kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 14,074
- 14,606
Tibu zote kwenye ligi zimefungwa na Yanga; ukiwa na akili mbovu utafirikiria Fountain Gates inaweza kuifunga Yanga. Inafahamika kuwa Simba waliweka matumaini yake kwa Foutain Gate kuisimamisha Yanga kwenye mbio zake za ushindi. John Noble alifungwa na timu bora kama vile wanavyofungwa magolikipa wote wa timu zote za ligi. Wamefungwa Simba, Azam na Singida wenye wachezaji ghali na fedha nyingi sana sebuse Foutain gates? Kama shida ilikuwa ni golikipa Noble kwanini wafungaji hawakufunga hata goli moja?
Hakuna golikipa ambae hawaogopi washambuliaji wa Yanga. Hofu ilisababisha Noble kufanya makosa kama yale. Wapeni Yanga sifa wanazostahili kupewa. Wachezaji hawahawa walioko Yanga wamecheza finali ya CAF Confederation, wametoka sare na Mamelods, wameshinda ngao ya jamii, ni watetezi wa kombe la ligi kwa mara ya 4 mfululizo, wameifunga Simba mara 4 mfululizo, wanaongoza ligi na wameingia nusu fainali ya CRDB cup. Ni punguani tu atafikiria Noble kapewa pesa ili afungwe kipumbavu kama vile. Kuna njia nyingi za kipa kufungwa kimazabe lakini huwezi kufanya kwa njia ile ya wazi kabisa; alizidiwa tu.