SoC03 Kuna mafenesi mangapi katika mbegu moja ya fenesi

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Mwanangu usipofanya hii homework kesho darasani utamfanya mwalimu ashindwe kuelewa aanzie wapi kupima uelewa wako.Somo lenyewe ni aina za matunda mbalimbali. Na hapo tulikuwa tumenunua tikiti,nanasi,mapera , fenesi,ndizi na machungwa. Mke wangu alikuwa akimenya matunda yote na akimuelezea binti yetu kipenzi wa miaka minne nyama na mbegu za kwenye matunda na kumfanya binti yetu ayahesabu matunda yale yaliyokatwakatwa.

Wakati tunakata fenesi,badala ya kumuuliza idadi ya mbegu Zilizomo katika fenesi ,nikamuuliza kuna mafenesi mangapi katika mbegu moja ya fenesi? Swali hili lilinifanya kutafakari.Ni rahisi sana kuhesabu namba za mbegu katika fenesi lakini kuna ambaye anaweza kusema kuna mafenesi mangapi ambayo mbegu moja ya fenesi inaweza kuzalisha? Kesho haionekani na haitabiriki . bado mkulima hupanda mbegu, kwa sababu tu anataka yeye mwenyewe na kizazi kijacho.

Nikakumbuka zamani nilikuwa naishi maeneo ya Boma Road maghorofa ya Canvas Morogoro kulikuwa na Bwana mmoja rafiki wa mazingira akisia mbegu za miti na kuuza,nilibahatika kujifunza aina mbalimbali za miti karatusi, sadilea, giriveria,mswila, kalibea, kashwelina, mitiki, mijohoro, mibono, michongoma na jamii ya miti ya mninga na mpingo.

AMA HAKIKA UKISTAAJABU YA MUSSA UTAONA YA FIRAUNI
Hata miti hii yote ya mbao hii inazo mbegu kama miti za matunda na kapunje cha mbegu ya karatusi ndani yake kana tumbegu tuduchuduchu twingi ambato ukitukusanya na kutusia unapata msitu wa miti mingi zaidi.
Swali ni je katika kila Mtanzania ambaye anakula matunda kila siku au kwa namna yeyote tu yale yanayeoza sokoni au kutupwa jalalani na mbegu zake au yanayejiotea barabarani au kujiangukia mitini, ingetokea kungekuwa na ukusanyaji wa mbegu hizi zote kama tunavyookota makopo pasipokuipoteza hata moja je ni lugha gani tungezungumza kama Watanzania.Je ni miti mingapi ingeweza kupandwa kila mwaka na kukua kufikia hatua ya kuleta utofauti.Yamkini ,tungekuwa matajiri wa mbegu za kila aina ya kiotacho ardhini.

Juzi juzi nilihudhuria kikao cha harusi ya kijana wa rafiki yangu ,tukiwa kwenye kikao nikapewa jukumu la kwenda kumnunulia vifaa vya kuanzia maisha kamavile kitanda, kabati na vifaa vingine vya useremala vya sebuleni ,nikiwa kwenye karakana ya mafundi seremala wakanambia wanatumia mbao za mchina ,nikashangaa inakuwaje hivyo, Ndipo nikaanza kufanya utafiti namna zile malighafi za mbao zinavyochakatwa kusagwa kwa mmachine na kuwa unga mpaka kuingia sokoni kama mbao.

Na namna ambavyo kama mashine zitafanya kazi nchini Tanzania ni dhahiri utunzaji wa mazingira na ukataji wa miti utakuwa wa kiteknolojia zaidi pasipo kuzuru mazingira wala kuharibu ardhi na kuongeza soko na tija katika rasilimali hii ya useremala na ujenzi.

Hebu tuangalie tulivyonavyo sasahivi, kwani kesho inanguvu ya kuturudishia vyote ambavyo labda tulidhani tumevipoteza au hatutaweza kuvipata tena.Mwenyezimungu anaijua kesho ya kila kiumbe.Anaweza asiisemee leo ,lakini yuko nasi katika kila hatua anawajibika. usiamini hatima, mwamini yule aliyetengeneza hatima yako.

Baadhi ya watu hujifunza kwa njia ya kuboreka kwamba mistari fulani haina kibwagizo na hadithi fulani hazina mwanzo, msingi au mwisho. Maisha ni kuhusu - kutokujua na kuukubali wakati na kuufanyia vyema bila kutambua kitakachofuata. panda tu mbegu sahihi na uishi kwa kumtegemea YEYE, ana fenesi bora zaidi kwa ajili yako.

Ufahamu wa ajabu ulitokea wakati wa ziara yangu kwa binamu yangu huko Tabora.Anaishi katika nyumba nzuri yenye bustani iliyotunzwa vizuri nyuma ya ua .Tulipokuwa tukitembea , alinifahamisha kwamba siku moja kabla alikuwa ameweka dawa maalum ya magugu, hivyo haikushauriwa kuketi kwenye nyasi.

Kwa ushamba wa kilimo nikamuuliza hayo magugu yanaitwaje akasema Sangari ila magugu ni aina ya majani yote ambayo huwa hayahitajiki au yanaonekana yana madhara kwa mimea mingine ambayo imepandwa na binadamu kwenye bustani, kilimo,au sehemu nyingine za asili. Kwa ujumla, gugu inasemekana Kuwa kero katika sehemu isiyohitajika.

Kama kawaida nilivyo fukunyuzi,aliponielezea nikaanza kujitafakarisha .Huwa naamini chochote kilichopo duniani huwa kiko kina jukumu ambalo kinapaswa kulitimiza.Hivi kwanini Gugu halina thamani?Inanitatiza, baadaye nilipopitia wavu, niligundua kwamba kulikuwa na mimea au mitishamba mingi muhimu ambayo hapo awali ilichukuliwa kuwa magugu na kutupwa. Ilikuwa tu kwamba uzuri au thamani yake iligunduliwa baadaye. Inastaajabisha sana, kama ambavyo watu wengi wa karibu nasi tunavyowachukulia kwa mtindo sawa kama magugu?

Kumekuwa na mifano ya watu wengi wakubwa ambao aidha waliondolewa makazini, mashuleni au majumbani kwa sababu tu walionekana hawana maana au wanawaharibu wengine wanaowazunguka au hawafanyi kile ambacho wengine wanakitaka. Lakini kwa kuongea, hatujagusa kiwango chao halisi.

Kila mtu ana kila kitu kinachohitajika ili kuwa mkuu-kila mtu binafsi kwenye sayari hii yupo kuchukua jukumu maalum - suala ni, tunawahukumu mapema sana na kuwakataa kama magugu kabla ya kuwaacha kuchanua kwa uwezo wao wa mwisho.

Kila mtu si wa kawaida na ana vipawa vyake vya kipekee. Wameumbwa kama kazi bora za kipekee katika maisha yao. Huwezi kutarajia watu wote wana sifa zinazofanana na wewe. kama magugu, ni lazima wawepo ili kutekeleza jukumu lao la kipekee, wao inabidi wawepo ili kukusaidia kukua na hilo lazima liheshimiwe. hivyo wakati mwingine unapokaribia kukataa mtu na kujiona hana maana na kama mdudu ,kumbuka tu kuwa haujagundua au kugonga uwezo wake halisi. bado.

Binamu yangu huyu analo eneo kubwa tukizunguka kwenye bustani zake na mashamba ya tumbaku Tabora huku nikishangaa shangaa katika umri huu wote huyu binamu yangu amewezaje kupangilia mambo yake ilhali yeye ni mwanamke tu. Matone ya maji ya mvua kwenye maua ya pamba yakawa yametuama akilini mwangu .
Pale tone la mvua likituama majini kwenye ziwa linapotea lakini matone la mvua likienda kwenye maua hutengeneza mng’ao kama lulu.Hii inamaanisha kampani ina umuhimu sana ?

Watu wanaomzunguka mtu wanaweza kumharibu au kumboresha.Inategemea unataka uangukkie wapi na yupi unamtaka karibu yako. Fikiria watu ambao unatumia muda mwingi nao ,ni wale watu ambao wanakutia moyo? Wanakupa hamasa? Wanakusaidia kutimiza ndoto zako ?Kama sio ,wwatupilie mbali ,kama vile mkulima anavyoyatupilia mbali magugu shambani .

tabia yako inaweza kuhukumiwa kulingana na kampani unayoikumbatia au unayokaa mbali nayo .ni bora wakati mwingine kuwa peke yako kuliko kuwa katika mduara wa majuto. kuwa na watu chanya ambao wanaweza kufanya wewe uwe wa thamani kama lulu na ung’are kama almasi. chukua uamuzi leo; chagua mduara wako, kwani huo utayaunda maisha yako

How-to-grow-Cotton.jpg
 
Hii aya
Kila mtu si wa kawaida na ana vipawa vyake vya kipekee. Wameumbwa kama kazi bora za kipekee katika maisha yao. Huwezi kutarajia watu wote wana sifa zinazofanana na wewe. kama magugu, ni lazima wawepo ili kutekeleza jukumu lao la kipekee, wao inabidi wawepo ili kukusaidia kukua na hilo lazima liheshimiwe. hivyo wakati mwingine unapokaribia kukataa mtu na kujiona hana maana na kama mdudu ,kumbuka tu kuwa haujagundua au kugonga uwezo wake halisi. bado.


Inakinzana na hii
Watu wanaomzunguka mtu wanaweza kumharibu au kumboresha.Inategemea unataka uangukkie wapi na yupi unamtaka karibu yako. Fikiria watu ambao unatumia muda mwingi nao ,ni wale watu ambao wanakutia moyo? Wanakupa hamasa? Wanakusaidia kutimiza ndoto zako ?Kama sio ,wwatupilie mbali ,kama vile mkulima anavyoyatupilia mbali magugu shambani .


Ni lini na yupi atupwe kama magugu, na lini na yupi awepo kutimiza jukumu lao la kipekee (😊ambalo ni kuvuruga amani ya wengine?)
 
Hii aya


Inakinzana na hii


Ni lini na yupi atupwe kama magugu, na lini na yupi awepo kutimiza jukumu lao la kipekee (ambalo Ni kivuriga amani ya wengine?)
Kiasi inatupasa tuishi kwa akili sana ilikuweza kubalansi matakwa ya nafsi zetu na jamii chanya
 
Kesho watoto wataelewa nani alikuwa mtiifu darasani na kufanya homework na nani alikuwa mtoro na kukwepa darasa...mtaa ndio umewalea watoto na ndio unaenda kuwapokea ,wapo watakaoendelea na wapo jamii itakayowaamulia waishie mtaani...watu washaanza kupigiana simu kuhusu wadada wa kazi na wakaka wakaka wakazi...urithi mzuri wa mtoto ni elimu...
 
Back
Top Bottom