~**~ kumbatio la mwenye makosa ~**~

Ni hadithi nzuri,mtiririko wako wa maneno na visa unaonyesha ni jinsi gani ulivyo mtunzi mahiri,mara nyingi sisi watu tulio addicted na novels tuna tend kutamani kuishi maisha yaliyopo mle,au kuiga character za mtu fulani ambaye mwandishi amemuelezea kwa ustadi mkubwa.So kutokana na hilo naendelea kutamani kama ungetunga hadithi zenye visa vya kisiasa,kijangili,kiuzalendo(i know ur good on that),Ili pia utujenge kwenye uzalendo,kama wakina Robert Ludrum,Ben Mtobwa,Issa tuwa,Msiba e.t.c.

jamani.. si ndio kuna kisa kinaitwa "uso kwa uso na kamanda".. usidhanie ni kisa cha mapenzi....
 
Naomba niweka nami mchango wangu kuunga mkono wale wote waliompongeza na kumshukuru mwenzetu MKJJ kwa kazi kubwa aliyoifanya tena kwa kipindi kifupi kutuletea riwaya.

Aidha napenda kusema kwamba kazi hii imetuonyesha kwamba tunao watunzi wazuri miongoni mwa jamii ya Kitanzania kwa viwango vilevile tulivyovizoea kwa wenzetu wa magharibi.Hongera Mh.MKJJ.

Baada ya kutoa pongezi, naomba nichangie yafuatayo kama tafsiri au mafunzo niliyoyapata kwenye kisa hiki:


Mafundisho - Kisa chochote kinachoandikwa, ni ama reflection ya maisha yalivyo au uwezekano wa mambo yatakavyokuwa endapo kutokuwa na hali kadha wa kadha. Nimeweza kujifunza mambo yafuatayo -

Hakuna masika yasiyo na mbu au siyo kila king'aacho ni dhahabu.

Maisha ya Tina na mumewe Boss KWA NJE NADHANI YANAONEKANA NI RAHA NA WATU HUENDA WAKATAMANI KUWA NA MAISHA kama yale.Laiti wangejua! Nadhani ndoa nyingi zina hali kama hii hasa kwa wale ambao maisha yanaonekana kuwanyookea kifedha, cheo n.k.

Ni mara nyingi utasikia watu wakisema familia fulani wanaishi maisha wayajuayo wenyewe... hakuna mawasiliano, hakuna mshikamano, hakuna upendo. Baba yuko kivyake, mama kivyake, watoto nao wakiona hali hii huanza kufanya watakavyo! Ikifikia hapo hali ya ndoa ni mbaya na hatari nyingi huweza kutokea. Wana ndoa wataanza kutafuta faraja kwingine kama alivyofanya Tina.
Tukimwangalia Tina tunapata maswali mengi sana.
Kwanini mjamaika na siyo mtu mwenye wadhifa kama mumewe?
Kwanini hamsamehi mumewe|?
Huyo mume mbona ni kama hafanyi jitihada za nguvu kurekebisha hali ya mahusiano na mkewe?
Je mume alikuwa na sababu yeyote kumsaliti mkewe na binti msaidizi wa nyumba wakati tumeonyeshwa kwamba maisha yao ya unyumba yalikuwa mazuri mno na kila mmoja akimfurahi mwenzie?
Ni wanawake wangapi hujitoa kwa waume wao kwa kiwango cha juu sana ili kuwafanya waume wasiwe na tamaa zisizo na sababu lakini bado waume hawatulii tatizo liko wapi?
Je mke alikosea wapi? na kama kuna makosa mume anapaswa kufanya nini ili mke ajue kuna upungufu sehemu fulani?

Tukija kwa mjamaika -
Ni "wajamaika" wangapi wanajikuta wakiziba mapengo ya akina Tina na Boss?
Nani wa kulaumiwa|?
Mwisho wa mjamaika na Tina huwa ni nini katika maisha ya kweli/halisi?

NINA MASWALI MENGI SANA lakini niishie hapa


Theme ya Kitabu - nadhani kuna watu wamesoma kama riwaya ya kuburudisha.Binafsi nimeisoma kama riwaya iliyotumia MAPENZI kuelezea kilio cha wanandoa wengi na mahangaiko yanayo wapata wana ndoa - wanandoa wanahitaji msaada wa ziada ili ndoa zisimame.
HUKU NI KUJITAMBUA/KUJIFAHAMU -

Wewe mama/baba/kaka/dada unajitambua KWA kiwango gani?
Je, uko mkweli kwa mwenzio? unajali kujua mwenzio anasumbuliwa na nini moyoni mwake?



Njia bora ya kufikisha ujumbe
Siku zote na hasa kwa watanzania, ukitaka watu wasome vitabu vyenye ujumbe mzito, tumia mapenzi.Ukitumia siasa utawapata wachache sana! Ndivyo watanzania walivyo na ndio maana magazeti ya udaku husomwa zaidi na kuuza zaidi kuliko maandishi magumu au mazito.
Ni ukweli hata kama kuna watakaoona tofauti.



Jumbe zilizojificha -
Kuna mengi yamejificha kwenye riwaya nzima
1. Gonjwa la UKIMWI -
Gonjwa hili siyo tishio sana kwa mahusiano! Watu watahusiana tu hata kama wanajua kuwa kuna hatari ya kupata ukimwi. Boss na Hausigeli sijui kama walitumia condom.Na ndio maana maambukizi mengi Tanzania kufuatana na takwimu ni baina ya wanandoa kuliko watu wasio na ndoa. Mjamaika hakushirikiana kingono na Tina bila kinga! Tumeonyeshwa pia matumizi sahihi ya "Kinga hii", na hili ni tatizo kwa watu wengi wanaodhani wanajikinga kumbe wanajipa hope tu.

2. Ugumu wa kusamehe katika ndoa

Wanandoa wengi hasa akina baba hudhani kuwa wanapokamatwa wamecheat basi msamaha ni automatic! haiko hivyo ndugu zanguni akina kaka. Msijidanganye. Wanawake wanakaa kimya tu kuepusha shari lakini msipofanya jitihada za kweli na dhati mjue maisha na uhusiano upo mashakani.

Ogopa mwanamke aliyejeruhiwa kisasi chake usipime! Mjue jinsi mnavyojisikia pale wake zenu wanapocheat na wanawake wanajiskia hivyo hivyo.

3. Unafiki kwenye ndoa -

Wanasiasa au watu wenye nyadhifa ni wagumu kuachana siyo kwa vile wanapendana sana bali ni kwa vile itaonyesha kushindwa kumudu uongozi mdogo ngazi ya familia na hii inapelekea kuonekana hafifu au unfit kwa madaraka makubwa. Hapo utaona wanasiasa na wengineo wakienda hadharani na wake zao waliovaa tabasamu la plastik! Yote haya ni kulinda mkate wao na siyo ndoa. Wengine hawaachani kwa sababu wamewekeza mno kwenye ndoa kwa maana ya muda na hata rasilimali nyingine.



Nini kifanyike? sina jibu. Poleni kwa kusoma mchango mrefu.
 
Aaaaah.....WoS....brevity is the soul of wit bana... Ijumaa yote maneno mingi hivyo ya nini bana?
 
NN,
Hata wewe unakataa kusoma maandishi marefu! I know u r kidn. No wonder MKJJ akawaleteeni kwa kipimo- chapter by chapter.
Lakini si nimekutakeni radhi?
 
NN,
Hata wewe unakataa kusoma maandishi marefu! I know u r kidn. No wonder MKJJ akawaleteeni kwa kipimo- chapter by chapter.
Lakini si nimekutakeni radhi?

Don't worry ma...I was just slipping in some levity...nothing wrong with cracking a joke or two on Friday...Jah bless
 
M.M.M umefanya haraka kuifikisha mwisho, nilidhani bado hatujafikia katikati kumbe ndo imeisha. Asante kwa hadithi nzuri.

Pendekezo langu: mpenzi aliyekosewa awe wazi kusema kama atasamehe au la, kama hawezi kusamehe bora separation ili kieleweke.
 
Nemesis.. kwenye stori.. it will take a twisting turn ambayo inaweza kuoneshwa kwenye movie ya "misery" tu ya Kathy Bates..
 
Thanks MMwanakijiji....I totally enjoyed it and I liked the ending....
 
MJJ nakushukuru sana kwa ubunifu wako wa njia ya kuichangia JF nafikiri hii itasukuma hili gurudumu mbele. Max nitawasiliana punde niweke fungu kwa hiyo ifuatayo :drum:
 
Back
Top Bottom