Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,049
Nilimsikiliza Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, hapo jana Katika kile alichokiita ni kutoa ufafanuzi na kilio cha wananchi kuhusu tozo nyingi wanazokatwa kupitia miamala ya simu na sasa kupitia Benki.
Katika maelezo yake alikiri wazi kuwa ni makosa kumkata mwananchi tozo, zaidi ya moja, Katika chanzo kimoja!
Kwa kuwa tozo hizo zilipitishwa na waheshimiwa wabunge wetu, ambao ni wa chama kimoja pekee cha CCM, isipokuwa kwa Mbunge mmoja wa kichaguliwa wa Chadema, nilichogundua ni kuwa hatuna wabunge makini wa kuhoji kile wanacholetewa na Serikali na kuamua kila kinacholetwa na Serikali, hata kama ni cha kuwaumiza Sana wananchi, wanachofanya wao ni kukipitisha tu, bila kujali madhara ambayo huyo mwananchi anayemwakilisha atakavyoumia.
Mwigulu pamoja na Mawaziri wenzake pia wameeleza namna hizo tozo zinavyofanya Kazi za kujenga vituo vya afya.
Niwaulize tu hao Mawaziri wetu wa CCM, hivi hii nchi ilikuwa ikiendeshwaje huko siku za nyuma, kabla ya kuanzisha hizi tozo kandamizi zilizoanzishwa ndani ya utawala huu wa awamu ya sita?
Hiyo ni hoja dhaifu Sana, iliyotolewa na hao Mawaziri, kwa kuwa nchi yetu ilijenga vituo vingi vya afya bila ya kumkamua mwananchi kwa tozo hizo kandamizi hapo siku za nyuma
Tatizo kubwa ninaloliona Mimi kwa nchi yetu hivi sasa ni kukosa Katiba ya nchi, inayoendana na mfumo wa vyama vingi vya siasa na badala yake tumeendelea kukumbatia Katiba ya nchi ya mfumo wa chama kimoja!