Kulikoni Dkt. Magufuli kutohudhuria karamu ya Mabalozi Ikulu?

Nimeshangazwa kidogo kwa kitendo cha Rais Dkt Magufuli kuwaandalia karamu ya kuukaribisha mwaka mpya, mabalozi na Maafisa wa kimataifa waliopo nchini na kisha yeye mwenyewe kumtuma waziri wake wa mambo ya nje kumwakilisha.

Kwa maoni yangu naamini hili ni kosa la kiufundi hasa ikizingatiwa kuwa Magufuli ndio ameanza tenure yake kama Raisi na hivyo angepaswa kutumia fursa hiyo kikamilifu ili kujenga taswira yake vema kimataifa kupitia kile anachokiamini na kusimamia.

Taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari haikusema ni dharura gani aliyokuwa Mhe Rais ilihali yupo nchini.
Aidha:

aliogopa kususiwa mambo ya znz
au anahitaji kwenda chuo cha kidiplomasia kidogo
sugu alimwambia take a flight man ! woga fulani hivi
 
Development studies ndio inafundisha Sadam ni Rais wa wapi? Nonsense
Huyu jamaa hajaacha hii tabia ya tu kukimbia kimbia kila kitu. Namkumbuka shuleni alikuwa anakimbia midahalo hata ile ya Development Studies! Ndio maana hadi leo anajua yeye anajuaga ya kwamba Sadam ni Rais wa kuwait!
 
Alaaah!!!ulipiga naye kitabu nn Mkuu??
 
Mambo yanavyoenda huko Zanzibar na katazo walilopigwa mabalozi hata kutembelea shule na zahanati sio sifa njema,kuepuka maswali na mihemuko ni bora kukaa pembeni!!!
Sasa mkuu wewe unadhani kwa yeye kukaa pembeni kukwepa maswali au mihemuko itasaidia kumaliza haya matatizo au jipu ndo litazidi kuwa kubwa?
 
Haha hafla imefanyika Ikulu na Magufuli hajaudhuria alaaa kumbe magogoni ni kubwa kiasi hiki ??

Ila hili ni tatizo Mkuu ,wacha tuendelee kuona
 
Huyu jamaa hajaacha hii tabia ya tu kukimbia kimbia kila kitu. Namkumbuka shuleni alikuwa anakimbia midahalo hata ile ya Development Studies! Ndio maana hadi leo anajua yeye anajuaga ya kwamba Sadam ni Rais wa kuwait!
Alikimbia kila kitu ndiyo maana akafika ikulu. Wewe uliyewahi kila kitu, bado tunaburazana humu.
 
Back
Top Bottom