Kuna Dunia nyingine mpya imepatikana

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
711
1,430
Kuna Dunia nyingine mpya imepatikana
1_20250217_190047_0000.png


Wanasayansi kutoka Nasa wamethibitisha kuwepo kwa sayari mpya aina ya HD 20794D Super Earth 🌎, iliyoko umbali sawa na miaka 20 ya miale ya mwanga katika eneo ambalo nyota zinakaa. Sayari hii kwa ukubwa ni takribani Mara sita ya Uzani wa Dunia.

Iligunduliwa kupitia mfumo wa Radial ufanya kazi ya kufuatilia mifumo ya nyota na kufanikiwa kunasa picha za moja kwa moja kuhusu Dunia mpya ambapo mzunguko wake wa Duara unaamanisha kuwa inazunguka ndani na nje ya eneo linaloweza kukaliwa na kuzua maswali mengi kuhusu uwezekano wa kukaliwa na maisha yakawa yanaenda.

2_20250217_190047_0001.png


Misheni za siku zijazo ni kuhusu uwezekano wa wanadamu kukaa kwenye Sayari zingine ambazo mwanzoni watu walikua wanajua haiwezekani ila miaka ijayo inawezekana na haswa kugundulika kwa Dunia mpya kutachochea zaidi watu kuishi huko.
 
Wafia dini watasema hiyo pia imeumbwa na Mungu.

Binadamu itafika miaka ataumba binadamu mwenzie hata bila ya kujamiiana.
Magonjwa kama Kansa ambayo kwa sasa ni ngumu kuyatibu, yatapata suluhisho.

Kuna mambo mengi mazuri na yaa kustaajabisha binadamu atayafanya hata kama ni miaka 4,000 ijayo.
Na itazidi kuwa wazi kwamba uwepo wa Mungu haiwezekani.

Watu duni na wasiojiweza kiuchumi watabaki hapa Duniani, huku wenye uwezo wakihamia Sayari zingine huko.
 
Hiyo itakuwa ni light years, si mchezo kufika. Imagine sayari za karibu tu hatuwezi kufika sawa sawa, 1 light year tu Nafikiri ni matrilioni ya kilometers Sasa zidisha na hiyo ishirini si ndio balaa. Tukiweza kusafiri Kwa spidi ya mwanga au inayoelekea kukaribiana na mwanga Kwa mbali basi tunaweza kusafiri kwenye space na kuweza kubadilisha mtazamo mzima kuhusu sayansi. Kuna uwezekano mkubwa Kuna matrilioni ya sayari kama ya kwetu...Tatizo ni moja tu haya mambo yanahitaji akili kubwa sana.
 
Hawa jamaa wakati mwingine wanatudanganya tu.
Mbona trip za kuelekea mwezi hapo jirani tu hazifanyiki sembuse kugundua dunia ya umbali mkubwa hivyo!
Mwezini hata wewe ukitaka unaenda tu ni mwendo wa miezi isiyopungua mitatu mpaka kufika.

Wanasayansi kwa sasa wapo interested na kuexplore maeneo mengine kabisa ya anga za mbali maana yanaweza kuwa potential zaidi kuliko mwezini ambapo mwaka 1961 walienda lakini zaidi ya sifa hakjna kingine walichokipata.Hizo sayari wanazozigundua ambazk wanaziita "Earth like planets" mpk sasa zimegundulika zaidi ya tisa ambazo zina sifa sawa na dunia yetu tunayoishi zikiwa na ardhi pamoja na kufunikwa na bahar na vyanzo vingine vya maji hivyo uwezekank wa kuwa na maisha a viumbe wengine ni mkubwa sana.

Kwa kutambua hilo miaka ya sabini NASA ilituma chombo kinaitwa Voyager kiende kikaexplore huko angani na kirudishe taarifa duniani juu ya uwepo wa ustaarabu mwingine huko angani,Chombo cha voyager tangu kilivyorushwa mwaka 1977 mpaka leo kinaendelea kurandaranda huko angani,na kikubwa zaidi kina ujumbe ndani ya CD inayoitwa Golden record ambapo ndano ya Golden records kumewekwa directives unaoonyesha ustaarabu wa dunia yetu ikiwa pamoja na muziki na utamaduni wetu,sauti za wanyama wanaoishi duniani,michezo yetu na maelekezo ya jins ya kufika kwenye dunia yetu.Nasa wanaamini ipo siku chombo hicho kitakapofika mwisho kitadondokea kwenye ustaarabu mwingine ambapo Golden records itakuwa msaada kwa Aliens watakayoikota
 
Back
Top Bottom