KWELI Kuna dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV ndani ya saa 72

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
PEP-HIV-Treatment-Medication-11.jpg


Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?

Je, kuna ukweli kwenye hili?
 
Tunachokijua
Njia ya kukukinga usipatwe na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira au hali hatarishi ipo. Kitaalamu huitwa Post-exposure prophylaxis, au kwa kifupisho PEP.

Kwa mujibu wa Miongozo ya Matibabu na Orodha ya Kitaifa ya Dawa Muhimu Tanzania Bara iliyotolewa na Wizara ya Afya mwaka 2021, PEP ni utumiaji wa haraka wa dawa ili kuzuia maambukizi kufuatia mazingira ambayo mtu anadhani yanaweza kumsababishia kupata maambukizi ya VVU (Mfano: kugusana kwa damu au maji maji mengine ya mwili).

PEP inasaidia kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Hata hivyo, inaelezwa kuwa inapaswa kuanza PEP ndani ya saa 72, au siku 3, baada ya kuambukizwa au kuhisi kuambukizwa VVU, la sivyo haitafanya kazi.

Mtu aliyepitia mazingira hatarishi yanayoweza kumfanya aambukizwe VVU anapaswa kufika kwenye hospitali yoyote ya serikali ili apatiwe msaada, pamoja na kupimwa kwanza kama tayari ni muathirika wa VVU au la.

Dozi ya mwanzo inapaswa kutumiwa ndani ya saa 2 baada kuhisi kuambukizwa na kabla ya kumpima mtu mwenye mashaka.

Kwa Tanzania, TDF 300mg+3TC 300mg+DTG 50mg au maarufu zaidi kama TLD ndiyo dozi ya dawa inayotumika kwa watu wazima. Kwa watoto, AZT+3TC+LPV/r ndiyo hutumika.

Muongozo huo wa Wizara pia unaonesha kuwa dozi hiyo hutumiwa na watu wazima kwa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa siku 28, huku kwa watoto ikitumiwa mara mbili kwa siku katika muda wa siku hizohizo 28.
Asante sana mzee na ikitokea pep ilifail huo mwez mmoja wa pep vipimo vya vitasoma positive?
Hakuna Jibu la Moja kwa Moja kuwa PEP imefail ila kama Ikitokea Ukapata Maambukizi na kwa bahati mbaya Ukaathirika Kutokna na Sababu mbalimbali..Ik8wa ni Pamoja na Kuchelewa Kuanza PEP..
Vipimo vitasoma Positive...

Ushauri wangu, Jitahidi Kuanza PEP mapema Atleast Stat pack ya Ndani ya Masaa mawili na isizidi masaa 72
 
Hakuna Jibu la Moja kwa Moja kuwa PEP imefail ila kama Ikitokea Ukapata Maambukizi na kwa bahati mbaya Ukaathirika Kutokna na Sababu mbalimbali..Ik8wa ni Pamoja na Kuchelewa Kuanza PEP..
Vipimo vitasoma Positive...

Ushauri wangu, Jitahidi Kuanza PEP mapema Atleast Stat pack ya Ndani ya Masaa mawili na isizidi masaa 72
Oooh sawa mkuu,,,, Ila yeye alianza 25hrs baada ya kuwa exposed na sasa kamaliza doz ndio majib yapo negative Dr.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom