Kuna haja ya Wananchi kudai Kodi ikatwe kwenye Mishahara ya Wabunge

Ndio maana kila kitu wanapiga makofi tuu bila kuhoji, ila huu ni ujambazi kabisa yaani yanapanga kodi halafu yenyewe hayalipi, hili swala itabidi libadilike tuu kwa nguvu za wananchi, mkoloni mweusi ni hatari kuliko mzungu
 
Pamoja na yote....

Ila mbunge ana haki kisheria kuongea anachoona ni sahihi....hasa ndani ya BUNGE.....

Kila mtu ana haki ya kujieleza na kusikilizwa......ndani ya BUNGE huongelewa mengi.....ingekuwa amefanya kosa kibunge basi SPIKA asingemvumilia kuendelea kuongea.....

#KaziIendelee
Tatizo lenu nyie Wabunge mko kimaslahi yenu zaidi, Mwananchi anapoonewa mnafanya nini? Sheria ngapi za kipumbavu mmepitisha halafu mnazishangaa wenyewe mmepitishaje?
Badilikeni, ili Kazi inayoendelea iwe kwa ufanisi mkubwa.
 
Hawa wabunge wetu wamejikuta Kama wao sio wananchi, wanajiona Kama wao Ni Daraja jingine kabisa katika jamii.

Wananchi tumewavumilia tukidhanj wao Ni watetezi wetu lakini kinyume chake imekua Ni Wala Kodi zetu. Wamekua wakipata exemption nyingi tu za bure lkn hata hawachangii Kodi Ina maana wanatumia Kodi zetu bila wao kukatwa.

Wanalipiwa bure matibabu Tena first class bila kukatwa katika mishahara yao Ina maana wanatumia Kodi zetu. Wanapewa kiinua mgongo kikubwa kabisa bila kukatwa katika mishahara yao Ina maana wanatumia Kodi zetu.

Wamekua badala ya kuwa watetezi ndo hao wanataka tuwekewe Kodi ya kichwa kwenye simu bila aibu. Kwa vile wao wanatumia umeme wa bure majumbani kwao wameona Bora tulipie Kodi ya majengo kupitia umeme wa Luku. Ifike mahali wananchi tuseme baasi inatosha maana ishakua too much haswa.

Wananchi tupaze sauti kila mahali tusikubali inatakiwa wote tukatwe Kodi zote tunazokatwa Kama ya bima, hazina au popote wote tukatwe na wao wakatwe.
WATANZANIA WATE TUKISEMA BASI, TUKIANDAMANA NCHI NZIMA WENYE AKILI MFULULIZO NA TUKISHINIKIZA KWA SIKU TATU TU WATATIA ADABU HAWA WATU NA WATATUSIKILIZA TU KWA VYOVYOTE OTHERWISE SAFARI BADO NDEFU SANA LABDA WATOTO WETU WATAWEZA.
 
Wewe unalalamika kitu gani???--- kwani hujui kwamba Wabunge sio raia wa nchi hii??!!, wao ni Expatriates na ndio maana licha ya kulipwa mishahara pia hulipwa "takrima ya vikao" (sitting allowances). In other words they are bank robbers, wanaibia sana nchi na hii inawafanya wasiwe na huruma kwa wananchi.
SURE MKUU
 
sasa itoshe na tuanzishe hashtag ya kila raia alipe kodi katika kila kitu!
ngazi zote za kiraia na ijulikane kwanini hawalipi kodi.
hata wakienda jimboni kwao na popote kila mtu ajue kuwa wabunge hawalipi kodi lakin wanapigia kelele maendeleo.
na ijulikane kiwango wanacholipwa na bado hawalipi kodi.
elimu hii ni MUHIM SANA! tena kuanzia chekechea. iambatane na elimu ya rushwa na haki.
 
Covid 19 watoke bungeni wanatafuna kodi zetu bure...
Wabunge mishahara ipunguzwe na walipe kodi.
Waanze kukatwa pesa ya mifuko ya hifadhi za jamii ili wajiwekee pensheni
NADHANI HATUNA MIPANGO WMADHUBUTI WA KUMOBILSE MAMBO, MAMBO MENGI YA OVYO YANAFANYIKA HATUNA PLATFORM NZURI YA KUYAELEZA HAYO MAMBO KWA WANANCHI.

LAZIMA WAJITOLEE WATU WA KUTUONGOZA KATIKA KUPINGA UPUUZI WA NAMNA HII, HATUNA MOBILISER, IWE TASASISI ZA KIDINI, WANASIASA, WANAHARAKATI, WANAFUNZI, TAASISI ZA KIRAIA, VYOVYOTE ITAKAVYOKUWA WHAT WE NEED IS MOBILISER WENYE MISIMAMO LAZIMA ALISHIKE HILI NA APO TUTAFIKA TU.
 
Tatizo lenu nyie Wabunge mko kimaslahi yenu zaidi, Mwananchi anapoonewa mnafanya nini? Sheria ngapi za kipumbavu mmepitisha halafu mnazishangaa wenyewe mmepitishaje?
Badilikeni, ili Kazi inayoendelea iwe kwa ufanisi mkubwa.
Sasa Kama tu unaongozwa na hisia kuniita mbunge huoni kuwa hata hoja utatambaa hivyohivyo?!!!🤣🤣

Mimi KULI tu hapa Sokoni Buguruni 🤣🤣🤣

Ikiwa bungeni wabunge wanaongelea MASLAHI YETU.....iweje KOSA kuongelea maslahi yao hapohapo bungeni?!!! Khaaaa 🤣🤣
 
Hawa wabunge wetu wamejikuta Kama wao sio wananchi, wanajiona Kama wao Ni Daraja jingine kabisa katika jamii.

Wananchi tumewavumilia tukidhanj wao Ni watetezi wetu lakini kinyume chake imekua Ni Wala Kodi zetu. Wamekua wakipata exemption nyingi tu za bure lkn hata hawachangii Kodi Ina maana wanatumia Kodi zetu bila wao kukatwa.

Wanalipiwa bure matibabu Tena first class bila kukatwa katika mishahara yao Ina maana wanatumia Kodi zetu. Wanapewa kiinua mgongo kikubwa kabisa bila kukatwa katika mishahara yao Ina maana wanatumia Kodi zetu.

Wamekua badala ya kuwa watetezi ndo hao wanataka tuwekewe Kodi ya kichwa kwenye simu bila aibu. Kwa vile wao wanatumia umeme wa bure majumbani kwao wameona Bora tulipie Kodi ya majengo kupitia umeme wa Luku. Ifike mahali wananchi tuseme baasi inatosha maana ishakua too much haswa.

Wananchi tupaze sauti kila mahali tusikubali inatakiwa wote tukatwe Kodi zote tunazokatwa Kama ya bima, hazina au popote wote tukatwe na wao wakatwe.
Naunga mkono hoja, pamoja na kwamba wanajiwakilisha wao na Matumbi yao kwanini wasitozwe kodi
 
Wakatwe kodi kwenye mishahara na posho.
Wakatwe pesa ya kuchangia mifuko ya hifadhi ya jamii.
Posho ya vikao iondolewe kwani wapo kazini.
wabunge/Spika wasiwe na uwezo wa kujipangia kufanya vikao vya posho.
Inatakiwa tupaze Sauti mpka mama Samia asikie kilio chetu wananchi. Kodi iwekwe Kama wafanyakazi wengine Kama. hawataki Basi watoke
 
Kama watu wanakukubali na wanataka uwe mbunge wao watakuchangia pesa ufanye kampeni badala ya wewe kwenda kuwahonga wakuchague.
Wabunge hawatoki SAYARI YA MARS.....

Mchakato wa mtu kuwa mbunge huhusisha PIA fedha nyingi.....

Hakuna "lofa" awezae kuwa mbunge....

Hivi unaweza Kweli KUTENGENEZA timu ya kukuwezesha mpaka kilele Cha kampeni bila ya KUWAWEZESHA KIFEDHA?!!!!

Bahati mbaya iliyopo tunapenda kudanganyana kuwa MHITIMU WA CHUO KIKUU anaweza kuwa mbunge simply kwa "kuweza tu kuongea". ....

Mh.David Silinde aliwahi kusema kuwa hakuwa hata na senti baada ya chuo kikuu ila ALIWEZESHWA NA MBOWE......

Sasa mtu awekeze mapesa yake halafu asilipwe kiinua mgongo?!!! Kweli ??!!!

Ikumbukwe miaka 5 anakuwa tu anawatukia wananchi....huku wengi e wakitaka msaada mpaka wa kifedha......

THINK THRICE

#KaziIendelee
 
Sasa Kama tu unaongozwa na hisia kuniita mbunge huoni kuwa hata hoja utatambaa hivyohivyo?!!!🤣🤣

Mimi KULI tu hapa Sokoni Buguruni 🤣🤣🤣

Ikiwa bungeni wabunge wanaongelea MASLAHI YETU.....iweje KOSA kuongelea maslahi yao hapohapo bungeni?!!! Khaaaa 🤣🤣
Wewe ni KULI umayewasemea wabunge? Ungekuwa KULI wla usingejua wabunge wanafanya nini Bungeni, ungechoshwa na kazi yako ya ukuli.
Maslahi ya hapo BUNGENI na KULI ni wapi wapi? Huoni kama ni MBINGU na ARDHI.
 
Kutokulipa kodi no uhujumu uchumi wabunge sharti waone aibu,nchi hii inategemea kodi wao wanajikwepesha kiss wanatunga sheria??
Kiunafiki unamteua Amisa kushawishi kodi huku we we uliyemteua hulipi kodi does it make sense
Wabunge wanatufundisha kodi sikitu halali kulipa ukiweza kujikwepesha basis kwepa nahili nijambo linaloonesha uwezo wao finyu kufikiri,tamaa ilivyo wajaa na kukosa uzalendo kwa taifa lao.
Shine shine site tutumie hashtag hii
#Wabunge msikwepe kodi,uzalendo kwanza...
 
Back
Top Bottom