Kukosea kupiga simu kwanini iwe kwa watu wa kabila moja?

Sozo_

JF-Expert Member
Jun 12, 2022
606
925
Mimi sio mfuasi wa kuponda makabila, nawapenda wote, hata mwenzi wangu sio wa kabila langu. Lakini najiuliza kwanini kila ninapopigiwa simu ya kukosewa huyo mtu anakuwa msukuma, kama sio mwanaume atakuwa mwanamke.

Nawajuaje? Mara nyingi husalimia kikwao, ama kuita majina yao, tunaposhindwa kuelewana huwa nawaambia wamekosea kupiga.

Wengine watarudia mara mbili au tatu na wakati umemwambia amekosea.
Hoja yangu ni kwamba kwanini wawe wasukuma tu? Ina maana nchi hii ina idadi kubwa ya Wasukuma? Au nini ndugu zangu?
 
Sijui kwanini aisee..wasukuma na Waha sijui kuna tatizo gani huko,halafu kingine hata zile namba ambazo zinabadilishwa na kupewa mtumiaji mwingine baada ya mwenye nayo kuitelekeza nazo pia wanazielekezea huko si mara moja nakutana na kesi hizi
 
Kumbe tupo wengi tunakutana na hili, wenye kuelewa watusaidie. Au kuna watu wanajifanyisha?
 
1662651464879.jpg
 
Back
Top Bottom