Magezeti karibu yote ya siku ya leo tarehe 11/04/2017 katika kurasa za mbele yametawaliwa na habari kuu mbili ambazo ni kuhusu tishio la kutekwa kwa wabunge 11 na habari ya kutekwa kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
Hata hivyo,katika magazeti yote ya kila siku niliyoyaona ni gazeti la Uhuru tu ndio ambalo halijaripoti habari yoyote kati ya hizo habari kuu mbili za leo.
Sasa sijui pamoja na uwepo wa Waziri wa Habari na Utamaduni uwepo huo nao bado si issue!
Anyway,wanajua wenyewe.
Kingine nilichogundua ni picha ya waziri Mwakyemba na hata alichokisema kupotezewa na magazei mengi katika kurasa hizo za mbele isipokuwa gazeti la Majira tu ndio limeonyesha uwepo wake katika magazeti niliyoyaona.