Kupitia Kipindi cha Chemsha Bongo Radio One nimejifunza kitu

Jana nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha Radio One Chemsha Bongo kuna kitu nimejifunza,kuna maswali ya kawaida tu Yaufahamu zaidi ila wengi waliopiga Simu walikua wakishindwa kuyajibu.

Mfano Jina la Mwanasiasa mkongwe Tanzania kuna mdau alijibu bado halijatokea Tanzania

Malala Ametokea nchi gani huyu dada alitajwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na mateso aliyopitia

Kabla ya Mark Sally Rais wa Senegal aliyepita aliitwa nani,Maswali yote watu walishindwa kuyajibu hadi kufikia Mtangazaji kutoa Majibu.

Taja nchi 3 zinazoanzia na herufi T Afrika Mtu anasema ni Tanzania tu.

Nikajiuliza Je ni Mitaala yetu ya Elimu haiwaruhusu watu kuyajua hayo au?Kipindi cha Nyuma kulikua na Vitabu vizuri sana ya Kiada na Ziada Shule mwetu.

Nakumbuka Jiografia Nimeanza kusoma kuanzia kilimo Cha Buni BUKOBA,Buni BURUNDI Mpaka Buni BRAZIL.

Kilimo cha Ndizi Bukoba,Ndizi visiwa bya Kanali mpaka Ndizi Jamaika.

Jiografia ilikua pana sana kwa leo hii sidhani kama mwanafunzi ukimuuliza kwa Tanzania wapi wanalima Mahindi zaidi atakujibu,Afrika na hata pia Duniani.

Kuna kipindi kulikua na Mashindano ya vyuo Vikuu yalikua yakirushwa Mubashara wenzetu walikua Shapu sana kujibu maswali manake kulikua na Vipengele vya michezo,masomo,historia mbalimbali ila sisi tulikua tunashindwa kuyajibu

Nimeshawahi Kuweka bandiko moja hapa jibu la kwanza watu walinijibu tukishajua itatusaidia nini?niwapongeze walimu wa zamani sana naimani hata sasa bado wapo akikufundisha Jiografia utadhani upo kwenye nchi husika kabisa.

Nliwahi kuwa na Rafiki Mjapan akashangaa nataja timu za kwao za Mpira kama vile Gamba Osaka akashangaa sana ni Sawa leo Umuulize mtu OTELULU GALAT ni timu ya mpira inayotoka nchi gani jibu litakua ili inasaidie nini?

Tupende kujisomea Vitabu mbalimbali ili tujue na Jiografia za wenzetu.
Kaka nafikiri kila mtanzania mahali alipo amsaidie mtanzania mwenzake kupata Elimu.
 
Lakini ukiuliza taja nyimbo mpya ya Diamond jibu linapatikana papo hapo bila kumung'unya.
 
Naimani Mwanafunzi wa leo ukimwambia Karanga zinalimwa Gambia kwa wingi huweza kuta hata haijui Gambia au umwambie Kilimo cha mpira Malaya/Malaysia atakubishia mpaka kesho.

Ukitaka kufurahia hii dunia at least uwe Nusu Nusu kila upande Mpira kidogo,Siasa Kidogo,historia kidogo,Jiografia kidogo.

Ukienda beach unajua hizi ni Coral reef,unajua ocean tides/waves kidogo

Unajua Sammata anachezea Genk

Unajua mji mkuu wa Ufilipino ni Manila

Unajua aina za ngombe kidogo Zebu,Fresian
 
Sawa mkuu,nasikia jamaa kapiga mkwala kwa Mh Mdee aombe radhi la sivyo atamtumbua!...ni kweli Gwajima kasema hayo au redio mbao?..
Ni kweli kabisa... Kamwambia akaombe msamaha kwa spika wa bunge kwa kumuita spika fala... La sivyo j pili yuko naye..

My take..

Ni kiki tu..kanisa la GwAjima saivi haliwezi kwenda bila kuwepo kiki hizi. Kashaandaa na ya jumapili ili watu tumsikilize...akiomba sadaka tutoe.

Aendelee kukamata wajinga.
 
Umeandika kitu kimoja kizuri sana.

Ukitaka uyajue haya angalia kipindi cha Skonga EATV ndio utajua shida iko wapi!

Mwanafunzi wa Kidato cha nne anaulizwa Mkoa Maarufu kwa ulimaji wa Tumbaku anataja "Mkoa wa Songea" .
Kwanza Songea sio Mkoa halafu hawalimi Tumbaku.

Hivi vipindi vinatoa majawabu ya jinsi Elimu yetu ilivyo.

Nikurekebishe kidogo Mkuu. Songea ni Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma, na katika Mkoa huu Tumbaku ipo na inalimwa kwa wingi sana katika Wilaya ya Namtumbo.
 
Vitabu siku hizi vinatupa mafua,tuna Google tu,tunasolve past papers tunafaulu mtihani tunakunja vyeti tunaitwa wasomi. Hizo knowledge & skills tushaachana nazo kitambo.
 
Bora hata kimambi yeye ana MBA halali kabisa na hakuwahi kughushi chochote!
Sasa mkulu think tank wake na plan master ni bashite, divishen zero asiyejua hata buni ni kitu gani, kwa mtu kama wewe si hohehahe kabisa uliyepo kwenye kundi la profound?
Haahaahaaaà! Mkuu hayo magamba yanapatikana kwa njia nyingi mbona,yasikutishe wala nini yaani hasa ukiwa mtoto wa kike ni maujanja tu.
 
Kuna mtoto wa aunt yangu kaja mid term ya pasaka nikasema ngoja niangalie kama yaliyomo yamo japo niulize mawili matatu ya darasani...dah ni aibu... Yeye anataka ajiachie tu kwenye sofa remote mkononi jicho kideoni...
 
Bora hata kimambi yeye ana MBA halali kabisa na hakuwahi kughushi chochote!
Sasa mkulu think tank wake na plan master ni bashite, divishen zero asiyejua hata buni ni kitu gani, kwa mtu kama wewe si hohehahe kabisa uliyepo kwenye kundi la profound?
Hukumuelewa mdau ni kuwa mtu mwenye MBA kazi yake ndiyo hiyo tunayoina kwenye mitandao badala mfano ya kuwaelezea Kina mama kutoka kibiashara?!?!? Umeelewa sasa Freyzem?!?!
 
Hukumuelewa mdau ni kuwa mtu mwenye MBA kazi yake ndiyo hiyo tunayoina kwenye mitandao badala mfano ya kuwaelezea Kina mama kutoka kibiashara?!?!? Umeelewa sasa Freyzem?!?!
Wewe unafanya kipi huku kwenye mitandao?
 
Back
Top Bottom