Yoab Mwana wa Seruya
Member
- Oct 4, 2018
- 13
- 28
MAPINDUZI YALIYOFELI
CC F. BUYOBE from Twitter
THE FAILED NKURUNZINZA’s COUP D’ETAT
Rais Nkurunzinza aliondoka Dar Es Salaam majira ya saa 12 na robo jioni kurundi nchini kwake Burundi akiwa na taarifa juu ya jaribio la mapinduzi.
Lakini tulikuja kushangaa kuona ndege ile iliyombeba Rais Nkurunzinza yenye namba ZS-OPR ikigeuza na kutua tena katika anga la uwanja wa ndenge wa Dar Es salaam nusu saa tu baada ya kuondoka.
Haikufanya hivi kwa kupenda bali ni neno la mapokezi kutoka kwa waongoza ndege Burundi.
Wakati ndege ile ikiomba kutua katika anga la Burundi, Waongoza ndege ambao wakati ule walikuwa ni wanajeshi waliopindua nchi, walimuuliza swali hili rubani wa ile ndege; “Status of Souls on Board?”
Rubani akawajibu “Customers”
Ndege haikuruhusiwa,rubani akapaa na kuomba tena.
Swali lilikuwa ni lilelile na jibu likawa lilelile kutoka kwa rubani.
Waongoza ndege wakajibu
"Clear to land at your own risk"
Hapa Rubani akaona ule ni mtego,
Ndege ikapaa tena na kuomba kutua Entebbe International Airport lakini ikakataliwa.
Baada ya kukataliwa ndipo ndege ile ikaamua kurudi Bongo na kama kawaida yetu ya ukarimu tuliiruhusu kutua tena.
Lakini ilikuwaje ndege ile haikuweza kudunguliwa na waasi?
Ni kwamba haikutambulika ndani ya ndege ile kama yupo rais Nkurunzinza kwani haikuwa na muito wa rais.
Kikawaida ndege za maraies huwa zinamuito maalum “call sign” zikiwa zimewabeba viongozi hao. Kwa rais wa Burundi muito wake huwa ni “Burundi 001” lakini siku hiyo ndege ile iliita kwa muito wa “ZS-OPR” ambayo ilikuwa ni namba ya Usajiri ya ndege ile mali ya kampuni ya South Africa
Kwa wakati ule ambao waasi walikuwa wameshaufunga uwanja wa ndege wa Bujumbura, Iliwawia vigumu sana kujua kama ndege ile ingeweza kumbeba rais Nkurunzinza na wasingeweza kutungua ndege ya nchi jirani ikiwa na abiria kuhepuka mzozo wa kidiplomasia.
Ndio maana rais alijiamini.

Sasa kuna swali la kujiuliza, Rais Nkurunzinza aliwezaje kunus harufu ya mapinduzi na hata kujihami kwa kuondoka bila kutumia ndege yake kitendo ambacho kilimuokoa?
Nitajibu swali hili nikiwarudisha nyuma kidogo,
Mapinduzi haya yangeweza kutabiriwa kama mtu angekumbuka uhasama uliokuwa umeibuka baina ya marafiki wawili ambao ni hayati Nkurunzinza na Meja Jenerali NIYOMBARE
Marafiki hawa walisoma chuo kikuu kimoja,wote walikuwa ni makamanda wa juu wa chama cha CNDD. Walipochukua madaraka,Niyombare alipata madaraka ya juu kama Mkuu wa majeshi,Balozi wa Kenya na kama mkuu wa Idara ya ujasusi nchini Burundi.
Akiwa mkuu wa Idara ya ujasusi ndipo urafiki baina yao ukaharibika.
Kwa nini?
Hapa tunalazimika kurudi nyuma mpaka mwezi February mwaka 2015.
Katika wakati huu, Yaani akiwa na miezi mitatu tu tangu kuanza kutumikia nafasi yake mpya ya Mkuu wa Idara ya ujasusi nchini Burundi, Meja Jenerali Niyombare alimtumia ujumbe wa siri kumshauri Rais Nkurunzinza kuwa maamuzi yake ya kujiongezea muhula wa tatu wa uongozi,Kunaweza kulifanya jeshi kutotabirika endapo litatakiwa kutumika kuwazuia waandamanaji ambao hawatapenda jambo hilo la kujiongezea muhula kinyume cha katiba ya Burundi.
Rais Nkurunzinza,baada ya kupokea ushauri huu kutoka kwa rafiki yake wala hakumjibu kitu na badala yake kwa haraka akatengua uteuzi wa Niyombare kama mkuu wake wa Idara ya Ujasusi.
Ili kujipa uhalali wa kugombea, Rais Nkurunzia akaamua kuitumia mhimili wa mahakama na kuitaka mahakama ya katiba nchini mwake kutangaza kuwa hakiuki katiba ya Burundi kujiongezea muhula wa tatu.
Majaji walikuwa kwenye njia panda juu ya hilo.
Tarehe 30 April 2015 majaji wa mahakama wa katiba walikuwa wamekutana ili kupitia vifungu vya sheria kama vile katiba na Makubaliano ya amani ya Arusha kuona kama kweli Rais Nkurunzinza ana haki ya kugombea kwa muhula mwingine wa tatu baada ya mihula yake miwili madarakani kuisha. Walipopitia wakagunduka hakuna sheria yoyote iliyoruhusu lile kutokea.
Wote wakiwa wameshakubaliana juu ya hilo, majaji wakaamua kurudi makwao ili kesho yake waandike uamuzi wao usiompa nafasi Nkurunzinza kuwania tena kiti cha rais.
Haikuwa kama walivyopanga.
Usiku huo huo wa April 30 2015 majaji wakaanza kupokea simu za kuwatishia maisha yao.
Hali hiyo ikawafanya kesho yake tarehe 1 May 2015 kwenda mahakamani na kutoa maamuzi kuwa rais Nkurunzinza anafaaa kuwania awamu ya tatu kwa mujibu wa katiba.
Makamu wa rais wa Mahakama ya katiba SYLVERE NIMPAGARITSE kwa kujua kuwa maisha yake yatakuwa mashakani kutokana na vitisho alivyokwishapokea na kuhofia wananchi wenye hasira kwa maamuzi mabovu, Tarehe 4 May 2015 akatorokea nchini Rwanda kutafuta hifadhi ya kisiasa.
Alikimbia Burundi kupitia mpaka wa RUSIZI baada ya kuvamia kizuizi pale IMBONEKURE(wanamgambo wa Serikali) walipojaribu kuwazuia polisi wa mpakani wasimruhusu kupita.
Muda huu wote tangu hukumu ya mahakama ya katiba, maandamo yaliugubika mji wa Bujumbura na maeneo ya jirani kupinga kitendo cha Rais kuvunja katiba. Polisi walishaanza kuoneka kuzidiwa nguvu pia vifo vya waandamanaji vikaanza kuripotiwa.
Tarehe 10 May 2015 ikiwa ni siku siku ya wanawake duniani,wamama na wadada wa Bujumbura walifanya maandamano makubwa kuunga mkono waandamani wengine wanaopinga rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu ya uongozi.
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawakupendezwa na hali ile huku Rwanda ikilalamika kupokea wakimbizi wengi wa Burundi na kutaka Nkurunzinza arejeshe amani nchi kwake.
Ikabidi uitishwe mkutano wa dharula nchini Tanzania wa viongozi wa jumuiya chini ya Rais Kikwete aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya.
JINSI TAARIFA YA JARIBIO ILIVYOPOKELEWA
Rais Kikwete alikuwa na maraisi wenzake kina Uhuru Kenyata, Paul Kagame na Yoweri Museveni katika Ikulu ya Dar Es salaam.
Umbali wa kama Kilometer mbili tu kutoka ikulu ya Dar es salaam, Yaani katika hoteli ya Serena, Rais Nkurunzinza na timu yake walikuw wanasubiri tu ujumbe wa kuitwa Ikilu ili kwenda kuungana na viongozi wenzake mkutanoni.
Nje ya ukumbi wa Mkutano, Rais Kikwete akapata “security briefing” kuwa Jijini Bujumbura Burundi hali si shwali kwani watu wamejitangazia Jamuhuri rais wao akiwa hapa nchini kwetu.
Katika kuonyesha kuwa taarifa ile ilimshtua rais Kikwete akawataka wageni wake ambao Viongozi wa nchi zao wamsubiri kidogo amepewa taarifa ya dharula.
Rais akiwa nje ya ukumbi wa mkutano akawaita mkuu wa Idara ya usalama Tanzania, OTHMAN RASHID na waziri wa mambo ya nje BENARD MEMBE na akafanya nao kikao kifupi kujadili taarifa ile.
Robo saa baadae, Rais akarudi ukumbini(VIP LOUNGE) na akawatangazia viongozi wenzake kuwa mapinduzi yamefanyika Burundi.
Habari hizi zikatembea tena Kilometer mbili kutoka Ikulu hadi hoteli ya Serena alipokuwepo rais Nkurunzinza na akaambiwa bayana kilichotukia nchini kwake. Hapo timu nzima ya rais Nkurunzinza ikaanza kuwa busy ikifanya mawasiliano na wenzao waliowaacha Burundi kujaribu kuelewa hali ya mambo na jinsi ya kurudi Burundi.
Kwa hiyo Rais Nkurunzinza aliondoka nchini mwake akiwa na machale kuwa muda wowote wangetokea wanajeshi kujaribu kumpindua.
Wakati huu sasa nafikiri alianza kuufanyia kazi ushauri wa Meja Jenerali Niyombare kuwa uamuzi wake wa kuongeza muda kama uzua maandamano, jeshi halitakuwa linatabirika katika kuzuia maandamano hayo.
Ndio maana aliweza kuondoka kwa kutumia ndege ya kukodi ya Afrika kusini. Hii ilikuwa siri yake yeye na watu waaliohusika na ulinzi wake. Kwani walioasisi mapinduzi hakuna aliyebaini kuwa ndege ya “Burundi 001” haikuondoka na “Burundi One” na wao macho yao yote yalikuwa yakiisubiri ndege ile bila mafanikio.
JINSI IDARA YA UJASUSI TANZANIA ILIVYOMSAIDIA
Baada ya kurudi nchini Tanzania, Mahali hasa alipofikia rais Nkurunzinza ilibaki kuwa siri kwa Idara yetu pekee ya ujasusi.
Ingawa habari za uhakika zinasema alikuwa katika vikao usiku mzima na Mwenyeji wake rais Kikwete kuangalia namna ya kurudi salama na kuzima mapinduzi yale. Hapo alikuwa ameshakataa offer ya Serikali ya Afrika Kusini ya kumpa ukimbizi wa kisiasa.
Baada ya team ya kina Othman Rashid kutengeneza route ya kumtoa rais Nkurunzinza na baada ya kupewa ushirikiano na wanajeshi waliokuwa bado watiifu kwa Nkurunzinza ndani ya Burundi, ndipo ikaonekana route ya Kuingia Burundi kupitia Kigoma ingezaa matunda. Hii ni baada ya kuwa na hakika kuwa wanajeshi watii bado wanalimiliki jumba la rais wa Burundi na Kituo cha Taifa cha Radio.
Sasa Rais Nkurunzinza akasindikizwa kwa ndege mpaka Burundi huku barabarani ukitengenezwa msafara “feki” wa rais Nkurunzinza kwa njia ya gari kupitia Mwanza.
Kwa hiyo kama kulikuwa na wanamapinduzi waliokuwa jijini Dar es salaam, basi walitoa taarifa zisizo sahii kwa wenzao wa Burundi kuwa rais wao anaelekea Mwanza.
Wakati akili zote zikielekea kwenye msafara uelekeao mwanza, Rais Nkurunzinza alikuwa juu angani ndani ya Helicopter iliyojikuwa na nembo ya watafiti ambayo ilienda kumshusha kijijini kwake Ngozi na kusafiri kwa siri mpaka kwenye ikulu yake.
Muda wote huo yaani ndani ya masaa 48 hashtag zilizokuwa zikitrend jijini Burundi ni #WhereIsNkurunzinza.
Jibu ili lilijibiwa tarehe 14 usiku kupitia tweet ya rais Nkurunzinza mwenyewe aliyeandika
“Nipo Burundi ndani ya Ikulu, Naamuru waasi wote wasalimu amri na nipo tayari kuwasamee”
Usiku ule ikaanza kusikika milio ya risasi katika kituo cha radio cha taifa kilichokuwa chini ya majeshi tiifu kwa rais. Pia vituo binafsi vya habari ambavyo waasi walitumia kutangaza mapinduzi vikachomwa moto.
Mpaka asubuhi dalili za mapinduzi yale kushindwa zilikuwa wazi na wanajeshi tiifu wakawa wanawasaka majeruhi katika mahospitali ili kujua waasi waliojeruhiwa. Zoezi hili nalo liliibua milio kadhaa ya risasi kwenye Hospital ya taifa Burundi.
OPERATION MBONGO ZERO
Kisa hiki kilichotokea Burundi kinafanana na kilichotokea kwa iliyokuwa nchi ya Zaire mwaka 2001
Operation Mbongo Zero ilikuwa ni jina walilobatiza wanamkakati waliokutana nchini Congo Brazaville ili kupanga jinsi ya kuiingia Ikulu ya Zaire (Marble Parace) na kutekeleza mauaji ya Rais Laurent Desire Kabila.
Yote haya yalifanyika baada ya wanajeshi wadogo “kadogos” ambao ndio waliomsaidia kabila kuingia madarakani kwa kumpindua Mobutu, kuhisi rais amewageuka hasa baada ya kurudisha urafiki na Paulo Kagame waliyekuwa wanamchukulia kama adui wa “kadogos”.
Ni kwa nini?
Ni kwa sababu kadogos wengi walikuwa ni wahutu walioshiriki mauaji ya kimbari Rwanda na kukimbilia nchini Kongo(Zaire).
Sasa na katika mapinduzi haya Kagame pia akatia mkono wake kwa kuwakingia kifua walioshiriki jaribio lile la mapinduzi nchini Burundi.
Hata alipoombwa na Serikali ya Burundi awarejeshe wahusika yeye alidai wale ni wakimbizi na sio waalifu. Maamuzi haya yameacha sintofahamu juu ya mkono wa Kagame kwenye sakata hili.
MWISHO
Sent from my CPH1701 using JamiiForums mobile app