Maguguma
Member
- Mar 13, 2023
- 13
- 6
Mabadiliko yoyote yale huwa yanaambatana na changamoto kadhaa, kitendo cha kuchukua hatua ya kufungia baadhi ya sehemu za starehe bila shaka kitawakumbusha wengi kuwa mamlaka ipo na inafanya kazi.
Kulikuwa na mazingira kadhaa ambayo yamekuwa hatarishi kwa miaka mingi, kwa kuwa mamlaka hazikuwa na ukali katika kuchukua hatua wahusika wengi nao wakwa wanachukulia poa lakini kiuhalisia changamoto za kelele zimekuwa ni kero.
Miji mikubwa na ile inayokua uchafuzi wa mazingira ya kelele ni mkubwa na waathirika ni wengi.
Nawapa pole walioathirika kwa kuwa natambua kufungiwa au kutozwa faini kumewaumiza watu wengi, lakini tunatakiwa kukubali kuwa mambo mazuri pia huwa yanakuja na maumivu.
Jambo la muhimu NEMC isifanye zoezi hilo kwa kumuonea mtu na waiishie kwenye miji mikubwa pekee bali waendelee kuwa ‘active’ na kwa kutenda haki.
Sisi pia Wananchi tunatakiwa kujua tunapotafuta vipato vyetu au kuburudika hatutakiwi kuwa kikwazo kwa wengine, tuwe na mipaka ya furaha yetu kutokuwa kero kwa wengine.