Bashite analindwa na sizonje, wote wawili wamelewa madaraka
Apelekwe mahakamani na wenye ushahidi sio kutulisha matango pori .
Watanzania tufikie hatua tuione mahakama kama ndio mahali pa kupeleka madai yoyte dhidi ya jinai sasa hii hali ya kuwa tunalambana kwa media wakati hakuna mshitaki sidhani kama ina tija kwa taifa.
Miaka zaidi ya nane alituhumiwa Mzee Lowassa pasipo na mshitaki mahakamni lakini watu wale wale waliotuhumu wakaja kumsafisha kana kwamba hawahusiki kabisa.
Tufikie hatua tuwe tunatumia njia sahihi kuthibitisha uhalali wa madai yetu ya msingi .
Ipo siku hatutaaminika hata na mapunguwani kwa kuishia kutoa tuhuma bila kufuata utaratibu sahihi.
Tunao mawakili wengi tu kwanini hii issue ya public kama raia mwema anasema anao ushahidi thabiti mawakili wasijitolee kumshtaki Makonda?
Wanamwachaje mtu mmoja analalamika na ushahidi anao fully
Halafu mtu huyo bado anadai yeye anahitaji kuombwa msamaha tu...Jamani kweli kwa makosa ya wizi wa cheti kelele zote ni ili uombwe msamaha tu?
Mawakili tusaidieni kuondoa kadhia hii.
Imetosha sasa hizi kelele.
Tuthibitishieni.
Vyeti vya sifuri watu wanavyo hapa bongo tena wanachukuliana tu.