dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,421
- 1,985
Kuna huu Uongozi wa Kifalme,
Inasemekana hata Afrika zilikuwepo Tawala lukuki zilizokuwa na nguvu za Himaya za Kifalme na kwingineko Ulimwenguni pia.
Kwa Afrika, Tawala za Kifalme ingawa unaaminika kuwa zilikuwa nzuri zikiishi kwa Utulivu na amani zilikuja kuvurugwa na kutokomezwa na 'Waliojivika' sifa ya ustaarabu na kutenda kila hila mwishowe tawala hizo zikadondoka wakaleta mapokopoko yao ya Demokrasia za kinafki.
Kwa Unafki na kwa sababu za wazi zilizokusudia kunyonya kila kilicho chema na kuacha visivyopendeza tu wanafki hawa (Waingereza) wakabakisha chembechembe tu za kuwa kulikuwepo na utawala huo Afrika lakini wakiwa wameshavuruga kila kilichokuwa kinaenda vyema awali.
Hata hivyo, huko Uingereza kabla yao kusambaza vibaraka wao Ulimwenguni kufanya hila. Utawala wa Kifalme ulikuwepo miaka mingi nyuma na bado unaendelea kuwepo. Ijapokuwa utawala huu upo Kisheria, Malkia au Mfalme ni cheo kinachoitwa 'Shereheshi'.
Viumbe hawa wachache (Kiongozi wa Familia ya Kifalme) ingawa yapo majukumu yake Kiserikali lakini kwa unafki mkubwa inasemwa kuwa wakifanya shughuli hizo za Kiserikali hawalipwi lakini kumbuka upo mfuko maalumu unaotokana na Pesa ya walipakodi unaoihudumia Familia hii inapata kila uchao. Na si Pesa ya kitoto.
Wakati huohuo Familia hii inaogelea katika ukwasi mkubwa na mpana na ambao umechumwa zama na zama.
Na waingereza raia wa kawaida wakibung'aa miaka yote.
Najiuliza, hawa jamaa (WAINGEREZA) si ndio wanaohubiri siku zote swala la Demokrasia?
Kwanini wasishinikize iwapo ni muhimu kuwepo kwa aina hiyo ya Mfumo kwao, kwanini Ufalme isitafutiwe namna nyingine ya kupatikana ili kuwepo na usawa badala ya watu wachache wale kurithishana?
Itakuwa Wamerogwa vibaya sana aisee.