Naam na ndivyo inavyotakiwa afanye,a report kwa mtandao husika,au arudishe ye mwenyewe,teknolojia inakuwa kwa sana,uwa Kuna utaratibu wakurudisha we mwenyewe ulokosea,!!,makampuni huwa yanatangaza Hilo.Kama amekosea kutuma arudishe yeye mwenyewe mhamala uliokosewa bila hata kukushirikisha wewe uliyetumiwa.
Wewe huelewi,mimi sinaga muda wa kuangalia salio, ukituma natoa
Soma comment no 83Nimesoma naona kama haiwezekani labda atokee alietapeliwa kwa njia hiyo anieleweshe.
Soma comment no 83Na nikitaka kuihamisha kwenye laini nyingine bila kuangalia salio nini kitatokea?
Soma comment no 83mimi sinaga muda wa kuangalia salio, ukituma natoa
Naomba ajitokeze hapa mtaalamu wa IT atufafanulie hili,maana wengi tunaona ni kama kiinimacho vile!!,humu kwenye jukwaa hili tunawataalamu wengi wa computer nk.Wewe huelewi,
Tapeli anakuwa amekuwahi kuomba Kutoa pesa kupitia ombi la kufanya muamala Kwa mtu aliye mbali, hivyo ombi lake litashufhulikwa kwanza mara tu utapoingiza password Kutoa pesa au kutumia pesa au kuangalia Salio.
Umeambiwa solution ni kuingiza namba ya Siri fake ndio njia pekee ya kucancel ombi la tapeli Kutoa pesa Kwa ac Yako.
Nilichogundua, uelewa Kwa watz wengi ni mdogo.
NB: Ukitumiwa pesa na tapeli, hakikisha unaangalia Salio Kwa password fake, hapo tapeli hatoweza kukuibia, labda akutumie pesa ingine.
Ahsante
😀😀😀Hawa washamba hawajawahi kujichanganya kwangu, atume basi hiyo laki nimuonyeshe ngoma inavochezwa 😁
juzi kuna MTU kanitumia buku,nikampigia akasema kakosea nikamwabia aitoe anasema nirudishe nikamwambia sifanyi Nazi hiyo⚠️ 🎭`
WIZI MPYA
Kuna mbinu mpya ya matapeli wamekuja na kuwalaghai watu inaoitwa 'IMERUKA'.
Tapeli hukutumia pesa kwenye simu yako akitumia namba yake.
Hii si pesa fake, ni ya kweli kabisa anakutumia pesa kidogo kama laki 100000 au elf 50000 na hata hana shaka.
Baada ya kutuma pesa hizi kisha anaanzisha muamala wa kutoa pesa kwenye account yako yako. kuna menyu ya kurequest muamala kutoka kwenye namba ya mtu mwingine ambae yupo mbali. Ila yule mtu atatakiwa aweke namba yake ya siri ili kuruhusu muamala huo.
Sasa tapeli anafanya hivyo kwa sababu anajua Unapopokea ujumbe kwenye simu yako kuwa umepokea pesa jambo la kawaida ni kufurahia na kisha kutaka kuangalia salio lako.
Ili kuangalia salio utahitaji kuweka Nambari yako ya siri (Msimbo).
Mara tu utakapofanya hivi utakuwa umethibitisha ombi lake la kutoa pesa kwenye akaunti yako.
Akaunti yako itaruhusu ombi lake la kutoa hela kiotomatiki na kuchukua pesa zako.
Ujanja ni kukurubuni tu kwa kiasi kidogo ili kukuibia.
Ili kujilinda dhidi ya ulaghai huu wakati wowote ulipopokea amana hiyo isiyotarajiwa, ili kuangalia salio lako kwanza weka Nambari ya Msimbo isiyo sahihi makusudi.
Kitendo cha wewe kuweka Msimbo wa uongo itafuta maombi yoyote ya tapeli kiutoa fedha toka akaunti yako. Kisha angalia salio lako kwa Nambari yako halisi ya Msimbo.
Kwa uhamisho huu mpya wa pesa za kielektroniki na Artificial Intelligence (AI) tufanye hivyo kila wakati ili kuepuka kudanganywa na matapeli hawa ambao kila mara wanakuja na mbinu mpya za kujaribu kutuibia.
Shiriki habari kama hizi kila wakati na familia na wafanyikazi wenza pia ili kuwafahamisha na kuwa macho.
KAA MACHO ‼️
View attachment 3150393