. Slaa ana uwezo mzuri wa kutunza familia na ni mtu asiyependa wake za watu. Ana mke mmoja tu first lady Josephine!.

4. Lengo la Dr. Kutangaza kuwa nchi haitatawalika lilikuwa zuri tu. Alilenga kuonesha umuhimu wa kulazimisha ushindi wake. Ni kauli nzuri inayopaswa kutolewa na mtu yeyote makini kama Slaa. Nchi isipotawalika ingesaidia yeye kuingia ikulu kiulaini. Na baada ya kuingia ikulu ghafla nchi ingeanza kutawalika. Dr. ana mbinu bwana.

5.Dr. Slaa ni mpenda demokrasia kwani alionesha mwanzo mzuri wa maandamano. Tumchague 2015 kwani itakuwa free kuandamana wakati wowote bila kibali cha polisi. Haki zote za watumishi zitapatikana kupitia maandamano, rais si ndo huyu jamani!

6. Dr. Slaa atatufaa watanzania kwani hataruhusu matumizi ya sheria. Kila mtu atafanya alitakalo na polisi watakuwa wakila bata tu. Ameonesha mfano mzuri wakati wa mikutano yake ambapo amekuwa akipinga sana polisi kukamata wavunja sheria.

7. Kikubwa ninachomfurahia Dr. Slaa ni kuwa akiwa Rais watanzania mtasahau shida zooooote. Hakutakuwa na rushwa hata moja, walimu mtalipwa kadri mtakavyo, wahitimu wa vyuo na shule wote mtaajiriwa, hakutakuwa na ufisadi, watu wote hatutalipa kodi, n.k.

Sifa zingine uzijuazo................................

Kwa haya, kwanini Dr. wa ukweli asiwe rais wetu 2015?
 
1. Nikiangalia Namna huyu Mzee alipoitaja Ile List of Shame Mwembe Yanga 2009 na Jinsi wale wezi walivyotishia kumpeleka Mahakamani bila Mafanikio ( Of Course That Day Haita Sahaulika kirahisi na wana CCM)

2. Nikiangali namna huyu Mzee alivyoipa Taabu CCM kuanzia alipokuwa Mbunge Mpaka alipoombwa na Chama Chake Kugombea Urais 2010

3. Nikiangalia Uchaguzi wa Juzi ambapo Wagombea wa CCM walioshinda kwa Kishindo ni wale walioahidi Kupambana na Dr. Slaa ikiwezekana wampoteze (Mfano Wasira)

4. Nikiangalia namna huyu Mzee alivyoichanachana Sekretariati Mpya CCM (Meghji - EPA, Kinana (Pembe za Ndovu), Mangula (EPA) Mpaka Sekretariati imekuwa si chochote si lolote Machoni pa wananchi

5. Nikiangalia Hadidu za Rejea iliyokabishiwa Timu ya CCM Online Hoes ( Majembe ya CCM Online) Ritz , chama , W. J. Malecela na Ukweli ukizingatia Hadidu rejea namba Moja ni Dr. Slaa, Namba Mbili ni Dr. Slaa namba tatu ni Dr. Slaa

6. Nikiangalia watu wanavyojaribu kuonesha kwamba Dr. Slaa hafai kugombea Urais kwa Sababu "AMEGOMBEA MARA NYINGI NA KUSHINDWA MARA NYINGI"

Kutokana na hayo machache (Wengine wanaweza Kuongezea) Ninaweza kabisa (Bila Shaka ) Kusema Kwamba

1. Dr. Slaa (Na viongozi wengine wa aina yake ambao wameshachora Mstari Kati yao na CCM) ni Tishio Kubwa kwa Uhai wa CCM and there fore CCM haitawaacha na Haitapenda Kabisa waendelee kuwepo katika Uwanja wa Siasa so ni Jukumu letu wapenda Mabadiliko kuwaombea dhidi ya Usetwani wa TISS

2. Dr. Slaa sasa amekuwa ni TURUFU ya Uongozi ndani ya CCM na yeyote aliyefanikiwa Kumtukana ameukwaa Uongozi ndani ya CCM

3. CDM ina hitaji Mrithi wa Katibu Mkuu mwenye Msimamo na Jasiri Kama Dr. Slaa. Ambaye Atachora Mstari kati ya Dhuluma na Haki,

Long Live Dr. Slaa, Long Live CHADEMA
 
Last edited by a moderator:
la hasha sina maana hiyo mm akisimama mkristo yyte yule mwenye sifa za kua rais kwangu ni sawa tu alimradi asiwe slaa na asiwe na sina imaaani naye kozi sijawahi sikia PADRE kaacha upadre nahisi kuna kaaajenda hapa kanaandaliwa siko tayari kua sehemu ya ajenda hiyo

Huyo ambaye ungemsikia NDIYE HUYU usiyetaka kumsikia!
 
Frankly speaking sijaona kitu kwa zitto kinachoweza kunishawisha kwamba hata ana mkaribia slaa, mara nyingi anataka sifa binafsi na wakati mwingine ananichanga na ties zake na baadhi ya viongozi wa serikali {ccm} nafikiri kama tuko serious dr slaa is the choice
 
CHADEMA lazima muelewe mitego ya kuwasambaratisha. Hii mada imetengenezwa toka mtaa wa Lumumba. Haina maana hata kidogo kwa wana Chadema. Tumia busara kutoichangia. Waachie wenyewe wana Lumuba waichangie. Ninyi idharau kabisa. Ona mpaka wanapenyeza suala la udini. katika Tanzania ya leo hii ni kitu gani. Hawa wana lengo lao wapuuzieni. Wanazidi kuichafua nchi yetu kwa kupandikiza siasa za ubaguzi kwa maslahi yao.
 
CHADEMA lazima muelewe mitego ya kuwasambaratisha. Hii mada imetengenezwa toka mtaa wa Lumumba. Haina maana hata kidogo kwa wana Chadema. Tumia busara kutoichangia. Waachie wenyewe wana Lumuba waichangie. Ninyi idharau kabisa. Ona mpaka wanapenyeza suala la udini. katika Tanzania ya leo hii ni kitu gani. Hawa wana lengo lao wapuuzieni. Wanazidi kuichafua nchi yetu kwa kupandikiza siasa za ubaguzi kwa maslahi yao.
 
Dr. P.W. Slaa na Mr. Zito Z. Kabwe ni wanasiasa mashuhuri hapa nchini.

Pamoja na kuwa Zito ana kasoro zake nyingi tu, bado ni kijana anayeuzika sana kwenye siasa za Tanzania. Ameshajijenga vizuri sana. Kuna siku alimbeza mwenzake Tundu Lissu bungeni, nikaona kuwa huyu jamaa kumbe kweli anatakiwa aekue kidogo. Sometimes busara zinaongezeka kulingana na muda.

Kama Zito kabwe atampisha Dr. W.P. Slaa agombee uraisi uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfanyia kampeni ya dhati, CHADEMA itafanya vizuri sana kwenye uchaguzi. Lakini kukiwa na kutofautiana kati ya Zito na Slaa, basi CHADEMA inaweza ikakosa mafanikio kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Matokeo ya mwaka 2015 yatachangia sana matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Napendekeza, Dr. Slaa aachiwe agombee mwaka 2015 na baada ya hapo akiwa raisi aongoze kwa miaka mitano tu, amuachie Zito, akikosa astaafu siasa, ataheshimika sana kisiasa hapa Tanzania kuliko wale ambao wanasema wamestaafu alafu baada ya muda mfupi wanarudi. Zito pia anatakiwa amrudishe David Kafulila CHADEMA ili washirikiane kuhakikisha Kigoma inakuwa ngome muhimu ya CHADEMA.
 
Nahavache huo ni ushauri mzuri.

Tatizo ni kusikia na kuchukua ushauri wa Wanachama

Muda huu ni wakati wa kujenga mtandao wa chama na kufika vijijini. Bila chama kujengwa kwa M4C kwa ushirikiano kwa wote, 2015 Chadema haitashinda. Sasa kama mmoja wapo atajitenga na kuanza kuutaka Uraisi kwa nguvu, ujue ana lake jambo.
 
Slaa ni kibabu,hatuhitaji ongozwa na vibabu.
Kweli kabisa Mkuu, tunatakiwa tuongozwe na vijana kama Kikwete, Membe, Wassira, Msekwa, Warioba, Kinana,Mangula, Malecela, Mkapa, Butiku, Makinda, Samweli Sitta, Lowassa n.k, bonge la point Mkuu na CCM wanaye mtetezi hapa JF
 
hizi ni tafiti za kisanii na jamii forum ijiweke kando nazo. DAIMA NI GAZETI LA MBOWE, ALIYEANDIKA WANASEMA NI KAMPENI ZA KURUDISHA HESHIMA BAADA YA CHADEMA KUTIKISWA NA VUMBI LA KINANA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom