kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Kuna Jambo linasambaa kwa Kasi Sana kwamba wenzetu huko Kaskazini wanapasua vyungu pale wanapoona Jambo limekaa kinyume Cha haki ili miungu yao iangaike na wale walioshiriki aidha kuua, kuiba, kudhulumu au kumnyanyasa mtu mwingine.
Kwa wasimavyo Chungu uangaika na kizazi na hakichagui kabila Wala umri. Kwa mnaofuatilia kuna kipindi tuliona matangazo kwenye groups kuhusu kusudio la kupasua Chungu huko Moshi nadhani Tundulisu alipopigwa Risasi na serikali baada ya kusikia lile tangazo walielekeza wahusika wakamatwe na njia zifanyike kisipasuliwe.
Means wapo baadhi ya watu wanaamini kina madhara na kinaua. Swali langu, kwa kuwa Taarifa zinadai safari hii Kuna vyungu vimepasuliwa huko Moshi kwa ajili ya wale wanawatesa watuhumiwa na Ugaidi, je tunaamini kinaweza kuleta madhara?
Lakini kwa upande w pili ,wapo watu wameamua kufunga na kumwomba Mungu awaadhibu wanaohusika na uovu huu. Je tunaamini maombi yao hayatapokelewa? Je yakipokelewa Nani ataadhibiwa na Nani hatoadhibiwa?
Kama tunaamini Chungu na Kufunga Ni njia sahihi yakuangaika na wanaotesa wanadamu wenzao kwa kujitwalia mamlaka, kuna haja gani yakuangaika kumbembeleza kiongozi wa kisiasa au mtumishi wa Umma atende haki wakati tayari mitego yakumshughulikia asipotenda haki ipo? Na kwanini wanaopindisha haki wanatafuta laana kwa vizazi vyao?