Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,948
- 32,056
KUJUA LEO YAKO UNAHITAJI KUJUA JANA YAKO
Nimeweka picha nne hapo chini tati ni za maandamano ya wananchi yakiwakilisha makundi makubwa mawili katika jamii ya Watanzania.
Picha ya kwanza ni ya Rais wa TANU Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa nje ya Ukumbi wa Karimjee akiwa anawaonyesha wananchi bango linalojieleza wenyewe kuwa Tanganyika itakuwa huru mwaka wa 1961.
Hii ilikuwa baada ya mazungumzo ya TANU na Waziri wa Makoloni Iain Macleod.
Mji wa Dar-es-Salaam ulilipuka kusikia kuwa mkoloni amekubali kutoa uhuru mwaka wa 1961.
Maandamano makubwa yalitoka Viwanja Vya Karimjee hadi TANU HQ New Street.
Ilikuwa furaha kubwa.
Katika picha ya kwanza aliye kulia ni Sheikh Issa Nasir kutoka Bagamoyo.
Sheikh Issa Nasir nimeelezwa alikuwa "Mlinzi Maalum" wa Mwalimu Nyerere.
Sheikh Issa Nasir alikuwa pia Mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU.
Hapo pembeni ya Mwalimu Sheikh Issa Nasir yuko na jeshi lake lakini huwezi kuwaona askari wake.
Mpashaji wangu habari kaniambia kuwa wakati wote Sheikh Issa Nasir alikuwa hakai mbali na Nyerere.
Taarifa hii nilitaka kuthibitisha kwa kuangalia picha ya Baraza la Wazee wa TANU iliyopigwa mwaka wa 1957.
Naam katika picha hii Sheikh Issa Nasir amechutama miguuni kwa Nyerere.
Pembeni ya Sheikh Issa Nasir ni Bi. Mugaya Nyang'ombe, mama yake Nyerere.
Katika picha hiyo wanaonekana Rajab Diwani na Oscar Kambona pembeni ya Nyerere.
Sasa tuje kwenye picha ya maandamano ya wanaopinga Waarabu kuwapo Port.
Nimeitazama sana picha hii na nyinginezo za maandamano kwa makini sana na kwa muda mrefu.
Nakuomba na wewe msomaji ufanye hivyo.
Nini unachokiona hapo?
Nimeweka picha ya tatu ya maandamano yaliyofanywa na Waislam kupinga kile Waisla walichodai ni dhulma na hujuma ya Baraza la Mitihani (NECTA) dhidi ya shule za Kiislam.
Maandamano haya yalifanyika mwaka wa 2012.
Baada ya maandamano haya Waislam kama sehemu ya jamii hawajaandamana tena.
Kuna historia ndefu kuhusu NECTA lakini lililo wazi ni kuwa toka kuanzishwa kwake halijapata kuwa na uhusiano mzuri na Waislam.
Mengine yanayosemwa kuhusu NECTA siwezi kuyaeleza hapa.
Maandamano haya mawili yote yana waandamanaji wake makhsusi.
Waandamanaji wa kuwakataa Waarabu wameonekana na sasa wanatambulika ni watu gani na wapi wametokea.
Waandamanaji wa kupinga dhulma za NECTA dhidi ya Waislam halikadhalika wanafahamika.
Ukisoma mabango ya makundi haya mawili yaliyoandamana utaona ni kwa umbali gani makundi haya yalivyoachana.
Kundi moja linazungumza na serikali kuhusu "Waarabu" kukabidhiwa Dar Port.
Kundi la pili muongo mmoja uliopita liliiitahadharisha serikali kuhusu dhulma dhidi yao katika kutafuta elimu.
Dr. Joyce Ndalichako ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa NECTA.
Baada ya maandamano ya Waislam dhidi ya NECTA aliondolewa lakini hakuwa mbali na Wizara ya Elimu.
Alirejea kama Waziri wa Elimu mwaka wa 2015.
Serikali haikujali shutuma dhidi yake za kuhujumu Waislam katika elimu.
Ingekuwaje leo kama Sheikh Issa Nasir na wenzake wangekuwa hai na wakashuhudia haya yaliyopo leo?
Taifa linajifunza nini katika haya maandamano mawili.
Kitu gani kimewafanya wale waandamanaji dhidi ya NECTA mwaka wa 2012 kujiweka mbali na maandamano dhidi ya "Waarabu" wa Dubai?
Mwenye macho haambiwi tazama.
Baada ya maandamano ya NECTA serikali ilipitia upya matokeo ya mitihani na ilikiri kuwa uonevu ulifanyika na wanafunzi wengi wa Kiislam wakapata haki yao.