Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,404
- 10,900
Wiki kadhaa zilizopita nilienda CRDB kuomba Mkopo binafsi.
CRDB wakasema lazima mshahara wangu upite kwao. Nikahamisha mshahara kutoka NMB kwenda CRDB ndipo nikajaza form za mkopo na kuzirudisha CRDB Bank.
Nilivyorudisha tu fomu loan officer akaniambia sasa hivi mfumo unasumbua kidogo huenda ukawa tayari after two weeks. Mie nikadhani yule afisa anataka kitu kidogo na kwa vile hizo wiki mbili kwangu hazikuwa nyingi sikutaka kuanza kuwaza habari za kitu kidogo.
Lakini baada ya kuanza kupita pita katika mitandao hasa page za CRDB naona kuna msururu wa watu wanalalamika kuwa huenda CRDB imefulia maana kuna watu wamerejesha fom toka December mpaka leo hawajapewa mkopo. Na wengine wameanza kukatwa rejesho bila kupewa mkopo. Ukiwapigia Simu CRDB au ukiwaandikia wanakwambia tunafanyia kazi suala lako.
Hapa najiuliza ina maana kweli mfumo unasumbua,au ni benki imeyumba haina fungu la kutosha kukopesha au kuna kitu gani kimewakumba CRDB?