Nakubaliana nanyi kuwa suala hili lilihitaji uchunguzi kubaini ukweli kwa kuwa naamini kila mhusika anaweza akawa amechangia kwa kiasi fulani katika tatizo lililojitokeza. Nilichotaka kuwakumbusha ni kuwa kulingana na sheria za utumishi, Rais ana mamlaka ya kumstaafisha/kumfukuza mtumishi yeyote pasipo kulazimika kutoa sababu. Kwa hiyo, kisheria, ana mamlaka hayo ingawa ukweli unabaki kuwa palihitajika uchunguzi ili siyo tu haki iendeke bali ionekane ikitendeka.