Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

Hahahaha we jamaa umewaza nini? Hivi huyo huyo kijana akimaliza hizo hatua zote akijibana akaanzisha hospital ukamwambia atoe ajira bila interview unadhani ni rahisi kiasi hicho.

Chukua process zote mtu anapitia hadi taasisi kama hospitali inasimama then unasema atoe ajira kwa graduate tena fresh from school bila interview 😂😂😂.

Labda tunatofautiana kwenye kuelewa maana ya interview. Kwa ninavyofahamu interview is more than academic certificates and maana huwa kuna written na oral pia na hata CV ingekuwa na Academic qualifications tu kama wangefikiria kwa style yako.
 
Mkuu a Doctor is a Healer kuna jinsi ya kumwambia mgonjwa ili a feel good huwezi kuja unamwambia mgonjwa ana ukimwi au cancer au ana siku tatu za kuishi huku unavuta fegi na kuchekelea au unatangazia watu bar kwamba fulani ana gono....

Ngoja nikupe Qoute from Person of Interest huenda ikakuonyesha what I mean....

Sameen Shaw: I watch the others. I watch the fear creep into them. I watch them make mistakes, and you think these feelings that I'm lacking make them better? You'd really rather have one of them working on you instead of me?
QMI Manager: Yes. Because if If the only thing motivating you is technical mastery, when one of your patients needs you the most, then this job just might start to bore you. That's the difference between fixing and healing. You have a brilliant mind, Sameen. And you're very gifted. But you'll never be a doctor.
Madaktari wameyapitia hayo yote ndio maana wanapewa leseni na kula kula kiapo cha Hippocratic.
 
Boss iko wazi uliishia la saba B tena ya chini ya mwembe😅
Naona umegeuka mpiga ramli kujua nimesoma mpaka la ngapi kupitia internet character called Wyatt Mathewson

Sikujua kama wewe ni mganga wa kienyeji

Kupitia internet nickname u can know exactly elimu ya huyo character?

TZ hakuna madarasa,kila mtu kasomea chini ya mwembe,naona huoni kundulo!
 
Wanyoosheni kwenye usaili huko maana mlikuwa mmezidi,
Interview ni kupata right person 😀😀 unakuta dokta wa sasa anaweka mkeka (both team to score) kwanza then anaingia leba kuzalisha mmama.
Na ma ticha hivyo hivyo una kuta ka ticha ni kasela kuliko wanafunzi 😀😀 vyeti unakuta ni A tu maadili ya kada yake ziro😀😀
 
Huna unachojua ,Madokta ni wengi sana sikuhizi
Hujui chochote, Shirika la Afya duniani (WHO) linapendekeza katika nchi uwiano wa daktari kwa mgonjwa uwe ni daktari 1 kwa wagonjwa 1,000 wakati Tanzania uwiano ni daktari 1 kwa wagonjwa 20,000.
 
Madaktari wameyapitia hayo yote ndio maana wanapewa leseni na kula kula kiapo cha Hippocratic.
Na hicho kiapo kinasema personality does not matter... ? By the way kabla hatujafika mbali what is personality...; kwa huyu mdau aliyeleta huu uzi anaonekana kwamba ni hubris..., which is can be very dangerous for a healer....
 
Mimi naona sababu kubwa kuwafanyia watu wa afya hasahasa MDs ni kutaka kujua walio na utayari wa kazi. Wengi wamekuwa wakipangiwa kazi chini ya TAMISEMI sehemu za mbali na wamekuwa hawaendi. Hii husababisha serikali kuingia kwenye database na kuajiri madaktari wengine tena

Ukiona mtu katumia gharama zake kwenda kufanya interview labda Mtwara huko au Kigoma ujue huyo yupo tayari kufanya kazi sehemu husika

Kwahiyo kikubwa hapo ni kupima utayari wa wahusika. Na ndivyo nilivyo tonywa na kiongozi mmoja wa utumishi
Wewe angalau unaweza kuwa na theory yenye mashiko na kueleweka.
 
Unaongea wewe,mimi ndio mwenye hospitali,unataka nifate utakacho wewe?

Kwahiyo A ndio amri ya kutuamrisha wenye taasisi kwa lazima tukuajiri?

Una A lakini jambazi na evil,nikuajiri kwenye taasisi yangu kivipi yaani?

Mali yangu,unataka uje kuniletea ulazima eti ulipata A?

Fungua taasisi yako utafanya utakalo,who cares!
Kama unataka kujua background ya mtu katika masuala ya usalama mwambie akuletee police report sio hizo interviews za kupoteza muda.

Halafu kuwa na Hospitali yako haimaanishi kwamba unaweza kuwa unaindesha katika mazingira fair na yenye mashiko, unaweza kuwa ni mjinga unayemiliki Hospitali au ni Hospitali iliyopo katika mazingira ya hovyo yanayoku favour mfano nchi inayozalisha idadi kubwa ya madaktari kuliko uwezo wake wa kuajiri kwa hiyo na wewe unanufaika na huo uhovyo.

Pia hospitali binafsi tofauti na hospitali za umma lengo kubwa na kuu ni kufanya biashara hivyo inawezekana ukawa unahitaji daktari ambaye ni mtu wa biashara zaidi(business minded) kupata/kuvutia wateja wengi zaidi kwenye hospitali yako.
 
Just imagine kijana kapata division one ya 7 au 10 form four kaenda high school kupiga PCB. Kapambana sana kachakaa kajitesa kajinyima kapata division one form six ya point tatu au tano.

Kaaply Muhimbili University kapitia mchujo katoboa akaanza masomo ya udaktari.

Kasoma miaka mitano bila kudisco tena kwa mateso makubwa bila kula bata mpaka kamaliza chuo.

Kabla hajaingia intern kafanyishwa mtihani wa MEDICAL COUNCIL OF TANGANYIKA katoboa kaanza interniship.

Kapiga intern kwa mwaka mmoja kisha kamaliza kisha kapigishwa pepa lingine la MCT katoboa.

Kasajiliwa na kutambulika kama MEDICAL DOCTOR na MCT.

Kijana huyu wa kitanzania aliyesoma kwa kujinyima na kujitesa tangu kidato cha kwanza leo hii anafanyishwa interview tena written interview sio prectical interview ili iweje?

Huyu kijana akikosa nafasi mnajua stress atakazopata mtaani na jamii inayomzunguka?

Hiyo michujo yote alopitia akipata ajira mnamlipa milioni moja na laki mbili ukitoa makato anabeba laki tisa bado mnampigisha interview ya nini sasa?

Hamuoni kama mnakatisha tamaa vijana waliopo shuleni na vyuoni?

Wadau
Ni huzuni kwa kweli.
 
Mimi ni muumini mzuri wa meritocracy.

Interview ziwepo na ziongezwe mawanda mapana .

Ndio maana hata natamani katiba ibadilike mawaziri wasitokane na wabunge.

Waziri nafasi ziwepo wazi watu wapply , kisha wakafanyiwe vetting live bungeni ndio wapitishwe itasaidia vingi sana.

Nimeshangaa tu nilipoona post moja humu kuwa usaili ulipangwa ni online halafu watu wamezuiliwa sababu hawana vitambulisho hapo ndio sijaelewa tatizo hasa ni nini , maana usaili wa online utahitaji kifaa chako , sehemu tulivu na internet tu.
 
Sasa mkuu kama nimekuita kwenye shughuli yangu ambayo nina vigezo tofauti (labda kwangu ukarimu na personality matters kuliko vyeti) sasa takupima vipi bila kukufanyia interview....

Kama vipi unaona wewe ni gwiji huwezi kufanya interview basi nenda kule pasipo interview au fungua shughuli yako ambayo utajiajiri kwa kutokujipa interview...

When in Rome do as Romans....

Ila that said nahamia pia kwa upande wa Serikali..., Ni upuuzi usio na kifani kuwa na madaktari mitaani hawana kazi wakati kuna uhitaji wa wauguzi (wauguzi hawatoshi) hizo pesa mnazonunulia V8 bora mpande daladala na kuajiri wauguzi...
Umeongea vizuri lakini.......
 
Kuna kiumbe mmoja huko huko kwenye medicine yenu aliitwa mahali kwenye interview baada ya kufika akapewa karatasi na peni akaambiwa aandike application letter akiwa mle mle ndani kwa kuwa aliyopeleka imepotea lkn uhalisia walikuwa nayo.

alitokwa na jasho pale pale maana alipewa kipimo ambacho sijui waliomfanyia hivyo waligundua kitu gani.
 
Kama unataka kujua background ya mtu katika masuala ya usalama mwambie akuletee police report sio hizo interviews za kupoteza muda.

Halafu kuwa na Hospitali yako haimaanishi kwamba unaweza kuwa unaindesha katika mazingira fair na yenye mashiko, unaweza kuwa ni mjinga unayemiliki Hospitali au ni Hospitali iliyopo katika mazingira ya hovyo yanayoku favour mfano nchi inayozalisha idadi kubwa ya madaktari kuliko uwezo wake wa kuajiri kwa hiyo na wewe unanufaika na huo uhovyo.
Hivi mkuu unajisikia unachoongea kweli?

Madaktari kama wewe ndio hatuwataki kabisa

Yaani wewe unadhani naweza anzisha taasisi nikaajiri specialists ikafanya kazi mpaka kiazi kama wewe ukaja kuomba ajira halafu bado nikawa eti "mjinga"?

Kwanini unaomba kazi na unajifanya una "akili"?

Kwanini usifungue taasisi yako wewe mwenye akili nyingi?

Unakuja kuniomba kazi kwenye taasisi yangu huwezi nipangia cha kufanya,kama unataka kunipangia ni heri usije kuomba kazi

Kwanza maliza shule uombe kazi serikalini wakulipe laki 8 halafu uje kuombe deiwaka huku private halafu uje kwangu halafu uniambie "sitaki interview" nakutwanga makofi sawa sawa on top of that nakuweka ndani muda wa kutosha maana huna financial muscle yeyote

Madaktari TZ ni watu waliochoka kiuchumi kama waTZ wengine,kwahiyo usijitie kuna somekind of superpower u have to run over systems owners

Mpo delusional,bado hamjakaa sawa,ngoja upigwe huko Tandahimba utibu wakulima wakuharishie vizuri then ulete kende Dar useme "sitaki interview"
 
Kada sensitive kama Udaktari lazima INTERVIEW nilikuwa nashangaa sana unaajiri vipi bila kuwapima unaowaajiri.?

Procedures za HR lazima ufanye interview ili upate kile unachotaraji.

Pia, background checks and vetting ni muhimu sana.. kuna taasisi nafanyia kazi kuna kitengo/watu maalumu wa Vetting na Vetting ni swala endelevu.. ukiwa upo kazini vetting inaendelea.

Tusiweke ubinafsi ktk hili swala. interview ifanywe tena ile INTENSIVE hasa.
 
Back
Top Bottom