Kundi gani linafurahia utawala wa Rais Magufuli mpaka sasa?

wachukia ufisadi sote tunamsifia , tunaopenda Tanzania ijitegemee kiuchumi na kijamii tunamsifia pia
 
Hahahahahaaaaaa! Magufuli hayupo hivyo. Anafanya mambo mengi kwa pamoja na yote yapo katika ubora ule ule.
uko nje ya mada, maskini shabiki kipofu, anachoongelea mtoa mada ni; Tangu Magufuli kushika madaraka =Kupungua kwa kipato + Kuongezeka kwa gharama za maisha = Kuzidi Ugumu wa maisha. Alitaka kujua hivi ni yeye tu, au ndio hali ilivyo kwa wengi hivi sasa?
 
Watanzania wote tunanufaika utawala wa Rais Magufuli. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuletea mtu sahihi kwa wakati muafaka


Ukiona mtu anayesupport kwa sasa hali ilivyo ujue huyo ni mtoto wa mama...K.K.K hivyo hajui kutafuta. Ila wenye kutafuta kwa hakika hali ya sasa ni ngumu si kidogo...kila kitu bei juu...pesa hakuna
 
Waliojiwekeza ktk miradi isiyostahili usimamizi wa hatua kwa hatu mfano nyumba za kupangisha kama yule afwande aliokuwa na houses 70 haifeel hii hali kbs hata oxygen anayovuta sio hii tunayotumia wengine ila wanaogopatu tu kujiachia kwa uhuru.
 
ambaye haufurahii ni wewe tu ambaye nafikiri hata uwezo wako wa kufikiri ni mdogo , hata jitihada anazozifanya Rais wewe huzioni , ulitaka akuletee pesa mfukoni ? wanaolalamika ni wale wenye fikra ndogo .Rais anafanya kazi kubwa sana ambayo inatakiwa apongezwe na kila mpenda maendeleo .
 
ambaye haufurahii ni wewe tu ambaye nafikiri hata uwezo wako wa kufikiri ni mdogo , hata jitihada anazozifanya Rais wewe huzioni , ulitaka akuletee pesa mfukoni ? wanaolalamika ni wale wenye fikra ndogo .Rais anafanya kazi kubwa sana ambayo inatakiwa apongezwe na kila mpenda maendeleo .
Ni kweli mkuuu...lakini mtoa mada anauliza ni nani mpaka sasa amenufahika kwa utendaji wa mkuu wa kaya... nani maisha yake yamebadilika... nani kipato chake kimeongezeka tofauti na mwaka jana...
wakulima
wafanyakazi
wafanyabiashara


Hali zao zikoje hadi sasa kulinganisha na utawala uliopita???


Fikiri nje ya box...fungua ubongo wako...panua fikra....
 
Ukipewa kazi kubwa usiifanye kwa kukamia utaumiza wengi na kukosesha watu amani. Mambo hufanywa step kwa step ndipo misingi itajengeka vema lakini kubwa Ni unaweza kubana watu saana na mpakamwisho lisionekane lamno ulilowabania hapo ndio tujus uongoz Ni spiritual plus art sio hamasa na ubabe
Bonge la point, post of the day,thanks
 
Ivi wee unaongea nini? Ivi May Mosi Rais alisema nini? na sasa kuna nini? Hiyo inasaidia nini?, watu wa kawida kabisa wana struggle mtaani na wanataabika sana. Bora watu waende Dubai ijumaa na warudi jumatatu ila tusife njaa na siyo wasiende harafu tutabike. After all, nini faida ya Magufuli kufanya yote hayo? Anamfaidisha nani? kama anafanya yote hayo harafu hayamgusi mwananchi moja kwa moja, yana faida gani?

Kwanza jua kuwa siku hizi ma-ofsini watu hawafanyi kazi kwa moyo tena, basi tu wanafanya kwasababu tu sheria zinawabana, ila produce is almost zero, sheria kibao mishahara duni, je inasaadia nini? Kama una ndoto kuwa Rais huyu atabadilisha maisha ya watu wa kawaida wewe ni kipofu ambaye huoni kabisa ila unadhani kuwa unaona. Maisha ni magumu mno mtaani, yaani wewe na wenzako mnaoshabikia vitu ambayo havipo mnastahili kupondwa mawe au umepewa ukuu wa wilaya nini?. Bora Mkwere arudi kuwa Rais wetu, na hakika Mkwere uongozi ni kibaji chake, leo shati lililokuwa linauzwa 20,000 sasa hivi linauzwa 40,000 haoni kama tuna rudi enzi za Nyerere, huoni muda siyo mrefu tutaanza kuvaa nguo za ushirika?
Unaongea kama chiriku, hujui hata unawazungumzia watu gani na hujui hata ni wapi unataka kwenda. Kaa chini kunywa maji mengi waambie hao wenzako wanaofanya kazi bila moyo waache kazi na kama Sheria zinawabana wakashitaki si kuna mahakama kitengo cha kazi?
Unapojaribu kujifanya kumzungumzia mwananchi wa kawaida acheni unafiki, hujawahi kumjali mwananchi wa kawaida na humuwakilishi kwa lolote zaid ya kumtumia kufikisha ujumbe wako. Miradi yenu ya kiwizi imebanwa sasa mnatakiwa wa kumtwisha zigo.
Halafu siku nyingine ukim quote mtu soma kwanza alichoandika na ukielewe, kama unatumia kichwakichwa soma tena utaelewa nilichomaanisha na kama ni wale ngumbaru kaa pembeni
 
Watanzania wote tunanufaika utawala wa Rais Magufuli. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuletea mtu sahihi kwa wakati muafaka

Nimekukataza sweeping statements mbona husikii. Frame your statements in a singular form
 
Watanzania wote tunanufaika utawala wa Rais Magufuli. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuletea mtu sahihi kwa wakati muafaka
Nahisi utakuwa umepandikizwa na chama hapa jf ili kutetea kila aina ya utumbo unaoonyeshwa na chama.
 
Hakuna ajira
Hakuna mzunguko wa fedha
Biashara zimedoda
Kila mtu anakuwa maskini
Makusanyo ya kodi yanalipia mishahara ya wafanyajazi wa serikali
. Makusanyo ya kodi yanawalipa makandarasi wa Kichina
.........itaendelea.....
 
Nimekukataza sweeping statements mbona husikii. Frame your statements in a singular form
Hajitambui hata yeye mwenyewe. Achana naye atakupotezea muda kwani yeye anaamini alizaliwa kwa ajili ya ccm na ccm ndio uhai wake. Njaa mbaya!
 
Watanzania wote tunanufaika utawala wa Rais Magufuli. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuletea mtu sahihi kwa wakati muafaka
Je wewe ni nani Kati ya hawa
Jenister Mhagama,Simbachawene,Mwigulu,Jaffo au Angela Kairuki?
 
Back
Top Bottom