Kuna ukatili unafanyika kwenye wanyama wanaofugwa kama Mbuzi, Ng'ombe

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,569
5,604
Hivi kwa jua hili, mbuzi au ng'ombe anafungwa juani kuanzia asubuhi hadi jioni. Hii sio sawa kabisa, kama mtu hawezi mkatia majani basi aende akachunge.

Unakuta mnyama anahema mpaka unamuonea huruma. Na pengine hata maji hawapewi hadi hio jioni. Hili suala ni la kuliangalia, hawaviumbe nao wana damu mateso si mazuri.
 
Kuna wale ng'ombe wanaosafirishwa kwenye magari sometimes siku tatu hawajala ,hawajanywa wakati dereva anasimamisha Gari anakula na kunywa

Kuna dhambi zingine hazisameheki
 
Bora na wewe umeliona hilo..Ng'ombe anabebeshwa mkokoteni wenye matofali takribani 800, akikosea kunyoosha njia atakula viboko vya uhakika hv hawa wanaotunga sheria hawalioni hilo wanyama wanateswa au kwasababu wao hawajui kuongea ..Inasikitisha sana.
 
Unazungumzia wanyama wakati binadamu wenyewe wanateseka chini ya CCM ya kina Wasira,kuna watu kupata mlo wa SIKU ni bahati na bado hana pa kulala.
Kwahio ukizungumzia wanyama kuteseka wala hawashtuki
Ipo siku utashindwa kubeba mimba ya mumeo na kuilaumu ccm
 
Back
Top Bottom