Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 22,171
- 23,647
Ng'ang'ana, simamia na kuongoza wizara, mamlaka au taasisi ulopewa kuisimamia kwa weledi, maarifa, bidii na ujasiri mkubwa, bila kubabaika, wala kuzingatia shinikizo ambazo hazina umuhimu wowote hasa kutoka kwa wanasiasa waliofilisika hoja na kupoteza uelekeo. Muhimu zaidi zingatia sheria, kanuni na taratibu za kikatiba zilizopo.
Ni muhimu zaidi kutafuta majawabu muafaka ya changamoto zinazoibuka na kuamsha hisia miongoni mwa jamii. Ni jambo la maanaa zaidi kusimama kidete, kusimama imara na kutafuta suluhu za kudumu kwa ufanisi unaostahili, kwa changamoto yoyote inayoibuka kwasababu, huo ni miongoni mwa wajibu wako wa msingi na ndiyo maana umepewa dhamana hiyo.
Hukupewa nafasi hiyo ili ujiuzilu likitokea changamoto. Na ikiwa hivyo watajiuzulu wangapi sasa?
Usidanganyike, chapa kazi bila kujali nani anakupenda au anakuchukia. Hilo ni jambo binafsi.
Jukumu la kuleta mageuzi, mabadiliko, na kutatua changamoto na kuongeza ufanisi katika utendaji wa taasisi au mamlaka ulopewa ni lako, kua mbunifu, onyesha njia.
Hakuna haja ya kuiga vitu ambavyo havina maana yoyote, eti kwasababu fulani na fulani waliowahi kujiuzulu, wakati huenda walioshindwa kazi, hawakua tena na fikra mpya wala mawazo mbdala ya kuongoza na kusimamia dhamana walizipewa.
Kujiuzulu ni kukimbia tatizo, kujiuzulu ni kushindwa kazi, kujiuzulu ni udhaifu na unyonge katika kupambana. Hapana kufanya kosa hilo la kukata tamaa unapokutana na changamoto nzito hata katika maisha ya kawaida tu. Mpaka kieleweke.
Mungu Ibariki Tanzania