Kujiongezea sifa usiyokuwa nayo ili upendwe ni hatari inayomaliza vijana wengi

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Feb 4, 2024
342
916
Kujiongezea sifa usiyokuwa nayo ili upendwe ni hatari inayomaliza vijana wengi

Mahusiano ni mfumo wa kihisia hivyo ili uwe ndani ya mfumo lazima uwe na hisia ila ni hatari kubwa sana kulazimisha hizo hisia kiasi cha kujipa sifa usizokuwa nazo ili tu upendwe.

Kama haupo kwenye hadhi yake kukupenda hata ukijipa hiyo hadhi bado kuna siku utaumbuka na wewe ndio utabakia hasara kubwa za uharibifu.

Katika kutafuta sifa za ziada ili kupendwa watu wamejikuta kwenye haya matatizo.

1.MADENI SUGU ; Hapa watu wamelazimisha waonekane wenye pesa ili wapendwe hivyo wamekopa ili kununua vitu vitavyowatambulisha kama matajiri lakini ki uhalisia hawana uwezo huo sasa baadaye ugumu unabaki kwao kulipa madeni.

2.KUISHI MAISHA YA KUAZIMA HOVYO, Hapa ndio tunakuta watu wanaazima mpaka nguo za jeshi ili waonekane wanajeshi waweza kupendwa matokeo yake ni kukamatwa kwa kuvunja sheria za nchi, hapa watu huazima nguo , magari mpaka manukaoto ili wajiweke kwenye muonekano usio wao kwa lengo tu la kutafuta kupendwa.

3.UMASKINI: Vijana wengi hujikuta kwenye dimbwi la umaskini kwa sababu wanaishi maisha ya maigizo sana yaliyo nje ya uwezo wao ili tu kutafuta kupendwa, kwa mfano mtu hana ajira yoyote ila anaongopa kwa mpennziwe kuwa yeye ni Mwalimu sasa kitachofuata hapo ni kuanza kuishi hayo maisha ya Mwalimu kwa gharama kubwa.

4.WIZI : Katika kutafuta sifa usizokuwa nazo hatimaye mtu huanza kuiba ili apate vitu vitakavyomfamya aonekane mwenye hizo sifa , Kama tayari umemwambia mwenzako wewe ni Mwalimu utaogopa kubeba mchanga hivyo utaona urahisi ni kuwa tapeli na mwizi.

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Mitandaoni @Fikia Ndoto Zako.
 
Fake it till you make it.

#Hakuna ugonjwa mbaya ambao hauna tiba unaitwa REALNESS.
 
Back
Top Bottom