Kuna baadhi ya wazazi wanaishi kwa siri na maumivu makubwa. Wanatamani wawaombe watoto wao msamaha lakini hawajui waanzeje

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
284,479
738,930
Ni mpaka uishi hayo maisha ndio unaweza kupata hisia halisi za hii mada.

Hapa nazungumzia wale wazazi kwa sababu zozote zile waliwatelekeza watoto wao udogoni na kuja kuonana nao ukubwani.

Hapa nazungumzia wale wazazi ambao walitengena kwa sababu zozote zile na watoto kulelewa na mzazi mmoja ama mzazi wa kufikia.. Mzazi wa kambo.

Kuna unafuu kidogo kama huyo mtoto/watoto huko wanakolelewa wakapata mapenzi kama ya mzazi halisi. Kuna wachache wana hiyo bahati. Wengi wameambulia mateso, masimango na shida za kila aina
Kuna wazazi wa kike walipata ujauzito wakiwa shuleni..wakaacha masomo na kulea mimba na hatimaye kujifungua salama.

Baadhi walitaka kurudi na kuendelea na masomo hivyo kuwaachia ndugu zao walee mtoto mara nyingi ni mama dada au shangazi.

Makuzi ya mtoto katika umri wa awali ni muhimu sana kupata mapenzi ya wazazi wote wawili.. Mmoja ama wote wakiyumba mapenzi hayo huhamishiwa kwa walezi wanaowalea.

Kuna wazazi ambao walitengena wakiwa kwenye ndoa na watoto na baada ya hapo wakapata wenza wapya! Hapo watoto wanaenda kuanza maisha mapya mageni kwa mama/baba wa kufikia

Kuna tofauti kubwa sana kati mzazi halisi na mzazi wa kufikia.. Daima kuna kitu kitapungua. Kuna baadhi ya wazazi ambao walipata watoto kabla ya ndoa na sasa wakapata watu wa ndoa, hapo wengi waliwaacha watoto kwa ndugu ili wao wakajenge ndoa zao.

Kuna wazazi waliwatelekeza watoto kwa ndugu na wao kupotea kwenda kutafuta maisha. Scenario ni nyingi lakini mwisho wa siku watoto huwa wakubwa na kuja kukutana na wazazi wao halisi(kwa wale wenye bahati hiyo)

Hapo watoto huwa na maswali mengi sana ambayo wengi huwa hawayaulizi.. Na wazazi nao huwa na maelezo mengi sana lakini hawajui waanzie wapi. Ukaribu kati ya wawili hawa huwa hauna strong bonds.

Matokeo yake ni watoto kuwa na vinyongo na wazazi wao.. Huku wazazi wakiwa na maumivu ya ndani, wakitamani wajieleze na kuomba msamaha lakini hawajui waanzie wapi

Zile nyakati za shule wakati watoto wakifuatwa na wazazi wao. Zile nyakati za shule watoto wanaposimuliana furaha za nyumbani na wazazi wao. Kuna ambao hawana cha kusimulia na hubaki na maumivu na maswali mengi.. Huku nao wakitamani wangekuwa na wazazi wao.

Ni afadhali waambie wajue kwamba wazazi wamekufa kuliko waambiwe wapo Hai

Mifano ni mingi hata hapa JF..!
 
acha tu as long as God is exist lives continue
 
Na Bado Kuna wazaz baada ya baadhi ya watoto kuanza kufanikiwa kwa mfano kupata ajira , huanza kiwatengenezea matabaka watoto hivyo kuwatraumice watoto.
Kuna wale wazaz wakianza kusali kwa kina mwakalumbililo priest huanza kutengeneza matabaka kama vile kuanza kutengeneza matabaka naona ya baba na watoto hasa kwa kina mama na mwishowe kuvunja uhusiano wa watoto na wazaz
 
Good message.Kuna kisa kimoja cha ndugu yangu ambacho pia ni funzo kubwa hasa kwa maamuzi ya Kiutu uzima kwa ajili ya kesho ya watoto.Mke wa jamaa ni mtumishi mkubwa tu serikalini na jamaa alipotaka wakae kwa pamoja Kagoma katakata maana wako mikoa tofauti na uhamisho inawezekana.Alichoamua jamaa ni kuwa na watoto na anaowasomesha vizuri tu na akaapa hatooa mke mwingine atafia umoumo kwenye ndoa yake.Ukimuuliza anasema kwake watoto wana thamani kubwa kuliko mateso anayoitoa.Kumbe watoto wengi wanateseka kwa sababu ya ubinafsi wa wazazi wao.
 
Wanasema bora mzazi amkatae mtoto na sio mtoto kumkataa mzazi

Maana mtoto ndo alichagua wazazi wa kumzaa
Hakuna mtoto aliyechagua wazazi wa kumzaa.

Ingekuwa ni hivyo hakuna mtoto ambaye angechagua kuzaliwa na wazazi maskini, walala hoi, walevi, pangu pakavu tia mchuzi.

Wazazi walikuwa kwenye starehe zao za kupigana miti, ndipo watoto wakazaliwa bila kuchagua wala kupenda.

Hakuna aliyetaka kuzaliwa kwenye hii dunia, Tumeshtukia tu tupo kwenye dunia bila kuchagua.

Tunazaliwa bila kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe. Tunashtukia tu, tumeshazaliwa bila kuchagua.
Hii nilipata kuisikia Kwa MTU mmoja anaitwa Dr Ellie V waminian katika mafundisho yake ya kiroho .
 

Aiseee 😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…